JK leo ameungana na waislamu wengine kote nchini kusali sala ya Eid El Hajj. Pichani anaonekana JK na mmoja wa waumini vijana baada ya sala ya Eid katika msikiti wa Gaddaffi uliopo mjini Dodoma leo asubuhi.
JK akiwapa mkono wa Eid waumini wenzake baada ya sala ya eid katika msikiti wa Gaddaffi uliopo mjini Dodoma leo asubuhi.
Baadhi ya waumini wa dini ya kiisalamu wakisali sala ya Edi katika msikiti wa Gaddaffi mjini Dodoma leo asubuhi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. MBONA HUYO DOGO WANAFANANA SANA? SIO MWANAE? AU?

    CHIBI.

    ReplyDelete
  2. Michuzi mbona hutuwekei kuwa Mhe. Raisi Amewateua Zakia Meghji na Shamsi Vuai Nahodha kuwa wabunge? Hiyo ni preview ya baraza la mawaziri. Meghji anarudi fedha na Nahodha mambo ya Ndani

    ReplyDelete
  3. Michuzi tafadhali mtusaidie hii sikukuu ya IDD ALHAJI inaposwaliwa kwa siku tofauti inatukanganya sie waumini wenye uelewa mdogo maana huku vijijini wengine tuko katika taasisi zingine kama mie muislam pekeyangu na tasisi yetu Bakwata inapeleka waislam huko Maka kwa shughuli hiyo ina maana haina mawsiliano ya uhakika kwa viongozi waliopeleka waumini huko nakufahamu hiyo arafa inafanyika lini maana nadhani saa zetu na Saudi Arabia hazitofautiani sana kiasi tupishane siku nzima na ulimwengu wa sasa utandawazi upo juu sana inatusikitisha sana hasa inapotokea sehemu ndogo kama Mbinga muislamu unashindwa kuelezea wenzio katika taasisi kwamba leo au kesho ni sikukuu maana dhehebu moja asubuhi ya tarehe 16 walipita na Kipaza sauti kutangaza ni sikukuu ya IDD na wenzio wanakuuliza juu ya jambo hilo kwa kutumia simu unabaki na maelezo yasio na majibu ya kitaalamu kwamba hao ni AnsalSuna naomba nyie mliopo kwenye vyombo vya habari mtusaidie- Mwambungu Mbinga,Ruvuma.

    ReplyDelete
  4. Annon wa Mbinga - sasa Michuzi hapo akusaidieje?? Yaani matatizo yako wewe na waajiri wako usaidiwe na Michuzi jamani??!!!?? Siamini kama mu wavivu wa kufikiri kiasi hiki!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...