CHAMA cha wachezaji mpira wa miguu nchini (Sputanza),kinaandaa tuzo maalum kwa ajili ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania bara 2010 -2011.
Katibu mkuu wa Chama hicho Said George alisema pamoja na kuwa kumekuwa na tuzo zinazotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), lakini chama chake kinataka kuipa hadhi zaidi tuzo ya mchezaji bora wa soka badala ya kuichanganya na michezo mingine.

"Tuzo za Taswa sawa, lakini tuzo ya mchezaji bora wa soka ina hadhi yake,
tunaanza kuitoa kwa mara ya kwanza ligi hii itakapomalizika na wachezaji ndio watakaopendekeza mshindi."alisema, na kuongezea kuwa kutakuwa na mchezaji bora wa mwaka, mshindi wa pili na wa tatu na
kuwataka wahisani mbali mblai kujitokeza kudhamini tuzo hizo.
Wakati huo huo Sputanza imelitaka Shirikisho la Soka Tanzania chini ya
mwenyekiti wake Leodegar Tenga kuvunja kamati ya kusimamia Maadili na Hadhi ya Wachezaji kwa kuwa imeshindwa kufanya kazi iliyokusudiwa na badala yake ipo kwa ajili ya maslahi binafsi.
Alisema kamati hiyo ambayo inaongozwa na wakili Alex Mgongolwa ambaye pia ni mnazi mkubwa wa Yanga, imekumbwa na mgongano wa kimaslahi kwa watendaji wake kugubikwa na upenzi badala ya kutenda haki.
"Ni wazi Yanga haikufuata taratibu wakati ikivunja mkataba wa wachezaji wake wanne, na ni muda mrefu sasa sakata hili halijapatiwa ufumbuzi, sasa ni dirisha dogo la usajili fursa ya wao kupata timu ya kucheza ni finyu kwa vile uongozi wa Yanga haujawalipa madai yao wanayostahili."alisema George
"Tunaitaka TFF kuizuia Yanga kusajili wachezaji wapya hadi hapo ufumbuzi wa wachezaji wao wanne upatikane, wachezaji hao wamefuata taratibu zote za kudai haki zao lakini wanaambulia danadana isiyo na mwisho, utaratibu wa kuzuia mambo yasipelekwe mahakamani kwa utatuzi wanachama wetu waende wapi?"alihoji George.
Kwa mujibu wa taarifa ya Sputanza kwenda TFF, Yanga inatakiwa kulipa karibu Sh milioni 253 kama gharama ya kuvunja mikataba yao.
Wachezaji hao ambao ni kipa Steven Malashi, John Njoroge, Wisdom Ndhlovu na Ally Msigwa wanaidai timu hiyo kiwango hicho cha fedha kutokana na kusitishwa kwa mikataba yao ambayo ilitakiwa iishe msimu wa 2012.
Mchezaji Steven Marashi anadai Sh milioni 37.5, Wisdom Ndlovu anadai Sh
milioni 82, Ally Msigwa Sh milioni 89.7 na John Njoroge Sh milioni 44.
Alisema mbali na wachezaji hao kulifikisha suala hilo kwenye Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi kwa wachezaji ya TFF. Pia waliwafikishia wao kama chama cha kutetea haki za wanasoka ili liweze kupatiwa ufumbuzi.
Alisema kwamba wachezaji hao wote isipokuwa Ally Msigwa walisaini mikataba mipya ya kuichezea timu hiyo Machi 18 mwaka huu chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa klabu hiyo aliyemaliza muda wake Imani Madega na Katibu Mkuu Lawrance Mwalusako na wanasheria wa wachezaji hao.

George mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ na Coastal Union alisema kwamba wachezaji hao wanaidai klabu hiyo fedha za usajili, mishahara yao ya mwezi na marupurupu mbalimbali yatokanayo na kuichezea timu hiyo katika kipindi chote cha mikataba yao.
"Fedha wanazodai ni nyingi lakini tulishakaa na wachezaji na kuzungumza nao wapewa kiasi kidogo hata milioni 15 au 20 ili wamalizane wasake timu nyingine, tukakaa kikao na kina Mgongolwa wachezaji wakahojiwa kama wamekubaliana na hilo suala la kupewa malipo hayo kiduchu ili wamalize wakakubali lakini cha ajabu mpaka leo hakuna kinachoendelea, hii kamati ivunjwe haitufai."alisisitiza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...