Ankal Mithupu,
Kwanza nikupongeze kwa kuendesha blog ambayo kwa kweli ni ya jamii. Maana cocktail ya habari zilizomo humu si mchezo. Yaani we acha tu. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Ankal uko juu. Wewe ni oroginal, wengine wote fotokopi. Haki ya nani vile. Yaani ulivyorudi juu kabisa kwenye chati baada ya kutuuzi na CCM yako wakati wa uchaguzi unastahili sifa. Raha imerudi kama zamani sasa. Mie nilishakata tamaa ati...
Mie Ankal ni mke wa mtu, nimeolewa mwaka unusu sasa. Na miezi mitatu iliyopita mie na mai hazbendi wangu tumejaaliwa mtoto mvulana ambaye anaendelea vyema. Tunashukuru Mungu kwa hilo kwa kweli.
Waama, baada ya salamu naomba msaada kwenye hili tuta kubwa lililo mbele yangu. Ni kwamba Mai hazbendi uazlendo inaonekana umemshinda linapokuja swala la 'Chakula cha Usiku'. Mie namwambie mtoto bado mdogo tusimbemende, yeye haelewi. Anadai tu chakula cha usiku, nami inabidi nimpe maana shetani naogopa asijemwingia na kuanza kusaka msosi nje. Yaani we acha tu. Kufa sifi ila cha moto nakiona. Mbaya zaidi nampenda ile mbaya.
Sasa Ankal, msaada ninaoomba kwa wadau wa blog ya jamii ni je, niendelee kutoa chakula cha usiku kwa baba sani ama vipi. Maana mwenzenu nshachangayikiwa kwani ninavyowajua wanaume huwa hawana dogo. Ukimnyima tu, huyooo... kenda nje. Ukimpa kosa, mtoto atabemendwa. Naomba wataalamu wa mambo haya wanisaidie. Samahani lakini. Ukiona hivyo mwenzenu mjue unga umezidi maji.
Wakatabahu
Ndimi Mdau Alice, Shinyanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Pole dada yangu kwa yaliyokusibu ila inaonekana hukupata kitchen party inayostahili. Anyway kwa ufupi kama ni baba wa mtoto wa ukweli hawezi kubemenda ila kama sio WATCH OUT!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. kwa kweli bado elimu ya uzazi inahitaji hasa kwa watu wengi
    kumbemenda mtu hakupo ila unahitaji kuwaona wataalamu wa uzazi na nyota ya kijani

    ReplyDelete
  3. nenda kawaone ma dactal ulio nao karibu humu hutapata ukweli.
    halafu kwani wewe uliishia la ngapi maana mambo haya ulipaswa uyajuwe tokea shule??

    ReplyDelete
  4. Habari muhusika (mama sani) kwanza nakuomba nikushauri kwa maswali machache, je huwa unahudhuria klinik??
    umeahi kuwauliza juu ya hili swala??

    kwa uelewa wangu ni kwamba hakuna kitu kinaitwa kubemenda katika mlolongo wa afya yaani hakuna ugonjwa wala madhara katika hilo tendo kiafya kwako ama kwa mtoto haya ni maneno ya mitaani tu kama ilivyo katika kula mayai kwa mama mjamzito nalo walikuwa wanasema ni mbaya je bado unaamini?

    aksante sana na usiku mwema

    ReplyDelete
  5. Dhana ya KUBEMENDA mtoto (mtoto kutokukua vizuri/kudumaa kwa sababu ya mama kufanya tendo la ndoa wakati ananyonyesha)ni dhana potofu na imechangia sana wanandoa kupata maambukizi ya VVU, kwa kuwa baba ananyimwa kiburudisho kwa miaka miwili! KUBEMENDA ni imani potofu, inagwa ilisaidia kwa wazazi wetu kupanga uzazi kwa kuwa njia za kisasa hazikuwako.Da ALICE ni ruksa kupata chakula cha usiku wakati wote wa ujauzito na baada ya wiki sita toka kujifungua, unachotakiwa ni kujihadhari na mimba ya bila kupanga, lakini kwa bahati mbaya ukipata mimba wakati unanyonyesha, usioogope endelea kunyonyesha mpaka unakaribia kujifungua, na kwa hali kama hiyo pia (mama mjamzito anayenyonyesha)chakula cha usiku ruksa kama unajisikia kufanya hivyo na kama hakuna tatizo la kiafya linalokinzana na tendo la ndoa wakati wa ujauzito. Unaweza pia ukapost maswali yako hapa..
    http://www.ivillage.com/staying-intimate-while-nursing/6-n-136878

    ReplyDelete
  6. Huyu dada simwelewi kidogo,labda atuambie kama baba wa mtoto ni mwingine. Kama mumewe ndiyo baba wa mtoto suala la kubemenda linatoka wapi? Kisayansi ni wiki 6 toka kuzaliwa mtoto ni ruksa. We dada acha kukupwa majukumu kwa kisingizio cha kubemenda.

    ReplyDelete
  7. Dada, Wengine hata baada ya mwezi kazi inakwenda mradi ujue kuhesabu siku zako. kama hujaona siku zako basi tumia Condom lakini kama umeona siku basi hesabu unajua siku za kupata mimba ni kuanzia siku ya kumi mpaka ya kumi na saba tangu ulipopata last menst. hesabu vizuri siku unayoanza uihesabu ukifika siku ya kumi tumia condom mpaka siku ya kumi na saba then bwerere. Msaada wa bure. Ukimnyima mwenzio usijeukalalamika matumizi yakipungua au ukimwi ukiwamaliza.

    ReplyDelete
  8. Ama kweli mimi nimekaa ughaibuni siku nyingi maana hilo neno hata nilikuwa sijawahi kulisikia. Hivi ninyi wanawake imani za kibwege kama hizi mnazitoa wapi? eeh nashukuru mke wangu hana imani kama hizi maana saa hizi ningekuwa nakwea wazungu sitaki kabisa upuuzi!! ebo!! haya nenda kajiandikishe twisheni kwa Mkichwe au Ngalawa au who ever the heck ana twisheni siku hizi.. Halafu mkisaidiwa mnalalamika pambafu!!

    Mdau, Ughaibuni.

    ReplyDelete
  9. Mama hayo mambo ya kubemenda yapo kabsaa ila sio kwa mumeo....Ile chakula ya mumeo haiwezi muharibu mtoto sabab ndo asili yake ndipo alipotokea.

    Na hili ni kwamba Unapokula chakula cha usiku moja kwa moja kinakimbilia kwenye maziwa sasa kama hicho chakula ni kutoka kwa baba wa mtoto hapo si rahisi kumuharibu mtoto....

    MTOTO ATADUMAA IKIWA HIYO CHAKULA CHA MTOTO UNAKULA SI CHA BABA YAKE NI CHA WANAUME TOFAUTI TOFAUTI....HAPO NI LAZIMA MTOTO UTAMBEMENDA, NA NDO MAANA KWA HUKU NJE UKIWA NA MIMBA HATA UKIWA UNANYONYESHWA HUWA UNAULIZWA KAMA MUMEO ANAVUTA SIGARA N.K...SABAB WANAJUA KAMA ILE CHAKULA YAKE PIA INAKUWA NA MADHARA KIDOGO YA MOSHI NA KWA VILE ILE CHAKULA KAMA AKIKUPA WEWE NI MOJA KWA MOJA INAENDA KWENYE MAZIWA YAKO NA MTOTO ANAKULA MAMOSHI YA SIGARA N.K...ILE CHAKULA YENYEWE INA VIRUTUBISHO (PROTEIN)....SIO KWA KUINYWA SORRY...KWA KUPITIA KULE KULE...

    KIUFUPI BAADA YA KUJIFUNGUA DAMU IKISHAKATA UKISHAKUWA MSAFI BASI NI RUKSA KUMPA BABA CHAKULA YAKE.....ILA CHA MSINGI NI TAHADHARI USIBEBE MIMBA NDANI YA MIAKA 2 ILI HUYO MTOTO WA KWANZA APATE MALEZI MAZURI...

    ReplyDelete
  10. Kwa ushauri wangu wa haraka nenda kachome Depo provera na hii ni siri yako mwenyewe. Wanawake tuliyo wengi tunafanya hivi. Make mimi nafanya hivi sasa ni mwaka wa 5. Kila baada ya miezi mitano naenda nachoma. Saa nyingine usimsikilize Baba Athumani, kwani mzigo mwingi unakuwa wewe. Amka ama weka Kitanzi cha miaka mitano ama kumi. Mimi najichomeaga bila mme wangu kujua. Na chakula anapata muda anaotaka niko tayari akiliza mbona upati mimba namwambia sijui. Siku nikiwa tayari nitaacha kuchoma sindano. Mama ama Dada wanaume wengine hawataki kusikia habari za uzazi wa mpango. Anataka akuzalishe ikifika jioni anaenda kupiga kinywaji ama nyumba ndogo wewe ndo unaangaka na watoto. Amka nenda kachome sindano kwa yeye anakwambia kila kitu anachokifanya. Sisimuka Dada achana eti unampenda sana ama litakuchwea mwenyewe. Huu ndo ushauri wangu.

    Mdau Dar Es Salaam

    ReplyDelete
  11. Da Alice Shinyanga,
    Km walivyosema "wataalamu" wengine hapa, hakuna madhara kufanya ngono na mumeo baada ya majuma sita tangu kujifungua (km umejifungua kwa njia salama, si kwa upasuaji, manake km kwa upasuaji utasubiri kwa muda mrefu zaidi, labda mizezi 6, ili kupata nafuu kamili). Jambo la msingi ni kuzingatia usafi baada ya ngono. Inashauriwa kuwa nawa/oga vizuri mara tu baada ya tendo la ngono kabla ya kumshika/kumnyonyesha mtoto. Pia, kuna nadhariatete nyingine (mafunzo ya dini ya kiislam) ambayo inashadidia kwamba mama anayenyonyesha (miaka 2 tangu kujifungua) hawezi kupata mimba ndani ya kipindi hicho. Hii ina maana kuwa kunyonyesha ni kinga dhidi ya mimba pia (inahitaji utafiti zaidi).

    Hivyo, Alice, ipeni miili yenu kitu inataka. Manake ukweli ni kuwa si mumeo tu anayetaka, hata wewe pia unataka, eehh, au siyo!!

    USHAURI KWA WADAU: Nadhani kuna haja sasa kwa wadau wa globu hii kuwa wastaarabu. Kuuliza si ujinga. Heri ya huyu aliyeuliza, kuliko yule anayekaa kimya. Wewe una mambo mangapi huyafahamu hapa duniani? Umeshauliza mambo mangapi hapa duniani? Hayo unayoyajua uliyajuaje km si kwa kuuliza au kujifunza? Kila maarifa yana mwanzo wake. Kuna wakati hukuwa ukikijua unachokijua leo, Sasa km wewe ulishawahi kuuliza, kwanini watu wanoomba ushauri ktk jukwaa hili hutukanwa, hudhauliwa, huzomewa, huzodolewa.....? Wengine wetu tuko mashuleni tunasoma/tunajifunza. Ukweli ni kuwa kusoma ni kuuliza pia. Tukumbuke kuwa "We never stop learning!" (Kamwe hatukomi kujifunza au Elimu haina mwisho, ukipenda).

    ReplyDelete
  12. We dada yangu, acha imani potofu, hebu kwanza nikuulize mtoto ana umri gani na je baada ya kujifungua ulipata matatizo yeyote kama huna tatizo na ni baba wa mtoto basi acha uchoyo shauri yako. Na kama unapata maumivu basi nakushauri uende ukawaone wataalamu wa magojwa ya kinamama walioenea sehemu zote hapa Dar kwa ushauri zaidi la sivyo mh sisi hatukakusaidia ukiachwa

    ReplyDelete
  13. KAMA WENGINE WALIVYO KWISHA ELEZA WEWE UZIDI KUMPENDA MUMEO CHA KULA CHAKE NI MUHIMU SAAAANA KWANZA USHUKURU MUNGU ANAKUTAMANI NA KUTAKA CHAKULA KUTOKA KWAKO...CHA KUZINGATIA NIKUTOPATA MTOTO MWINGINE BILA YA KUPANGA. TUMIENI CONDOMU KAMA UNA WASIWASI."CHAKULA YA BABA NI MUHIMU, HAIWEZIKUHARIBU MTOTO" MIMI NA MDOGO WANGU TUMETOFAUTIANA KWA MIEZI 14. INA MAANA KUWA NIKIWA NA MIEZI MI TANO (5) MAMA ALIPATA UJAUZITO. WOTE TUMEKUA VIZURITU. HUU NI MFANO MOJAWAPO LAKINI IPO MIFANO MINGI SAANA...MPE BABA CHAKULA CHAKE.

    ReplyDelete
  14. Duh sekta ya malavidavi watu wanajituma kweli na kujitutumua hahahaaaaa mi nashukuru sana mmempatia mafunzo na maelezo mazuli san wala hana haja ya kwenda clinic tena dada mpe mzee vituziiii kama alivyovizoea aendelee kula raha duniani hureeeeeeeeee!!!!!

    Mdau Jamaica

    ReplyDelete
  15. Dada uliyetoa ushauri wa Depo-Provera; ingawa ni ushauri mzuri, naomba niseme kwamba hii kitu siyo kwa kila dada. Kama wewe hujapata madhara yoyote, una bahati. Lakini wengi wanapata 'side effect'. Mimi nilichoma mara moja tu na nikaacha haraka sana. It was severely bad. Muwe waangalifu.

    ReplyDelete
  16. Kwa ninavyo fahamu mimi ni kwamba kubemenda mtoto hutokea hivi
    1. Homoni zitumikazo kumstimulate mama mtoto kwa ajili ya kufanya mapenzi ndizo hutumika pia kutengeneza maziwa ya mtoto, sasa zikitumika huko, content ya maziwa ya mtoto hupungukiwa baadhi ya virutubisho na hivyo kumfanya mtt akose vitu muhimu kwa ukuaji wake
    2.Na athari utokea zaidi ikiwa mtoto hajafikisha miezi sita na inashauriwa kutofanya mapenzi kwa kipindi hicho hata kama ni mmeo,
    3. tafadhari subiri mtt afikishe miezi 6 hapo atakuwa ameshapata virutubisho muhimu

    ReplyDelete
  17. Hii ni changamoto kwa wanaotoa mafunzo kwenye kitchenparty, mara nyingi wanasahau kutoa mafunzo ya uzazi wanafundisha kumfurahisha mume tu lakini baada ya kujifungua wanasahau kutoa elimu ya uzazi.wengi waliotangulia wameeleza kwa ufasaha na ndivyo ilivyo, usafi baada ya chakula cha usiku ni muhimu kuoga vizuri kabla humjamnyonyesha mtoto.

    ReplyDelete
  18. Kama mtaalam wa saikolojia naweza kusema kwamba malenga wetu walitumia njia mbalimbali kuepusha nusu shari enzi ile ya zamani mathalani kuwakataza kina mama wajawazito wasile mayai wasijeota vipara ilhali wakitaka msaidia mtoto asipitilize kukua mama akashindwa kupushi. Halikadharika hili la kubemenda linamantiki yake katika usafi. Labda baada ya kuzingatia usafi wako wewe mwenyewe baada ya tendo na kabla ya kumhudumia mtoto wako, mumeo pia (nikiamini yeye ndiye baba wa mtoto) azingatie usafi kwa kuhakikisha hatoki nje ya ndoa kipindi hiki. Hapo mtoto habemendwi.

    ReplyDelete
  19. kama ni baba halali wa mtoto mpe vitu. ila kwenda nje haitakiwi ukiwa unanyonyesha. lumi dsm

    ReplyDelete
  20. wee dada mshamba,!!!!!!!! mie mwanamke mwenzio, nina watoto wa-2, na walipokuwa wachanga, nilikuwa nakamua kama kawa! Hakuna kitu kinachoitwa kubemendwa! Labda hivi....Ukibeba mimba, na kumnyonyesha mwanao anaweza kudhurika na maziwa, lakini ndugu yangu.....kamua kama kawa

    ReplyDelete
  21. we uliyeandika comment ya tatu kujifanya msomi ni kiroja!unajitia ujuzi huna lolote. baada ya kusoma comment yako ndo nimekuona goat!shule gani umesoma hiyo? dada mtoto haaribiwi na baba mtoto.

    ReplyDelete
  22. Jamani jamani, hakuna kitu kinaitwa kubemenda katika ulimwengu huu!
    Iwe ni kwa mmueo au si kwa mmeo,
    La msingi zingatia kutopata mimba na maambukiuzi ya magonjwa ya Zinaa ikiwa ni pamoja na VVU.
    Ninyi vilaza mnaosema kubemenda kupo mlisoma wapi? au bado mko karine ya 16?
    Theory hizi za kubemenda zilikuwa zinatumika na Babu zetu kama si nyanya zetu kama mojawapo ya njia za kucontrol uzazi, baba hapewi kitu hadi miaka miwili.
    kwa sasa dhana hiyo haipo.
    Hao wanaosedma watoto wanabemendwa si kweli but wanapata utapiamlo, sababu ni kutokuwa attentive kwa mtoto mara mama anapopata ujauzito mwingine.
    mlishaona watoto wa Kihindi, wnapishana miezi na unakuta yako health kinoma.

    !

    ReplyDelete
  23. Mdau wa MasakiNovember 16, 2010

    Akina Dada,

    Kuna huduma ya SMS ya ushauri wa uzazi. Ni bure kwani hulipii SMS wala zinazoenda wala majibu yanayokurudia, na ni hivyo kwa mitandao yote ya Tz. Na ni huduma inayotambulika na Wizara yetu ya Afya na Ustawi wa Jamii, pamoja na kufadhiliwa na wahisani kadhaa.

    Huduma hii inaitwa M4RH, ambayo kirefu chake ni "Mobiles for Reproductive Health". Ilifanyiwa majaribio Kenya kwa Kiingereza, kisha kutafsiriwa kwa Kiswahili na kuzinduliwa pia Tanzania.

    Upeleke SMS yenye neno la "M4RH" (bila hivyo vibano vya "") katika namba 15014. Baada ya dakika chache, utapata jibu linalosema "Karibu kwenye huduma bure za maelezo ya uzazi wa mpango (M4RH)"

    Kwenye majibu hayo, utapewa orodha ya huduma za aina mbalimbali, kila moja ikiwa na namba yake. Hivyo, ukishachagua mojawapo, unafanya SMS ya REPLY, na kuiandika hiyo namba katika ujumbe wako. Utakapopata majibu, unaweza pia kupewa namba ningine uchague kupata ufafanuzi zaidi, au urudi mwanzo tena.

    Kwa taarifa zaidi, pamoja na mifano ya matumizi, unakaribishwa kutembelea:
    http://www.fhi.org/en/Research/Projects/Progress/GTL/mobile_tech.htm

    Hii huduma ni mpya na bado haijatangazwa kwa mapana ili kuwasaidia akina dada zetu waishio mbali na maeneo yanayotoa huduma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...