Viongozi wa tawi la CCM Napoli pamoja na wajumbe na baaadhi ya wadau wakiwa katika picha ya pamoja.

Usiku wa kuamkia leo jijini Napoli palikuwa hapatoshi katika mnuso ulioandaliawa na tawi la Chama Cha Mapinduzi Napoli-Italy, sherehe hiyo iliyoalika Watanzania wote na wageni wataliani ilianza majira ya saa kumi jioni mpaka kuche.

Katibu wa tawi ndugu Kagutta N.Maulidi katika salaam fupi kabla hajamkaribisha mwenyekiti wa tawi la CCM Napoli alisema ushindi wa Chama Cha Mapinduzi ni wa Watanzania wote kwani ni Watanzania walioamua kuchagua tena CCM kuliongoza taifa letu.Aidha katibu aliwataka watanzania kuendeleza umoja wao na ushirikiano.

Mweyekiti wa tawi ndugu Abdulrahaman A.Alli wakati wa kufungua sherehe hiyo aliwashukuru na kuwapongeza Watanzania wote,wana usalama, wasimamizi wa uchaguzi wote na serikali kwa jumla kwa kuendesha uchaguzi wa amani, wengi wa wageni wataliani waliokuja katika sherehe walikuwa wametokea Tanzania kwa utalii, wamesifia sana usalama na amani ya Tanzania.

Aidha mwenyekiti alimpongeza Mh Raisi Dr JAKAYA MRISHO KIKWETE kwa kuchaguliwa tena kuliongoza taifa letu.

Katika sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa jumuiya ya Watanzania Italy tawi la Modena,Padova,Genova ,Mwakilishi wa Jumuiya ya Wanzania Italia TANZANIA ndugu EMANUEL KAPONGO na Wanajumuiya wanaoishi Roma. Usiku wa jana watanzania wengi waliomba fomu za kujiunga na Chama cha Mapinduzi.

picha za tukio tembelea
WABONGO UGHAIBUNI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. bora nyinyi mnaojua kufurahia maswala ya nchi yenu big up kwa sana NAPOLION sio nyinyi wakimbizi na wabeba mabox kazi yenu umbea na kukandia kila jambo.CCM JUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUAA

    ReplyDelete
  2. NAPOLI MKO JUU, WAKILISHENI NCHI YENU,BIG UP JK WATANZANIA WAKO PAMOJA NA WEWE NDIO MAANA TUMEKUCHAGUA TENA UNAKUBALIKA!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...