NYUMBA / APARTMENT
INAHITAJIKA DAR-ES-SALAAM.

WADAU, NAHITAJI NYUMBA YA KUANZIA VYUMBA VIWILI MPAKA VINNE. IWE FULLY FURNISHED, SEHEMU NZURI NA ULINZI WA KUTOSHA. MAJI, UMEME, SEHEMU YA KUEGESHA GARI NA BARABARA INAYOPITIKA.

NI MATARAJIO YANGU KUIKODISHA NYUMBA HIYO KWA KIPINDI CHA MIEZI 2 KUANZIA TAREHE 15/12/2010 LAKINI KUNA UWEZEKANO WA KUONGEZA HADI MIEZI SITA.

NAOMBA MDAU YOYOTE MWENYE NYUMBA NZURI AMBAYO INAKIDHI VIWANGO HAPO JUU TUWASILIANE KWA E-MAIL
NITASHUKURU KAMA UTAAMBATANISHA NA PICHA ZA NYUMBA YAKO, FURNITURE ZILIZOMO NDANI, NA MAELEZO YOTE MUHIMU KAMA NAMNA YA MALIPO NA MASHARTI MENGINE YA MKATABA.

WASALAAM.

MDAU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. kama unataka nyumba nzuri za kuanzia vyumba 2 nenda mlimani city utapata vizuri zaidi full furnished,road za kuingia na kutoka ziko bomba,ulizi ni wa kumwaga,umeme,maji na vitu vingine ni bomba tu.

    mdau Karia.

    ReplyDelete
  2. mdau Karia.....

    mimi pia nina hitaji kama hilo ila kama kwa wiki mbili tu, tafadhali unaweza kutuwekea mawasiliano yao hao mlimani city maana cha ajabu karne hii hawana website kweli??

    na unaweza kutujuza kama unajua kiasi gani na terms zao plz plz plz

    Asante Mdau

    ReplyDelete
  3. swahiba wangu mbona kuna apartments kibao zimejaa maeneo ya upanga kariakoo hata city centre, pochi lako tu ila kama unataka za kwetu wahapahapa hizo ni bila samani na ni kuanzia miezi sita na kuendelea. Mimi ninayo moja kubwa tu yenye vyumba vinne, viwili vinajitegemea na sebule na dining na jiko na public washroom iko Picha ya ndege kibaha kilomita 48 toka mjini dar es salaam sehemu tulivu kuna maji na umeme na eneo la maegesho. Tuwasiliane swahiba...huku ndiko kuwezeshana kwa wazawa. napatikana 071 321 1726

    ReplyDelete
  4. kwa nini usijenge ya kwako?

    ReplyDelete
  5. Mkuu Laizer,

    Ninatafuta apartment ambayo ipo city center kwa mwezi mmoja na nusu; vipi unaweza kunipa contacts?

    ReplyDelete
  6. Anayehitaji ni yupi sasa?

    ReplyDelete
  7. Anonymous..nipigie nikupe contacts..lakini si unajua tena kazi ya udalali?
    waswahili tunasema bakhshish...iwepo

    ReplyDelete
  8. Kwa jinsi ninavyowafahamu wabongo ni lazima uuziwe mbuzi kwenye gunia...wabongo tumekuwa matepeli sana hasa kwenye masuala ya kupangishana nyumba na kuuziana viwanja.

    ReplyDelete
  9. Mimi ninayo iko kipunguni maeneo ya moshi bar. Lakini maji ya kutoka chini ya mwamba yaani ya kisima cha ku-drill. umeme upo. contact: resalindajenes@yahoo.com

    ReplyDelete
  10. jamanini msinishambulie nipo nje ya point nalielewa hilo natafuta mwl anayefundisha kizungu kiinglish nakipenda sana lakini sikijui plz anayejua aniambie huyo mwl

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...