Mrisho Mpoto
Msanii mahiri wa mashairi nchini,Mrisho Mpoto ameeleza kile anachoamini kwamba,tasnia ya sanaa na wasanii wa Bongo hawawezi kamwe kupata mafanikio katika ngazi ya kimataifa kutokana na ulimbukeni wa kuiga sanaa za watu wengine, kudharau asili yao na kujipachika usupastaa wa kubumba.

Mpoto aliyasema hayo wakati akiwasilisha mada yake iliyohusu Muziki wa Asili na Mashairi kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii ambapo alisisitiza kwamba,wasanii wa bongo wamekuwa ni wa kulalama na kulia njaa kutokana na kazi wanazozalisha kushindwa kabisa kupata mvuto wa kimataifa na kushindana kwani zimekuwa kwa asilimia kubwa zikifanana na tamaduni za nje hivyo kukosa jipya.

Akijitolea mfano yeye mwenyewe Mpoto alisema kwamba, ameweza kukaa chini na kubuni sanaa ya asili ya Tanzania ambapo amekuwa akighani mashairi na kuyaweka kwenye mdundo wa muziki na hivyo kupendwa na idadi kubwa ya watanzania na kupenya kimataifa hivyo kumfanya kupata mialiko na fursa nyingi za fedha ambazo zimekuwa zikimpatia mafanikio makubwa.

Kwake yeye Mpoto anaamini kwamba, Sanaa ya Tanzania na wasanii wake hawaonekani kugundua siri ya kufanya kazi za sanaa zenye asili yao na badala yake wamekuwa makasuku wa kujifananisha na kuishi maisha kama ya Ulaya na Marekani huku kazi zao zikifanana kila kitu na hizo za nje hali ambayo imeifanya sanaa kupwaya na wasanii wenyewe kuishi maisha ya njaa.

Aliongeza kwamba, ni ngumu kupata msanii wa bongo anayefanya sanaa peke yake kwani mara nyingi lazima wachanganye na shughuli zingine ili kupata kipato kutokana na kazi zao kutowalipa.Katika hili Mpoto anaamini kwa kiasi kikubwa limesababishwa na wasanii wenyewe kukosa ubunifu, kuiga kila kitu kutoka nje, kulewa sifa za mapema, kukumbatia sanaa zisizo za asili yao na kujipachika usupastaa wa kubumba.

“Nimekuwa nikipata mialiko mingi nje ya nchi,siku chache zijazo nitaenda Denmark,Finland,Ufaransa, na Uholanzi.Si kwa kuwa napendwa sana bali ni aina ya sanaa ninayofanya ina asili yangu ya Tanzania na inanitambulisha kila ninakokwenda.Waache wasanii wengine wavae nguo chini ya makalio yao au hata watembee uchi mimi nitabaki na magunia yangu.Hili ndilo naamini litaweza kunipa mafanikio na ninayapata” alisisitiza Mpoto.

Mpoto ambaye kwa sasa ni msanii pekee aliyepata mafanikio makubwa kutokana na kupata mikataba mingi ya matangazo, mauzo ya kazi zake na mialiko ya kimataifa kutokana na kukumbatia sanaa ya asili aliwashauri wasanii wa bongo kuacha kunakiri (kukopi) sanaa za nje na badala yake wakune vichwa katika kubeba sanaa ya asili ambayo hapana shaka itawatambulisha kimataifa na kuwapa mikataba minono ya ndani na ya nje.

Mpoto aliyekuwa ameambatana na muimbaji wake wa Mjomba Band,Ismail alisema kwamba, inatia aibu na kinyaa unapoangalia sanaa za bongo kwani zinaonekana kuandaliwa na watu wenye njaa, wanaosaka fedha za fastafasta kuliko kujali nini wanapeleka sokoni hali ambayo imekuwa ikiwafanya wasanii wa Tanzania waonekane ni wa hovyohovyo, wa kudharaulika na wasio na mkakati wa kufikia mafanikio ya kisanaa.

“Kuna watu wamefanya sanaa miaka nenda miaka rudi lakini hawapigi hatua.Wamekuwa ni watu wa kulalamika bila kuzingatia ni kwa kiwango gani sanaa zao zina ubunifu na kubeba asili na utambulisho wao.Ndugu zangu tusipozingatia haya mafaniko tutayasikia tu na tutakuwa watu wa kuganga njaa na kupiga mizinga ya vocha” alimalizia Mpoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Hajawabeza bali amewapa ukweli ulio wazi. Nasisi washabiki ni sehemu kubwa ya waharibifu sanaaa ya hapa nyumbani kwa kupenda na kutukuza na kushangilia upuuuzi usio na thamani

    ReplyDelete
  2. huyu jamaa matangazo anayofeature yametulia yote! sikiliza pia matangazo ya fataki!! Big up

    ReplyDelete
  3. huyu baba kweli ameongea, muzik wa bongo ni wa africa magharib, mombasa. congo,europe na america. tanzaina hakuna mzik wala asili ndombolo kwa wingi. ayway watakonipinga wanipinge tu lakni bong hakuna mdundiko wala sekinde, zimepotea zote

    ReplyDelete
  4. Ankal acha uhuni. Weka matokeo ya Ubungo hapa tuserebuke

    ReplyDelete
  5. Very true nakubaliana na huyu msanii 100%.

    Tunahitaji ubunifu wa Kitanzania sio kuchota kila kitu cha nje kuanzia Zaire, Afrika Kusini, Amerika, Ulaya, India , Uarabuni - duu...

    Tumekuwa kama dodoki?? We need originality and that is what makes you unique and have your own product and that is a ticket to lasting success hata usupper sta kama ndio unautaka

    ReplyDelete
  6. Mpoto heko kwa kusema ukweli.

    Wape wape vidonge vyao, wakinuna wakicheka shauri yao!

    AMKENI NYINYI WASANII KUJIDAI KUIGA UZUNGU AMBAO HAMUUWEZI HAUTAWAPELEKA PO POTE.

    ReplyDelete
  7. Mpoto heko kwa kusema ukweli.

    Wape wape vidonge vyao, wakinuna wakicheka shauri yao!

    AMKENI NYINYI WASANII KUJIDAI KUIGA UZUNGU AMBAO HAMUUWEZI HAUTAWAPELEKA PO POTE.

    ReplyDelete
  8. Mjomba kwa kila neno uliloongea na nukta ulipoiweka ni la msingi na kuzingatiwa sana,

    Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio kumwambia sikia ni ngumu kama mwenyewe kaamua kusikia,

    Changamoto kwenu wanamuziki wa kizazi kipya mkiamua kuwa waziwi na wapofu kama mlivyoamua sawa lakini mjomba AMEMALIZA

    ReplyDelete
  9. wape wape vidonge vyao! wakimeza wakitema shauri yao! Msema kweli kipenzi cha mola.

    ReplyDelete
  10. Huyu Mpoto, mbona amewajia juu sana wenzie? Unaosema ni ukweli mtupu hususan kuhusu kazi za wasanii wa bongo kukosa mvuto. Sio Muziki tu, hata filamu ni Nigeria a-z!

    ReplyDelete
  11. Nakufagilia sana ndugu Mpoto. Mimi nimeishi nje ya nchi kwa takriban miaka 15 sasa na muziki wa kufoka huku nchini Marekani unahusishwa na uhalifu, madawa ya kulevya nk. kwahiyo ukitoka Bongo unakuja huku na muziki huo ni sawa na kuchota maji kisimani kupeleka baharini, pili kuna daraja fulani la waungwana hawatopenda muziki wako na hao ndo wengi na wenye uwezo kwa kipato. Washabiki wa kufokafoka wengi wapo Ghetto wanasubiri mgao wa posho ya serikali au roba za mbao ili waishi. Vita mbele ndugu mpoto!!!!

    ReplyDelete
  12. Mjomba umezungumza kweli kabisa. Tatizo letu kubwa ni kwamba tunadhania njia pekee au nzuri ya kukubalika ni kujikataa.

    Ingawa ukweli ni kwamba ukishajikataa wewe mwenyewe basi kila mtu atakukataa.

    Wasanii wa kizazi kipya wanakuja stockholm kufanya show yao ya muziki wa kizazi kipya. Wakati Wasweden wenyewe wakitaka show ya muziki wa rap basi watawaalika wamarekani, na kamwe hawatakualika wewe m-bongo. Na ndo maana mkija huku ughaibuni washabiki wenu ni wabongo wenzenu tuu.

    ReplyDelete
  13. "Waache wasanii wengine wavae nguo chini ya makalio yao au hata watembee uchi mimi nitabaki na magunia yangu.Hili ndilo naamini litaweza kunipa mafanikio na ninayapata”

    Hakuna cha kuongezea...

    ReplyDelete
  14. Safi Mpoto. Huwa nakereka kusikia Mtanzania anazungumza Kiswahili cha Kikenya eti kwa sababu anaigiza sinema au anafanya kazi hotelini. Ni kinyaa. Hata huku nje ya nchi tuna tatizo la Watanzania kukikataa Kiswahili wakidhani wanakuwa wajanja. Huwezi kuwa Mmarekani au Mwingireza kwa kukataa Kiswahili wakati wao wanakitamani. Wakenya mpaka wanaidanganya dunia kwamba Kiswahili ni chao wakati ukweli si hivyo; hii ni kutokana na Watanzania kukidharau. Wape wape Mjomba Mpoto.

    ReplyDelete
  15. Huyo msanii hana lolote. Anapata hizo show kwasababu wazungu wanapenda kuona blacks (africans) wakibehave kama nyani.
    Kama wewe unakaa mbagala au manzese muziki wako lazima uwe na hasira na mambo ya wizi, madawa ya kulevya nk.. Uwezi ukamwambia bongo flava ambaye amekulia kariakoo aimbe kuhusu mbuga za wanyama tanzania..
    KWAHIYO LIFE IMITATES ART SOMETIMES..
    Kila mtu ana ujumbe wake.. Lazima wanamuziki waongee kuhusu mbagala, manzese au ilala.. nani atawakilisha..
    Kuhusu marekani.. mimi mwenyewe nipo huku toka 96 na bongo nakuja sana kila mara.. Muziki wa bongo sio kama hiphop ya marekani.
    Kwanza thought process tafauti na topics hazifanani.. sijasikia Bongo flava artist kaisema Bentley or diamonds rights or buying crystals bottles.. or poppin pills.. Kama nimekupoteza.. exactly that..
    Kila artist ni mzuri na hakuna shida. Mbona Terminator au rambo films zinapendwa..
    Kama mtu anaenda kuwa monkey au an example of Tanzania na anavaa magunia ..That's not Tanzania music.
    Kama wewe unapata hela kuvaa suit au gunia vaa.. usitukane watu au usijifanye umeona light at the end of the road.
    ZAMANI WALIKUWA WANAWAVALISHA SLAVES MAGUNIA NA KUWALAZIMISHA KUIMBA.. HUKU WAO WANAKUNYWA WHISKY.. NAFIKIRI IT'S THE SAME THING.. KWAHIYO TULIA..
    DON'T KNOCK THE OTHER MAN HUSTLE!!
    Julius Temu..MDAU LA CALIFORNIA

    ReplyDelete
  16. Huyu naye fala tu, watu wote tunafocus on election saa hizi, wewe kazi kuponda wenzio na kujitapa tu, mwanga nini? Toka hapa na magunia yako...

    ReplyDelete
  17. Mdau wa California hapo umeongea. Utamaduni wa Tanzania siyo kuvaa magunia, huo ni upuuzi kushabikia umasikini. Huyu Mpoto ana points muhimu ameongelea lakini nadhani yeye anaweza asiwe mtu anayefaa kuongelea originality au hata creativity, hamna anachofanya ambacho wengine huko nyuma hawajafanya....no idea is original.

    Hip Hop yenyewe ya marekani imechukua ideas nyingi, ikiwemo sauti kutoka Africa. Hao ni ndugu zetu anyway, siyo kwamba watu wanaenda kucopy country music.

    Nikimalizia, ingawa nina mengi ya kusema kuhusu hili, ni kwamba kuna wengi dunia hii wanaopata hela nyingi kila siku, ikiwemo mamilioni, kwa kujidhalilisha. Huyu mtu anaweza akawa mwandishi mzuri wa mashairi, lakini sidhani kama wazungu anaoenda kuwatumbuiza wanamuita kwa sababu ya mashairi yake.....by the way, historia inasema wazungu wanaogopa sana weusi duniani kujiunga pamoja kisiasa, kiutamaduni, kiuchumi, huyu mzee anaweza akawa anawakilisha nia yao bila kujua.

    ReplyDelete
  18. mlisho mpoto umaarufu hauji kiivyo hapo mwanangu Buuuuuuuu!!!!!!!!!
    Naungana na mdau wa carfonia acha mambo ya kufuaatilia watu, hata kuyatoa ujayatoa umeshaanza sifa, tulia kijana au tafuta washauri wakushauri kabla ya kuongea yaani unakera!!!!!

    Mwe!!!!!!

    mda wa mbeta!!!!!

    ReplyDelete
  19. Hivi nyie wabeba box wengine mbona wagumu kuelewa hasa we Julius Temu wa California (kama kweli)... Mpoto alikuwa anazungumza na Wasanii wenziwe mbele ya Jukwaa la wasanii kama kumpinga wangempinga hapo na wangeanzisha naye bifu wamuimbe vibaya kama wanaweza...
    Lakini jiulize ni jambo gani la uongo ambalo amelisema..? Ni kweli kuwa Wasanii wa BongoFleva ndio wanaolalamika sana kuwa wanaibiwa kazi zao na wahindi, kazi zao haziuzi sokoni, wanazouza kipato hakilingani na jasho walotoa..
    pili ni kuwa hakuna mziki kama mziki unaoitwa bongofleva kwa sababu wote wanaimba aidha RnB, Hiphop,Reggae, Ragga, Chacha, Soul, Nigerian, etc.. hii inaitwa ladha za bongo sababu mziki tunaoiga tunaongezea vionjo vyetu ambavyo ni lugha ya kiswahili, lafudhi za kiasili,etc but wasanii wengi kama si wote utasikia wameingia kwenye mziki aidha kwa kuvutiwa na Bob, Michael Jackson, Usher, Tupac, Snoop etc hii ni kuthibitisha kuwa wanaiga tena hadi mavazi yao...
    unaposema sio asili yetu kuvaa magunia, hivi niambie kabla ya wakoloni babu na bibi zako walikuwa na kiwanda gani cha nguo hapa afrika walipokuwa wananunua nguo zao kama sio kuvaa, majani, ngozi nk. Sasa Mpoto amekosea nini.
    Je ni uongo kwamba Mpoto anaonekana ktk kila tamasha kubwa la kitaifa na ya Kiserikali na ya kijamii, pia katika matamasha mbalimbali ya burudani? Je ni uongo kuwa kila mtu wa rika zote walibambwa na nyimbo za Mpoto hata wale ambao zinawalenga lakini bado wanavutiwa nazo? Je hukumbuki jinsi Mpoto alivyozoa Tuzo za Kili kwa nyimbo inayopendwa zaidi, na nyimbo bora ya mwaka, pamoja na tuzo nyingine nyingi tu..? je hujui kuwa Mpoto kila mara mguu ndani mguu nje kwa mialiko ya nje ya nchi anayoipata..? Je hujui kuwa Mpoto ndio Msanii anayeongoza kwa sasa kupata matangazo mengi ya kibiashara kyk vyombo vya habari nchinio TZ... (rudi nyumbani ujue yote haya)
    Nawashauri kuwa ukipewa ushauri ufanyie kazi sio kupinga tu... Mpoto yuko Down to earth sio mtu anayejikweza na usupastaa mbuzi...

    ReplyDelete
  20. Ras Job wa (ir)

    kaka pole kwa mawazo yaliyokusonga, najua unauwezo kisanii, ila kidogo umepotea wanakudanganya hawa wanaokusifu, kaka sijazoea kuficha ukweli.nawapenda wote Tz sipendi kuona mtu anamzarau mwingine maana kila mtu ana uwezo wake aliopewa na mungu ktk kufikilia. haujanifurahisha ila umeniboa kaka.

    usione wasanii wanaimba wanapata shida wewe kaka ukiwa kama Ras TOA MSAADA WA KUWAELIMISHA SIO KUWABEZA HIVYO KAKA, RASTA HAIKO HIVYO, kama ujumbe wanautoa mziki kuiga amerika ndio ishu, wakikuiga utauza kaka, mi nimpenzi wa nyimbo zote REGGAE NDIO HOME sijaanza kuimba ila nawapenda wote hapa tz, RAS JOB TZ IRINGA.NAWAPA BIG UP WASANII WA BONGO WA AINA ZOTE, POLENI KWA MAELEZO YA KAKA ALIPOTEA KIDOGO TUMSAMEE NAE NI MTU TUUU TUNAOMBA MTUNGE NYIMBO ZA KUMSIFU ATAKAE TANGAZWA KUIONGOZA NCHI YETU TUMPE SAPOT RAIS SHEN, SEF, KIKWETE, SILAA,BILALI NA WABUNGE WOTE BIG UP MNAO UWEZO WOTE MTUONGOZE FRESH. TZ WOTE MKO FRESH Ras JOB wa IR,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...