Habari/Picha Na Francis Godwin,Iringa
MAUWAJI ya kinyama yazidi kutishia maisha ya wakazi wa manispaa ya Iringa baada mfanyakazi mmoja wa kituo cha kuziba pacha za magari katika eneo la Mshindo mjini hapa Nico Chalale (28) kukutwa amekufa kifo cha mashaka kwa kunyongwa shingo usiku wa kuamkia sikukuu ya Krismasi ikiwa ni siku moja baada ya kuchinjwa mfanyabiashara wa samaki Bukuri Mvula na watu wasiofahamika jirani kabisa na eneo hilo.
Kijana huyo alikutwa akiwa amefungwa kamba shingoni huku akiwa amepiga magoti hali inayozua maswali zaidi kwa wakazi wa mjini Iringa na kuingia na hofu zaidi ya kuwepo kwa mtandao wa watu wanaojihusisha na mauwaji hayo.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wakazi wa eneo la Mshindo walisema kuwa kifo cha fundi huyo ambaye mwili wake ulikutwa eneo la kazini kwake unawafanya kuingiwa na hofu zaidi na kuliomba jeshi la polisi mkoa wa Iringa kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya mauwaji hayo.
Wananchi hao walisema kuwa inasikitisha na kutishia uhai wao kuona watu wakiendelea kunyongwa na kuuwawa kinyama katikati kabisa na mji huo wa Iringa .
Kwani walisema kifo cha Chalale ni tukio la tatu kutokea ndani ya kipindi kifupi cha wiki mbili ambapo tukio la kwanza lilikuwa la aliyekuwa kamanda wa kampuni ya ulinzi binafsi ya Force Group marehemu Charlesy Tulo ambaye alikutwa amejinyonga katika mti mfupi unaokisiwa kuwa na futi kama tatu wakati yeye ana urefu wa fupi 5 .
Hata hivyo walisema mauwaji hao hayakuishi hapo kwani siku moja kabla ya Krismasi mfanyabiashara huyo wa samaki Mvulla alikutwa akiwa amechinjwa shingo kama kuku na mwili wake kutelekezwa ndani ya daladala mbovu.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla ametihibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi .

...hata kama wanyeji wa Iringa tuna tabia ya kujinyonga tikichukia hii inatia shaka,inatisha!
ReplyDeleteila haiingii akilini hata kidogo kwan hata aliyezaliwa leo huwezi kumdanganya eti mtu kajinyonga huku kapiga magoti ina mana kajinyongaje??????? ina mana alikua anajikazia mwenyewe kamaba na mikono au mana mi sielewi hebu nisaidieni wadau bora hata huyo aliyechinjwa kesi yake inaonekana wazi kua ni watu wamemchinja sasa hao ndugu waliojinyonga huku kapiga magoti na huyo wa mti wa futi 3 wakati ye ni futi 5 haiingii akilini kabisa hao watakua wamenyongwa
ReplyDeleteWachaga Pesa, Wahaya nanii, Wapare Wabahili, Wagogo Wachafu, Wanyalu wao kamba tu. Kweli mila na desturi, azibadiliki. Mwiindi hata azaliwe namtumbo, atabaki kuwa muhindi tu.
ReplyDeleteHivi nyie mnaosema kwamba wanyalukolo wana tabia ya kujinyonga, jee unawajua wanyalukolo wangapi waliowahi kujinyonga? Mimi ni mzaramo, nimezaliwa na kukulia bandari salama. Nawajua watu kadhaa waliojinyonga na kati yao hakuna mnyalukolo hata mmoja.
ReplyDeleteHayo ni mauaji ya kutisha na hayafanywi na mtu mmoja bali ni kikundi cha watu makatili. na hao watu wanaishi humo humo mjini na kuna watu wanajua ni kina nani ila wanaendelea kunyamaza. tatizo la nchi yetu hakuna kitengo maalum cha kufatilia mauaji kwa uchunguzi wa kina. hakuna njia za kukusanya forensic evidence. hapo kuushusha huo mwili bila ya kukagua mazingira kwa kina tayari washapoteza evidence muhimu ambazo zingewasaidia kukamata wahusika. kwa mfano hiyo kamba walifunga itakuwa na alama ya vidole na hata ngozi za wahalifu ambazo zingeweza kukamatisha wahalifu. pia hapo pana alama za viatu ambazo kwa kutumia POP (Plaster of Paris) wangeweza kupata alama za viatu ama miguu ya watu ambayo ingekuwa vigezo muhimu wakikamata wahalifu walinganishe.huyo marehemu kucha zake zitakuwa na ngozi za wahalifu alipokuwa akijitetea na hivyo DNA kwa kukamata wahalifu...inatia uchungu sana kuona watu wanapoteza maisha kijingajinga na hakuna anaejali..wauaji wako mtaani wakijisifia..na hayo nilosema yanaweza kufanyika kwasababu teknologia zote zipo tanzania ila watumiaji hawapo ama mawazo ya kutumia teknolojia hayapo.
ReplyDeleteWewe uliyesema wahaya nanihii, ni nini hiyo?
ReplyDeleteSaidi umesema ukweli kabisa. Hilo eneo lote ingekuwa ni huku U.S., lingezungushiwa tape ya police inayokataza watu kusogelea ili ushahidi usipotee. Hapo watu wa forensics wangefanya kazi yao na kulinganisha ushahidi na washukiwa (suspects). Ni jambo la kutisha watu wanauliwa kama kuku wanavyochinjwa vile.
ReplyDeleteHalafu maskini mtu wa watu wanaweza wasimzike kikanisa ati kwa vile kajinyonga kumbe si ajabu huyu kauliwa. Tanzania tunahitaji darasa sana. Watu wengi huwa wanajisemea kitu tu bila scientific evidence yeyote. Ajira hamna wakati kazi ziko kabao Tanzania. Hapo wamepoteza ushaidi mwingi tu kwa kujifanya wanajua sana kumbe hawajui lolote...Clock in clock out bila kufanya kazi....Hatuko pride ya kazi zetyu na kuzifanya kwa ufania. Watu bora wa lipwe tu lakini hawajali ubora wa kazi zao.
ReplyDeletewaha wana sifa ya uchafu na roho mbaya. Wasambaa nao wanapenda mno kukaribisha wageni, wale wanaojiita wazanzibari wanapenda sana nanihii, wafipa ni uchawi...
ReplyDelete