Waziri Mkuu mteule wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimwelekeza jambo Mbunge wa jimbo la Vunjo Mh. Augustino Mrema wakati walipokutana leo viwanja vya bunge mjini DodomaMwanasheria mkuu wa Serikali jaji Frederick Werema akimpongeza Waziri mkuu mteule Mh. Mizengo Pinda mara baada ya jina lake kuthibitishwa na wabunge katika nafasi ya waziri mkuu leo Bungeni Dodoma. Waziri Mkuu mteule Mh. Mizengo Pinda akitoa hotuba kwa wabunge mara baada ya kuthibitishwa na wabunge katika nafasi ya uwaziri mkuu.



SPIKA ANNE MAKINDEA AKIMTANGAZA MH. MIZENGO PINDA KUWA WAZIRI MKUU MTEULE. BAADAYE KURA ZA KUMDHIBITISHA ZIKAPIGWA NA MATOKEO NI KWAMBA:

KURA ZILIZOPIGWA: 328

KURA ZA NDIO: 277 (84.5%)

KURA ZA HAPANA: 49 (14.9%)

KURA ZILIZOHARIBIKA 2 (0.2%)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hivi nao wabunge wanaharibu kura kivipi? Watakuwa wa chadema hawa

    ReplyDelete
  2. Ebu punguzeni mchecheto, anne makindea ndio nini?????? sema anna makinda na sio anne

    ReplyDelete
  3. Naona michuzi umekuwa mfaransa sasa ..huwezi tena kuspeli A badala yake unaweka E .. nini.. AnnE MakindEA..(Anna Makinda)

    ReplyDelete
  4. Jamani ile bahasha yenye jina la waziri mkuu Raisi na Spika walikabidhiana wapi? Mie nilikuwa najua kuwa inatakiwa kukabidhiwa Bungeni kwa spika pale mbele kwenye kiti chake? Kwenye ile picha chini inaonekana Spika aliitwa kwenye Hotel?? au Ikulu?? na kukabidhiwa Bahasha ya jina la waziri Mkuu? Je, hii tutajuana kama halitavuja manake Spika alikaa nayo toka asubuhi hadi jioni ndio akatangaza jina na waziri mkuu. Naombeni Protocol ya hili tukio jamani katiba inasemaje? Jina la waziri mkuu litakabidhiwa kwa Spika wapi?

    ReplyDelete
  5. Kwani hayo uliyo andika 'Nilikuwa najua' ulijuaje? Kama huna ref. uliza tu protocali bila kuweka 'ujuaji' wako Mdau!

    ReplyDelete
  6. Mhe. Rais Kikwete,
    Ahsante sana kwa kumuamini na kuridhika na utendaji wa Mhe.Pinda na kumteua tena kuwa Waziri Mkuu. Watanzania wanayo imani nanyi kuwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010-2015 itaendelea kuwa ya kiwango kikubwa na kasi nzuri. Ndugu Pinda, imani ya Rais Kikwete kwako ni tafsiri ya matamanio ya wananchi katika serikali kuleta maendeleo. CCM UK iko bega kwa bega nanyi.

    MAINA OWINO
    CCM UK

    ReplyDelete
  7. Jamani tunavyomkosoa MICHUZI wakati mwingine tuwe na data JINA LA SPIKA SIO ANNA NI ANNE HAPO MICHUI HAJAKOSEA

    ReplyDelete
  8. Sio Michui ni Michuzi hahahahaha usimuharibie Michuzi jina. Joke tu hizi Mwanzo Michuzi ulikosea Asilimia naona umebania Comment hahaha. Pinda Oyeee MZ.

    ReplyDelete
  9. Wewe Mdau Tarehe Tue Nov 16, 09:40:00 PM,
    Mimi Najua kanuni ya 25 (1 na 2), inasema baada ya kuapishwa kwa spika na wabunge, rais atapeleka bungeni jina la mbunge aliyemteua kuwa waziri mkuu na baadaye Bunge litamuidhinisha.
    Sasa hapo Raisi Hakupeleka jina, ila alimwita Spika kwenda Ikulu kuchukua jina. Anatakiwa kupeleka jina Bungeni sio kumwita Spika kwani huo ni muhimili mwingine

    ReplyDelete
  10. Wewe Tue Nov 16, 09:40:00 PM
    Angalia ibara ya 51 (a) ya mwaka 1977, Rais wa Jamhuri ya Muungano atateua jina moja la mbunge na kulipeleka kwa Spika wa Bunge ili liidhinishwe na wabunge.
    Haijasema Rais atamwita Spika,bali Rais 'atalipeleka' yaani Rais anatakiwa kwenda kwa Spika SIO Spika kwenda kwa Rais.

    ReplyDelete
  11. PINDA HOI.. Hapo Rais umeonyesha uungwana kwani kama kiongozi huyo Mh PINDA ni mfano wa kuigwa na wengine wangekuwa wakweli na wawajibika hivyo basi ninaamini Tanzania yenye neema itawezekana...tunasubiri Baraza la MAWAZIRI SASA..!

    ReplyDelete
  12. I support the nomination 100% we need more leaders like Pinda , who are humble, know that they are there to serve the people , are selfless and not corrupt ...excellent choice!

    ReplyDelete
  13. A very good PRIME MINISTER.Please this term have your directives obeyed strictly regarding money minting seminars, expensive cars,and other luxuries because the t tax payers cannot afford anymore.Put under control offices which are out of control because many ministries are becoming uncontrollable.This is our humble request to you sir.please also revise salaries of doctors and teachers.WISH YOU LUCK.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...