MBUNGE wa jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi 'Mr Sugu' akimwaga mistari ya 'free style' kwa wanahabari waliokuwa katika viwanja vya bunge, mjini Dodoma jana, mara baada ya kuwasili hapo kwa shughuli za bunge. Picha na John Bukuku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hello!

    Usiibane hii. Nampa hongera SUGU kwa jitaada kubwa.
    Kwa ufupi ukiuliza mafanikio ya SUGU ya historia, Nadhani kati ya wabunge wote waliongia SUGU anayo sababu ya kujivunia.

    Ndie muasisi wa Bongo fleva, ama mziki wa kizazi kimya. Tangu hapo vijana wengi wajizolea ajira na pesa za kutosha. Huyo ndo mr Sugu.

    Ndie mwanzilishi wa Maralia haikubariki. Japo kuna watu walirukia na kumpora na kuanza kumchafua jina kwa vile walikuwa na vyombo vya habari. Nao polisi hawakusita kumsumbua. Lkn watanzania wamempa heshima yake. Mungu hutuza kwa kila jema tulitendalo. kuna watu waliiapa kuwa hawatamuita Mh. Sasa ole! wakubali tu.

    ReplyDelete
  2. Anonymous 12:51:00 AM, Nakuunga mkono na mguu pia hawa jamaa walisaau Sugu alishawai imba Sugu ni kama mvua na uwezi kuzuia mvua, na kuna mistari aliwaambia kuwa yeye alianza kuimba toka AM enzi David Wakati Mkurugenzi RTD. He made it, na wapo waliokuwa wanasema hawezi kupata now he is in there, Mheshimiwa Joseph 'May, 2 Proud, MrII, Sugu' Mbilinyi

    ReplyDelete
  3. Annoy wa 12:51 kula GWARA.umeongea ukweli mtupu huyo ndo 'SUGU' bwana amefanya bidii na MUNGU kamuongoza ndoto zake zimetimia.sasa sijui RUGE ataendelea kupika majungu ama atakaa kimya.kaazi kweli kweli lol.
    Mdau-UGHAIBUNI.

    ReplyDelete
  4. HAHAHAHH KWA WALEEEEE.................HII INAITWA MALIPO HAPA HAPA DUNIANI

    ReplyDelete
  5. Big up SUGU japo nakukumbuka sana na mashairi yako wakati waitwa 2 proud..kweli umezihilisha wewe ni mvua na kamwe huwezi izui mvua "japo nasikia kuna watabe wanaizuia,sijui hii sayansi ya asili ina ukweli?" la dhahili ni kuwa huwezi kuikwepa mvua..itakunyeshea tu..kwa RUGE na timu yake ambayo inataka kumonoporise soko la mziki na mji umeonyesha ww ni nani na iwe fundisho kwa vijana wengine msikubali kukatizwa na baadhi ya watu kwani muweza ni allah tu..ujumbe Gadina mweshimu san huyu jamaa, ndo alimtoa my wife wako kwa kumpa chorus tu kwenye money money pesa...

    ReplyDelete
  6. Mdau wa Bongo FlevaNovember 13, 2010

    Oya anon wa kwanza hapo juu Sat Nov 13, 12:51:00 AM.

    Ni vizuri kumfagilia Sugu kwa kushinda Ubunge. Hata mimi namkubali huyu kamanda.

    Ila linapokuja suala la mwanzilishi wa Bongo Fleva ni vizuri kuweka rekodi sahihi.

    Msanii wa kwanza kabisa kutoa single na album ya nyimbo za kufoka foka kwa Kiswahili ni Mc Salehe Jabri toka Zenji. Alitoa album yake iliyokwenda kwa jina la "Swahili Rap" mwaka 1992. Album hiyo ilikuwa na vibao maarufu kwa Kiswahili kama vile Ice ice baby, OPP, n.k. Na ilivuma sana kwa sababu kilikuwa ni kitu kipya kabisa enzi hizo kurap kwa Kiswahili.

    Sugu alikuja kutoa album baada ya Salehe.

    Pia neno Bongo Fleva lilikuja baadae zaidi. Lilibuniwa na mtangazaji wa Clouds FM (jina nimemsahau). Hivyo wakati Salehe Jabri anatoa album ya "Swahili Rap", na wakati Sugu anaingia kwenye gemu music huo ulikuwa unajulikana kama swahili rap tu.

    Salehe alipotea kabisa kwenye anga za music baada ya kutoa album hiyo. Hakutoa nyingine tena, au kama alitoa basi haikuvuma kama "Swahili Rap"

    Sugu ndio akavuma sana miaka hiyo ya 90 kiasi kwamba watu wengi hudhani yeye ndio mwanzilishi wa rap za kiswahili.

    Ni hayo tu. Tusipindishe historia.

    ReplyDelete
  7. nakukubali sugu.juhudi zako zimekufikisha mbali.big up mtu wangu mungu akubariki kafanye kazi kwajuhudi.katete ndugu zako wambeya na watanzania nakujua wewe nimchapakazi.

    ReplyDelete
  8. Mdau hapo juu ndio, Salehe Jabri alitoa hiyo albamu yake ya kiswahili alikuwa msanii wa kwanza kurekodi lakini hakuuza hiyo albamu ilikuwa kwa ubishoo kuonyesha anaweza kurap. Ila hata yeye sio kwa kwanza kuanzisha kurap kwa kisahili kwani tayari kulikuwa na underground wana rap. Kina marehemu Nigga One walikuwa wana rap kabla Salehe ila hakurekodi tuu.
    Sugu alikuwa msanii wa kwanza kuuza kwa mafanikio. Kulikuwa na Kwanza Unity kabla ya hapo ila hawakuuza, walijaribu lakini hawakuwa na mafanikio ya kuuza. Nakumbuka walikuwa wanauza cassette tape kule viwanja vya saba saba wao wenyewe, kina Fresh G, Rhymson na wengine. Wakaja Hard Blasters (Original)d hawakuuza vizuri pia hadi Nigga Jay alipojiunga nao ndio waliweza kuuza. Kwa hiyo hiyo ndio historia fupi ya mziki wa Rap Bongo.

    ReplyDelete
  9. Wewe anon wa sat nov 3,02:02:00pm,asante kwa historia fupi ya muanzilishi wa miziki ya kufokafoka,lakini huyo salehe jabir mbona hakurudi tena?ina maana alishindwa game alikuwa anazuga tu,sugu iko damuni,no matter watu sugu moto chini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...