KOMBOLELA SHOW JUMAMOSI HII
Novemba 20, 2010
@ 01:00pm - 02:00pm EST,
3:00pm -10:00pm East African Time

Dunia yetu inazidi kuwa ndogo kutokana na maendeleo ya kisayansi, hasa katika teknolojia ya habari. Zaidi ya hayo, Tanzania imefungua mipaka yake kwa makampuni ya nje kuja kuwekeza nchini, kitu ambacho kinapelekea kuwepo kwa ushindani mkubwa wa kibiashara na ukuwaji wa ubora wa bidhaa na huduma zinatolewa kwa mteja wa kitanzania. Lakini mbali na maendeleo hayo, bado kuna malalamiko ya vijana wengi wa kitanzania kukosa ajira. Ni dhahiri kwamba mojawapo ya vijana kujikwamua ni kujitosa kwenye ujasiriamali.

Radio Mbao kupitia Kombolela Show itakuwa na mahojiano na Mbwana Alliy ambaye atachangia uzoefu wake katika mambo ya ujasiriamali, hasa katika eneo la teknolojia ya habari (information technology).

Mbwana Alliy mtanzania ambaye kwa sasa hivi makazi yake ni Marekani, ambako anajihusisha na mambo ya teknolojia ya habari katika jimbo la California (eneo maarufu la Silicon Valley). Zaidi, Mbwana ni vmmiliki wa www.yellowmasai.com, tovuti inayojihusisha na masuala ya uwakala wa usafiri na utalii.

Jiunge nasi kwa kupitia hapa:
ili usikose uhondo!
--
Metty

Your Host

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kombolela sio,ngoja tumtafute atakayesafa. kuku na bata walifanya harusi chumbani/ikisanso.Huu mchezo ulitufundisha mambo mengi pia kuharibu mabinti za watu.Watu tulikuwa tunajificha midizini(migombani) vichochoroni afu moto kibati kama unavyojua.Uswahilini poa sana kuliko getini.Watoto wa getini hawaujui mchezo na faida zake.LOL.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...