Boeing la Air Tanzania likiwa juu ya mawe katika uwanja wa ndege wa airport ya Mwanza kama ionekanavyo pichani hapo.Ndege hii ilipata mushkeli miezi kadhaa iliyopita pindi ilipokuwa ikitua uwanjani hapo. Hadi leo mustakabali wake haujulikani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Lol!Itakuwa imeokoa maisha ya watu wengi kwa kukaa juu ya matofali doh!!

    ReplyDelete
  2. Ukilaumu serikali unaonekana mpinzani ukilaumu chama tawala unaambulia matusi. Eti tucheke tu hakuna wakuwajibishwa

    ReplyDelete
  3. habari nilizonazo kuhusu hiyo ndege haikuwa ya air tanzania, air ATC waliikodisha kutoka kwa mtu fulani, hivyo jamaa amekwisha lipwa insurance yake na anafanya mipango ya kuja kuichukua hiyo ndege hapo mwanza

    hivyo ATC haina deal tena na hiyo ndege kidumu chama cha Any Time Cancellation (ATC)

    ReplyDelete
  4. Kama kawaida. Kazi Bure!

    ReplyDelete
  5. AIBU KUBWA. NA HII NDIO 'NATIONAL FLAG CARRIER. NI NEMBO YA TAIFA (SYMBOL).INA MAANA TAIFA LIKO JUU YA MAWE!! SERIKALI NA WATU MAKINI HUWA HAWACHEZI NA VITU KAMA HIVI.LEO HII TULIPASWA KUWA KAMA KENYA AIRWAYS, ETHIOPIAN AIRLINES NA MASHIRIKA MENGINE YA NDEGE YANAYOMILIKIWA KWA SEHEMU KUBWA NA SERIKALI. KILA NCHI INA CHOMBO HIKI MUHIMU. TANZANIA NINI INATUSHINDA KUENDESHA ATC KWA MAFANIKIO JAMANI!?

    ReplyDelete
  6. MBONA RASILIMALI ZA TANZANIA ZINACHEWA HIVI JAMANI? HII NDEGE ILINUNULIWA KWA KODI WA WATANZANIA, WANAHUSIKA HAWAONI HILI???

    ASANTE MICHUZI KWA KUTUWEKEA PICHA HII, WATANZANIA WENYE AKILI WATAJUA NINI KINACHOENDELEA BONGO

    mdau
    a-town

    ReplyDelete
  7. matanga ni lini maana shirika limezikwa

    ReplyDelete
  8. Hii si ya kufurahia hata kidogo.Ni matokeo ya ubinafsishaji usio na tija kwa taifa.

    ReplyDelete
  9. Hii italuja kuua, tena kiongozi.

    ReplyDelete
  10. MHHH! JAMANI ZITAKUJA KUUWA WATU HIZI NAOMBA SAANA WAWEMAKINI. MAANA TANZANIA BADO SAAAANA.

    ReplyDelete
  11. THIS IS BREAKING NEWS!!!!


    Ghailani - The Tanzanian indicted of terror charges of bombing in Tanzania and Kenya..

    The first former Guantanamo Bay detainee to be tried in federal criminal court was found guilty on a single conspiracy charge Wednesday but cleared on 284 other counts.

    Read the story from

    http://www.nytimes.com/2010/11/18/nyregion/18confess.html?partner=rss&emc=rss

    ReplyDelete
  12. Mikausho MikaliNovember 18, 2010

    ATCL itarudi angani kwa kishindo si muda mrefu toka sasa.Serikali inajipanga vizuri

    ReplyDelete
  13. Michu,

    Haya sio matumizi ya neno "pindi". Hii ni lugha gongana.

    ReplyDelete
  14. BREEEKING NYUUUUZZZ

    Nyie watu, pamoja na Micuizi pia) acheni uchochezi. Mnataka kutibua hali ya hewa na kutuondolea amani tuliyoizoza miaka na miaka. Uchochezi utawasaidia nini? Fanyenii kaaz ndugu, acheni kulalama ovyo na kuyakuza mabaya machache mnayoyaona! Siri kuu ya mafanikio ni kufanya kaaz! Kwani hii ni ajali ya kwanza kutokea? Kwani ATC ndio shirika lakwanza kupata ajali? Mbona hili hutokea kwa mashirika mengine, tena makubwa ya nchi zilizoendelea seuse Tanzania? Nani hajasikia juu ya ile femaas Swiss Air na jinsi ilivyoyumba? Ni nani leo hii hajui mgogoro uliokomaa wa Alitalia? Au huko pia kuna mkono wa sisyeeemu? Acheni kelele za bure ndugu, fanyeni kaaz. Wewe michuuz usipoiweka hii ujumbe utakuwa umekukuna, na hili ndilo lengo langu!

    ReplyDelete
  15. Asalaam alaykhum Ankal,

    Nakumbuka toka siku ya kwanza umetuhabarisha habari hii ya ajali ya ndege toka mwanza na ilikua ni muda mfupi tu toka ajalia itokee tayari ulikua umeshatupatia taswira na kisa cha ajali asante sana kwa umakini wako juu ya habari muhimi.

    Binafsi si walaamu kabisa Rubani wa ndege, Engineer wa ndege alieiruhusu Iruke kwa siku hiyo maana ndege imeruka ikiwa salama kabisa toka Dar. Matatizo yaliaanza wakati ndege ilipokua ikitua maji yaliingia katika engine na engine ya upande mmoja kuzima baada ya hapo engine moja tu ndio ilikua inafanya kazi kitu kilichosababisha ndege kuvutwa upande mmoja na kutoka katika lami na kuelekea katika majani.

    Kwakua mvua ilikua imenyesha uwanja mzima ulikua umetota kabisa ndege ilipoacha lami iliingia katika majai na tairi ya mbele kutiti katika matope kutokana na speed ya wakati wa kutua tairi ilichomoka na ndege ikakaa chini alhamduklilah hakuna abiria aliyeumia.

    Kwa kisa hiki ukiangalia kabisa mamlaka ya kiwanja ndio wanpaswa kulaumiwa kwasababu hawakua makini kabisa wakati wanmruhusu rubani atue na uwanja umejaa maji kiasi ya kuhatarisha maisha ya watu na hakuna aliyeliona hili yaani inauma sana na huwezi amini bila aibu mamlaka ya uwanja wanaidai serikali pesa ya ndge hiyo kukaa hapo kwa muda wote huo wakati wao ndio chanzo cha ajali na sio ubovu wa ndege kabisa inauma sana uzembe bila ya kuwajibishwa basi tu haki ni kwamungu duniani hapa tunasukuma siku tu.

    Wasalaam

    Mdau Madagasca!!

    ReplyDelete
  16. then kuna ahadi za kujenga international airport kila mkoa. ni za kutua nyungo au.........

    ReplyDelete
  17. Wewe unashambulia matumizi ya neno "pindi' angalia wewe mwenyewe ulivyotumia vibaya neno "gongana." Siku hizi kuna watu wanatumia Kiswahili kama Kiingereza kwa kusema "lugha gongana" badala ya "lugha inayogongana." Huu ni mfano mmoja tu. Kiswahili kina muundo wake, tusichukue Kiswahili kwa Kiingereza na kudhani tuko sahihi.

    Iko siku watu watasema: "Nchi endelea" badala ya "nchi zilizoendelea." Hakuna hata lugha moja duniani inayotumia muundo wa lugha nyingine. Zinaweza kufanana lakini siyo kuharibu lugha nyingine kwa kudhani kuwa ni maendeleo. Kiswahili kina tatizo sana hasa kutokana na watu kudhani kwamba kadri kinavyofanana na Kiingereza, ndivyo kinavyokuwa sahihi.

    Siku hizi tena tuna watu wanaoiga Wakenya, hasa wafanyakazi wa hoteli za Tanzania na waigiza sinema na hata wanamuziki. Huu ni ulimbukeni. Acheni kuiga vya wengine vyenye makosa. Mtu asiyeheshimu cha kwake au asiyejua cha kwake ni mtumwa wa mawazo.

    Mfano mwingine ni watu kutumia neno "nyimbo" kumaanisha "wimbo mmoja" wakati kwa Kiswahili sanifu nyimbo ni wingi wa wimbo. Utasikia mtu anasema "nyimbo hii" kwa kuwa kuna Mkenya amesema hivyo. Sasa zikiwa nyingi utaziita "zimbo"?

    Mdau Washington DC.

    ReplyDelete
  18. ndege iko juu ya mawe lakini aahh wafanyakazi wa ATC wanapokea mishahara minono pamoja safari za n'gambo sasa sijui wanapata wapi mapato ya kuwalipa iwapo ndege zenyewe haziruki hili nalo neno!!!

    ReplyDelete
  19. Asalam Alaykum Kaka Michuzi.

    Najua hukupost post yangu iliyopita kuhusu ukurekebisha kuhusianna na majina ya vitu. Mara ya mwisho nilikurekebisha kuhusu uandikaji wa "Chuo Kikuu cha University Of Dar Es Salaam" na kukwambia kuwa sio sahihi. Inapaswa kuwa "Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam" na sio kama ulivyosema awali maana hilo neno "University" sio jina bali ni kielezo cha kukwambia kuwa hii ni taasisi ya aina gani. Na pia nilitoa mfano wa kusema "Barabara ya Morogoro Road" ambalo ni tatizo sawa na hilo la "University" kwani unarudia maelezo ambayo yanakuwa hayaleti maana kama yatatafsiriwa kwa aidha kiingereza au kiswahili. Leo umekuja na hii ya "Uwanja wa Ndege wa Mwanza Airport" ambayo ni tatizo sawa na hayo mawili yaliyopita.

    Naomba ukubali pale unapopewa "Challenge" na sio kuzuia post za watu maana unakuwa husaidii umma badala yake unapotosha wanaojaribu kujifunza lugha yetu nzuri ya Kiswahili.

    Asante.

    ReplyDelete
  20. ......watu wengine jipeni uhuru wa kuelewa tamaduni za watu wengine! kuna lugha za mtaani au kwa watani wajadi wanaita "SHANG" humu kwa Ankal kuna lugha inatumika kama mwenyeji haikusumbui ......."my wife wake" usikariri mzee, just enjoy!!

    ReplyDelete
  21. it is suprising that the managemnt of atcl is still there. huu ni uhuni because they know they getting paid for doing nothing na serikali inafumbia macho. je tutafika. the story keeps repeating itself when are going to learn to be proud of what is ours? great shame to those who have simpathy na atcl management

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...