Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Taasisi ya UTSS (Under The Same Sun),Peter Ash akizungumza na Katibu wa Elimu Mkoa wa Mwanza (hayupo pichani) wakati alipomtembelea ofisini kwake mapema leo asubuhi.kushoto ni Mkurugenzi Muendeshani na Masuala ya Utawala wa Taasisi ya UTSS,Paul Ash.Katibu wa Elimu Mkoa wa Mwanza,G. Sahani (aliesimama) akiwakaribisha wakuu wa Taasisi ya UTSS kutona nchini Canada ambao wamewasili leo jijini Mwanza kwa ajili ya kutembelea shule za Jelly's na Lake View zenye watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albino) ambao wanahudumiwa na Taasisi hiyo.
Mmoja wa Watoto wenye Ulemavu wa ngozi (Albino) anaefahamika kwa jina la Manyashi Emmanuel ambaye anasoma katika shule ya Jelly's ya jijini Mwanza.Mtoto huyu ni mmoja kati ya watoto walionusurika kupoteza maisha kutokana na imani potofu na zenye ushirikina ndani yake ambapo Dada yake aliefahamika kwa jina la Mariam aliuwawa na watu hao.
Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Taasisi ya UTSS (Under The Same Sun),Peter Ash (kulia) akiwa na Mkurugenzi Muendeshani na Masuala ya Utawala wa Taasisi hiyo,Paul Ash (kati) wakiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi hiyo,Vicky Ntetema wakati walipofika katika shule ya Jelly's eneo la Nyasaka kata ya Nyakato jijini Mwanza leo.
Mtoto mwenye Ulemavu wa ngozi (Albino), Manyashi Emmanuel akiwa na ndugu zake ambao wote wanasaidiwa na Taasisi hiyo baada ya kuwachwa na Wazazi wao.Kulia ni Damacha Emmanuel (7),anaefuata ni Mindi Emmanuel (13) ambaye ndie aliesaidia kutoa ushahidi Mahakamani na kufanikiwa kukamatwa kwa baadhi wa watuhumiwa, na mwisho ni Jeremia Emmanuel.
Mwenyekiti wa Shilikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Mwanza,Alfredy Kapole (katikati) akimueleza maswala mbali mbali yahusuyo Shirikisho hilo,Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Taasisi ya UTSS (Under The Same Sun) yenye makao makuu nchini Canada,Peter Ash (kushoto) pindi alipotembelea ofisi za Shilikisho hilo mapema leo asubuhi.kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho kwa Mkoa wa Mwanza,Mwl. Mashaka Tuju.
Bw. Peter Ash akionyesha utofauti uliopo kati ya Mzungu wa kawaida na Mzungu yeye ambaye ana Ulemavu wa Ngozi na kuwataka watoto woote wenye Ulemavu wa ngozi kujiona ni sawa na watu wengine na wala hawastahiki kutengwa.
Bw. Peter Ash akiwa amekaa chini na watoto mbali mbali wenye Ulemavu wa Ngozi katika shule ya Msingi na Sekondari ya Jelly's iliopo maeneo la Nyasaka kata ya Nyakato jijini Mwanza.
Jengo la Ofisi ya Shilikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Mwanza.
Mdau George Njogopa akimsaidia mmoja wa Watoto wenye Ulemavu wa Ngozi kumvisha miwani.
Safari ikiendelea..
Baadhi ya wadau waliopo katika msafara huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Wazungu ajabu sana wameweza kupata madawa na makrimu ya kumwacha mtu mweusi kuwa mweupe na wameshindwa kupata madawa na mkrimu ya kumfanya albino kuwa mweusi au hata hadharani waepuke na mauaji, hamna njia ila hio tu kuwatafutia vidonge za kuwabadilisha rangi ndio itasaidia.

    ReplyDelete
  2. Huko kuweka mikono kwenye meza
    kuna ashiria nini? next time uncle,simama wima.km mtaalamu wa body language.hiyo ni nerves na disinterest.
    keep up the good work.

    ReplyDelete
  3. Yakhe, sijui, nikuite, Sapientologist?

    Mbona umechagua ya hiyo mikono tu na kuacha "body languages" nyingine hapo pichani?

    Wengine wakikusoma watafikiria kuwa unataka ueleweke kuwa hao wageni hawako 'interested'?

    Ingawa mikono ya namna hiyo kwa Wazungu inaashiria nervousness, insecurity or anxiety’ au kwa maneno yako, ‘nerves na disinterest’au kwa maneno mengine zaidi ‘frustration, restraint, anxiety or negative thoughts’, ingefaa zaidi kuwauliza hao Wazungu wenyewe!

    Hata hivyo, sidhani kuwa hiyo ‘nerves’ na disinterest’ ni kutokana na hayo yanayozungumzwa au waliyoyaona!

    Mimi nafikiri kuwa wako hivyo kutokana na mazingira ya hao ndugu zetu ma-alibino! Yaani, ‘plights’ za ma-alibino wetu ndizo zinazojenga ‘nerves na disinterest’ au kwa maneno mengine zaidi: ‘frustration, restraint, anxiety or negative thoughts’

    Wanasikiliza kwa makini ili waweze kujenga mazingira ya ‘calmness, security na reassurance’ kwa hao ma-albino wetu. Ni matumaini yangu kuwa hicho ndicho kitovu cha ujio na ugeni wao.

    Kamwe, hawaonyeshi ‘negativity’ inayoweza kuandamana na maneno 'nerves' na 'disinterest'; hawakuwekewa bunduki kichwani na kuletwa kwa lazima kuzuru sehemu hizo! ‘Plights’ za ma-alibino wetu zimewakuna vichwa!

    Thanxs kwa kuleta yasiyoweza kuonekana au kueleweka kwa wengine.

    Na wewe, keep up the good work!

    Msomaji na mchangiaji wa michuzi.blogspot.com

    ReplyDelete
  4. Anony 11:51pm.Naona hujamuelewa huyo Bwana anaitwa June.
    Yeye amehoji kuhusu Katibu wa Elimu wa mkoa kuibinukia meza kwa mikono wakati akitoa maelezo kwa hao wageni.Yeye hazungumzii body languages ya wazungu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...