Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Taasisi ya UTSS (Under The Same Sun),Peter Ash akizungumza kwa msisitizo mkubwa na baadhi ya watoto wenye ulemavu wa Ngozi wanaosoma katika shule ya Dekapoli iliopo Maswa mkoani Shinyanga leo.
Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Taasisi ya UTSS (Under The Same Sun),Peter Ash akiongea na Watoto wenye Ulemavu wa Ngozi wa shule ya msingi Dekapoli waliofika katika hoteli ya Karena iliopo Shinyanga mjini leo.
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya UTSS,Vicky Ntetema akifurahi jambo na mmoja wa Watoto wenye Ulemavu wa Ngozi ambaye yupo katika shule ya Buhangija iliopo mkoani Shinyanga leo.
Watoto wenye Ulemavu wa Ngozi wakipewa Kofia za kujizuia na jua zilizotolewa na UTSS katika shule ya Buhangija mkoni Shinyanga leo.
Watoto wakisoma moja ya Vitabu vitolewavyo na UTSS.
Mdau Nicolous akiwa na Mtoto Upendo anaelelewa katika shule ya Buhangija ambayo pia ni sehemu maalumu iliyotengwa kwa ajili ya kuwalindwa ndugu zetu hawa ili wasidhuliwe na watu wabaya.
Baadhi ya Watoto walipo kwenye shule ya Dekapoli wakiwa na mafuta ya yenye dawa za kulinda ngozi zao.
Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Taasisi ya UTSS,Peter Ash (kushoto) akionyesha kofia zinazotakuwa kuvaliwa na watu wenye Ulemavu wa Ngozi.kulia ni Mkurugenzi wa Masuala ya Utawala wa UTSS,Paul Ash ambaye ni kaka wa Peter Ash.
Namma ya kutumia mafuta ya kulinda ngozi.
Sehemu ya Mahema yanayotumiwa na baadhi ya Watoto wenye Ulemavu wa Ngozi katika shule ya Buhangija ambayo pia inawalea na kuwalinda Watoto hao.
Baadhi ya wadau wa UTSS kutoka Dar es Salaam wakiwa na viongozi wa Chama cha Maalibino Mkoani Shinyanga.

UTSS imeweza kutoa misaada mingi sana kwa Watoto wenye Ulemavu wa Ngozi katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga,ambapo wameweza kuwasaidia Watoto hao kupata elimu iliyo bora na vifaa mbali mbali vya kuweza kujikinga na jua ambalo ni natizo kubwa sana kwa watu wenye Ulemavu wa Ngozi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. MWENYENZI MUNGU AWAJALIE WOTE WALIOHAMASIKA KUSAIDIA MAALBINO WA TANZANIA. TANZANIA NI MOJA YA NCHI ZENYE MAALBINO WENGI ZAIDI DUNIANI.

    WATANZANIA NASI TUAMKE, TUWAJENGEE UPENDO NA KUWASAIDIA WAAWEZE KUENDESHA MAISHA YAO AMBAYO YANAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA KWA UPANDE WA AFYA HASA YA NGOZI NA CHANGAMOTO KUTOKANA NA TISHIO LINALOWAKABILI LA MAUAJI YANAYOFANYWA NA WATU AMBAO HAWAJUI KWAMBA NA WAO KUNA SIKU WATAKUFA NA WATAKUTANA NA HUKUMU YAO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...