Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za Pongezi Mheshimiwa Anne Makinda kwa kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika salaam zake,Rais amesema,Spika Makinda amechaguliwa kwa sababu ya uwezo wake,uzoefu na umakini wake.“Ninakuahidi ushirikiano wangu katika shughuli zako za bunge na za kujenga nchi yetu kwa ujumla”Rais Amesema na kuongeza kuwa kuchaguliwa kwa Mama Makinda “Ni heshima kwa Chama Cha Mapinduzi, umejenga imani kubwa kwa wanawake na umewatia moyo na shauku ya kufanya kazi kwa ufanisi na ueledi katika jitihada zao za kushika nyadhifa mbalimbali za maamuzi.”Rais amesema na kumtakia kheri katika shughuli zake za kila siku.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu
Dar-es-salaam.
12 Novemba, 2010
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu
Dar-es-salaam.
12 Novemba, 2010
Huyu naye walewale anadhani hatujui nini kinaendelea? Sikio la kufa ....najua unaweza bania comment but msg sent
ReplyDeleteHaya wafalme njozi, mnaojua kila kitu. Nongwa nongwa zimewajaa, roho mbaya za kwanini, chuki zimewajaa, hamna lolote mnalojua zidi ya roho za kwanini! Eti mnajua kinachoendelea kazi redio mbao na uzushi usiokuwa na kichwa wala miguu!
ReplyDeleteBi Anne Makinda ndio keshakuwa Spika, mkinuna, mkilia shauri yenu. Tumewastukia na makundi yenu, hakuna cha nani wala nini wala sijui nani. Mmeula wa chuya mwaka huu!
Siasa yeyote sio kuzua maneno na mnapozua mnasababisha vurugu ndani ya Bunge”amesema mwanasiasa huyo aliyejiwekea historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Spika wa Bunge la Tanzania.
ReplyDeleteAmesema, anasikitika kwamba, kulikuwa na kashfa moja tu katika Bunge lililopita iliyohusu mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura kati ya Serikali na kampuni hewa ya Richmond.
“Pale zilitakiwa Richmond zaidi ya 10’ alisema Makinda katika moja ya kumbi za mikutano katika Ofisi ya Bunge mjini Dodoma na akabainisha kwamba, wakati mwingine wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani huungana kwenye suala kama hilo.
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo ila MCHELEA MWANA KULIA,HULIA YEYE mmewachekea hadi wanaanza kuwapangia safu!tutayaona mengi safari hii mi yangu macho tu.
ReplyDeleteWashika dau mnapaswa kutoa hoja zilizo wazi badala ya vipande vya mipasho na maandishi ya khanga. Suala muhimu, Mh. Anna Makinda MB ameukwaa uspika kwa wingi wa kura mara tatu zaidi ya mpinzani wake, au kulikuwa uchakachuaji wa kura katika zoezi hili kama mnavyolia pindi mnaposhindwa? tehe tehe tehe!!!
ReplyDelete