Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda akiingia Bungeni baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo mjini Dodoma. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akila kiapo cha kuwa mbunge wa jimbo la Mpanda Mashariki ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa akila kiapo cha kuwa Mbunge wa jimbo la Monduli ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Hai Mh. Freeman Mbowe akila kiapo cha kuwa mbunge wa jimbo hilo mjini Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Muhambwe, Kibondo-NCCR –Mageuzi, Mh. Felix Mkosamali akila kiapo cha kulitumikia jimbo hilo mjini Dodoma. Akiwa na umri wa miaka 24 tu Mh. Mkosamali ni mmoja ya wabunge wenye umri mdogo walioapa leo. Picha na Anna Itenda na Aaron Msigwa - MAELEZO.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. “I have been in the Parliament for all may life” amesema Makinda akimaanisha kwamba, amekuwa bungeni maisha yake yote na kwamba, kitu kikubwa alichokifurahia katika maisha yake ni kuwa Mbunge

    ReplyDelete
  2. Mkosamali mshikaji vipi mambo?
    Siasa yeyote sio kuzua maneno na mnapozua mnasababisha vurugu ndani ya Bunge”amesema mwanasiasa huyo aliyejiwekea historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Spika wa Bunge la Tanzania.

    Amesema, anasikitika kwamba, kulikuwa na kashfa moja tu katika Bunge lililopita iliyohusu mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura kati ya Serikali na kampuni hewa ya Richmond.

    “Pale zilitakiwa Richmond zaidi ya 10’ alisema Makinda katika moja ya kumbi za mikutano katika Ofisi ya Bunge mjini Dodoma na akabainisha kwamba, wakati mwingine wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani huungana kwenye suala kama hilo.

    ReplyDelete
  3. Ni waziri mkuu mstaafu!

    ReplyDelete
  4. Uzalendo kaka Michuzi uko wapi??? Au ni macho yangu??? Bungeni kapeti lina bendera ya nchi halafu wabunge wanakanyaga. .... Je inamaanisha kua mbunge yupo juu ya nchi au mbunge anatumikia inchi??? Naomba msaada.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...