Hadi sasa matokeo ya viti vya Ubunge yameshatangazwa katika majimbo 104 bado 135 kati ya yote 239. Kati ya hayo, CCM imeshapata majimbo 66, CHADEMA 19, CUF 15, NCCR Mageuzi 2 na TLP 2.

Mojawapo ya sababu za kuchelewa kutangazwa matokeo ya baadhi ya majimbo ni kutokana na utaratibu wa NEC unaotaka matokeo kuingizwa katika kwenye compyuta ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kabla ya kutangazwa.
Kwa matokeo kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. HAPA SIFAHAMU INA MAANA MAJIMBO YA ZANZIBAR BADO HAYAJAMALIZIKA YOTE?MBONA TUNAONA CUF MAJIMBO 15 WAKATI MAJIMBO 22 AU NDIO ZANZIBAR HAIMO KATIKA HAYO MAJIMBO?

    ReplyDelete
  2. Asante Ankal kwa link ya NEC, matokeo yamepangwa vizuri sana na yanakupa hali halisi ya wapigakura jinsi walivyochagua, na hisia zangu zimekuwa kama nilivyotegemea Dr.Slaa ameshinda majimbo ambayo kweli ana nguvu na Prof.Lipumba vilevile.

    Kwahiyo sioni hilo zengwe Dr.Slaa analotaka kuanzisha la kukataa matokeo na eti uchaguzi urudiwe!!! NEC mpaka sasa wanafanya kazi nzuri sana ya kisasa, hata Marekani ambapo umefanyika uchaguzi wa maseneta na wawakirishi jana bado matokeo mengine hawajui na yatachukua siku kadhaa, na wao ndio nchi iliyoendelea sana kwenye teknolojia ya mawasiliano!

    Dr.Slaa wawache NEC wamalize kazi yao, nakupongeza kwa kazi nzuri uliyoifanya kusaidia wenzio kuingia bungeni lakini kwa matokeo niliyopitia kwenye mtandao wa NEC wewe huna uwezo wa kuwa RAIS na wewe mwenyewe unajua na wafuasi wako wanajua hilo.

    Dr.Slaa jiepushe na aina yoyote ya uchochezi kwani itakuharibia hadhi yako na kuigawa nchi katika makundi na wewe kukumbukwa kwa mabaya. Kuwa mvumilivu, ni hatua nzuri mliyoipiga, chaguzi zinazokuja CCM ndiyo inawezakuwa chama cha upinzani na siyo CHADEMA au CAFU lakini kwa uchaguzi huu wewe kuwa RAISI au CHADEMA na CAFU kuwa na vitu vingi bungeni haiwezekani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...