TEKNOLOJIA MPYA YA UJENZI KUPUNGUZA
UHABA WA NYUMBA TANZANIA

Pichani ni ujenzi wa mfano wa nyumba hizo

Tatizo sugu la ukosevu wa makazi hivi karibuni litapata ufumbuzi nchini Tanzania. Ufumbuzi huu upo karibu sana tofauti na wanavyofikiria watu wengi. Pale Wazo Hill, tarehe 18 Novemba 2010, wadau wa masuala ya ujenzi walishuhudia utengenezaji wa technolojia ya Moladi foamwork ambapo nyumba iliyotengenezwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa kutumia njia nafuu zaidi ambayo hivi karibuni inatarajia kuingia soko la nchini.

Uhaba wa upatikanaji wa makao nchini kwa ajili ya wale waliopo mijini kumeleta ongezeko za nyumba zinazojengwa kiholela. Kumekuwepo na ongezeko la mahitaji ya nyumba na hivi kusababisha uhaba na uhaba huu umekuwa ukiongezeka kila mara. Inakadiriwa kuwa upungufu wa makazi kwenye miji ya Tanzania inafikia nyumba 1.2 milioni.

Moladi Tanzania, ambao ndio wakala pekee wa teknolojia ya Moladi imedhamiria kutoa ufumbuzi wa uhaba wa makazi kwa kutengeneza nyumba kwa kutumia muda mfupi kwa kutumia Moladi formwork. Urahisi na kasi ya teknolojia ya Moladi imerahisisha ujenzi na kwa mafanikio kwenye baadhi za nchi za Afrika kama Zambia, Ghana, Zimbabwe, Angola, Botswana, Mozambique, Nigeria na Afrika Kusini.

Tangu mwaka wa 1986 Moladi imeleta njia mbadala tofauti na ujenzi uliozoeleka na inakidhi unafuu, ubora na uimara. Moladi foamwork ni ya kipekee, nyepesi, inaweza kurudiwa kwa matumizi mengine na yenye gharama nafuu.

Nchi yetu ambayo haina muundo mbinu ya uhakika, Moladi inaleta ufumbuzi ya makazi nafuu yanayoleta maendeleo katika jamii. Teknolojia ya Moladi na uimara wake inapunguza gharama na kuleta makazi imara na madhubuti ambayo inajengwa kwa muda mfupi sana.

Kampuni ya ukandarasi ya Holtan (E.A) ndio kampuni teule nchini Tanzania kwa ujenzi wa Moladi nchini ambapo wanauwezo wa kujenga nyumba nyingi kwa muda mfupi ambayo ni imara na yenye gharama nafuu.

Ushirikiano wa Holtan na Moladi inatokana na kiu ya kukidhi mahitaji ya makazi kwa kutumia mbinu ziliyozoeleka na teknolojia ya Moladi ambayo itachangia maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.

Kuonyeshwa kwa umma kwa mradi huu wa Moladi tarehe 18 Novemba ni ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuifanya Tanzania kuwa ya kwanza kuutumia teknolojia ya kuongeza makazi ya Moladi.

Kwa maelezo zaidi kuhus Moladi Tanzania wasiliana nao kwenye namba ya simu: +255222701588/90
au barua pepe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Lakini nyumba kama hizi zi muamana kweli kwa waizi na majambazi nahisi ni rahisi kuiba na hata kuingiliwa na majambazi wakavunza nyumba, sijui wataalam hawa wanafikriaje ikiwa zina muamana itakua vizuri kwa wananchi wa tanzania kujipatia nyumba kama hizi waishi maisha mazuri na kwa usalama zaidi.

    ReplyDelete
  2. Acheni longolongo hapo kila kitu imported halafu mnasema bei nafuu? Kwani bei ni siri siku hizi, tajeni basi. Mna wasiwasi gani kuweka bei zenu humu wakati ninyi ni mawakala pekee kama mnavyosema hapo juu.
    mimi

    ReplyDelete
  3. Kwa nchi kama Tanzania hii itawarahisishia vibaka kuvamia watu tu. Je si rahisi kwa vibaka kuvunja hayo mabati na kuingia ndani? Nina mashaka sana kama hizo nyumba zinaendana na mazingira yetu ya kukabiliana na vibaka.

    ReplyDelete
  4. lingekuwa jambo la busara kutujulisha gharama ya hiyo nyumba ya mfano ili tutoauishe na nyumba kama hiyo kwa njia tunazojengea, mara nyingi tekinolojia mpya zinapokuja Tanzania huonekana kuwa aghali kuliko njia za asili.

    ReplyDelete
  5. HAYA HALMASHAURI ZETU, THIS IS NICE FOR SHULE ZA KATA NA OFISI ZA SERIKALI

    ReplyDelete
  6. Thanks for thinking positively about human shelter. The main issue is the cost of the house and technical part of the construction style durability and limitation of the style. That would determine whether the style will solve the current housing problem. Otherwise keep it up good job
    Mdau wa makazi

    ReplyDelete
  7. Oohooo jamani, nyumba hizo si ndiyo zile ambazo upepo na hasa wa kimbunga huzing'oa kirahisi na kuzitupilia mbali huku na kule kama inavyotokeaga mara kwa mara kule Marekani na nchi nyingi duniani wakati wa upepo wa vimbunga?. Kisha kwa wezi na majambazi ambao huvunja nyumba za watu kwa ajili ya kuiba kwa nyumba hizo si ndiyo itakuwa ni rahisi zaidi kuzivunja na kuwaibia watu? Jamani ni kweli tuna shida ya nyumba lakini isije kuwa ndiyo yale tunayoambiwa kwamba BURE GHALI!!!. No, we had better think twice or even thrice before commencing to do that.

    ReplyDelete
  8. Hapa mmenikumbusha ule ugunduzi wa mabomba ya mianzi 1994 kutatua tatizo la maji. Hivi kwanini tunaendesha reverse kwenye freeway?

    ReplyDelete
  9. Why a long winded sales pitch which says nothing about what Moladi is, materials used and it's technical qualities?
    Hapa naona ni tangazo la mauzo ya kitu ambacho hakikuelezwa thamani au ubora wake zaidi ya ujenzi unao tumiwa sasa. Je ina tumia materials gani, ni za hatari kiafya labda? Naona maswali ni mengi kuliko jibu walilotowa. Hebu jielezeni zaidi.

    ReplyDelete
  10. zita uzwa bei gani?

    ReplyDelete
  11. HALOOO!! WEE ANON WA 10:28:AM WE NDIO UMESEMA,NI KWELI, HAYAA OFISI ZA SERIKALI, NA SHULE, NDIO PA KUCHANGAMKIA HAPO, WATOTO WENGI TANZANIA BADO WANASOMEA CHINI YA MITI,. KWA HIYO, HIYO NI BORA WAJENGEWE SHULE NA HIYO TEKNOLOGIA SI BEI RAISI TU,

    ReplyDelete
  12. Taaarifa ndeeefu lakini haina mashiko.......maswali mengi kuliko majibu! hiyo moladi ina asili gani? fibre! chuma? Plastic? inachukua muda gani kusimamisha? aaah.....badala kututia hamu mmetubore!

    ReplyDelete
  13. Watu wanaongelea kama hii ni Kampuni ya Serikali, Sasa serikali ndio wanatakiwa waongee nao wawalipe hawa wawajengee Shule za Serikali za Bei nafuu hasa Vidudu na mabanda ya Red Cross Vijijini iwe kama hospitali sehemu ambazo Hakuna hata Matibabu. MZ.

    ReplyDelete
  14. Nyie kweli Watu hawajaona Grand Desgn mmngeenda South africa Uswahilini kule Soweto mngeziona hizi nyumba na nzuri tu Plastic ni kati tu Inasimamishwa Zege la maana hizi ni nzuri sana kwa watu wa hali ya chini moja nafikiri ni TZsh10 million. sasa mafisadi wasije kuingilia tu deal. manake sie walalahoi ndio tunazisubiria. James

    ReplyDelete
  15. Inakadiriwa kuwa upungufu wa makazi kwenye miji ya Tanzania inafikia nyumba 1.2 milioni. hiyo point hapo juu kidogo nikujiuliza sawa upungu 1.2 milioni je Serikali nao watajenga hilo eneo Viwanda? Shule? Hospitali? wakazi wa hapo wakikaa wajue nini wanafanya cha kula kwenye matumbo yao na familia zao au ndio umaskini mwengine uzidi hapo? XtoZ

    ReplyDelete
  16. For technical information on moladi construction technology visit www.moladi.net

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...