KOMBOLELA SHOW JUMAMOSI HII Novemba 13, 2010 @ 01:00pm - 02:00pm EST, 3:00pm -10:00pm East African Time
Edmond Lyatuu Kutoa Tathmini ya Uchaguzi!
Kama tunavyojua mwaka huu ulikuwa mwaka wa uchaguzi. Matokeo ya uchaguzi yametoka na Mheshimiwa Jakaya Kikwete ameweza kutetea nafasi yake ya urais.
Mbali na hilo, mengi yamejitokeza katika uchaguzi wa mwaka huu, ikiwa ni pamoja na vyama vya upinzani, hususan Chadema, kuongeza viti vyao vya uwakilishi Bungeni. Kwa sababu hiyo, kuna mambo mengi ya kujiuliza, kutafakari na kupambanua kuhusu mwelekeo wa kisiasa Tanzania kwa siku za usoni.
Radio Mbao kupitia Kombolela Show itakuwa na mahojiano na Edmond Lyatuu kujua yaliyojiri kwenye uchaguzi mwaka huu, mtazamo wake juu ya mustakhabali wa taifa la Tanzania na mengine mengi.
Edmond Lyatuu ni mtanzania aliyeishi Marekani kwa muda mrefu na sasa ameamua kurudisha majeshi Tanzania ambako anajishughulisha na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na uchungaji, biashara, ushauri, n.k.
Jiunge nasi kwa kupitia hapa..Usikose Uhondo!!!
Real Life Gospel Show Sunday November 14, 2010 @ 04:00-06:00 EST
Dada Lulu Massawe Kuchambua Swala la Mahusiano.
Kama tunavyofahamu, swala la mahusiano ni swala nyeti sana. Katika nchi nyingi zilizoendelea zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya watu wanaooana wanapeana talaka na hali hii inaendelea kuenea hata kwa nchi zinazoendelea.
Familia nyingi duniani zinaonekana kuyumba na vijana wengi wanasita kuingia kwenye ndoa. Ni kitu gani kinasababisha hali hii? Je kuna tumaini lolote katika swala zima la mahusiano? Kama umekutwa na hali hizi utafanya nini?
Dada Lulu Massawe wa jimbo la California nchini Marekani atategua kitendawili hiki. Dada Lulu ambaye ni mzaliwa wa Tanzania amehusika kufundisha katika semina na mikutano mbalimbali katika majimbo mbalimbali ndani ya nchi ya Marekani.
Je ni muhimu kufuata misingi ya ndoa, familia, na mahusinao kwa ujumla sawasawa na neno la Mungu?. Usikose uhondo wa kipindi hiki Jumapili hii Novemba 15, 2010 saa sita usiku kwa saa za Tanzania (04:00pm EST). Tuungane kujifunza pamoja kupitia www.radiombao.com.
kusikiliza live, bonyeza hapa http://cp.radiostreamhost.com/radio/player.php?station=kpentertainment&nc=6503393
Utawala,
Radio Mbao
http://www.radiombao.com

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...