Wanachama wa vikundi mbali mbali wakila
'tizi' kujiandaa na Bonanza hilo la fungua mwaka
Kujinyoosha muhimu wakati wa tizi

Chama cha mchezo wa mazoezi ya viungo Zanzibar (ZABESA) kimepanga kuandaa Bonanza litakalofikia kilele chake siku ya Jumamosi ya tarehe 01/01/2011 katika kiwanja cha Amani Zanzibar. Hili ni bonanza ni la pili, baada ya kukamilika lile la awali ambalo lilifanyika tarehe 01 Januari, 2010.

Bonanza hilo litavishirikisha vilabu 20 vya mazoezi ya viungo ambavyo kwa kawaida huwa vinafanya mazoezi katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar. Wiki ya bonanza itaanza tarehe 25 Disemba ambapo itakuwa ni siku ya kufanya rehasal na siku ya jumapili tarehe 26/12/2010 kutakuwa na michezo ya mpira wa miguu, kuvuta kamba nk itakayowahusisha wanachama wa vikundi vya mazoezi katika maeneo mbali mbali ya mji wa Zanzibar.
Lengo kuu la bonanza
Lengo kuu la bonanza hili ni kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kujenga afya zao. Aidha bonanza hili linatoa fursa ya kuvikutanisha vilabu vyote vya Zanzibar vinavyofanya mazoezi ili kuonana, kubalishana mawazo, kuelimishana na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuimairisha afya zao kwa ujumla pamoja na kujenga uhusiano mwema na Serikali na taasisi nyengine za kijamii.

Malengo mahsusi
Bonanza hili linakusudia kufikia malengo yafuatayo:
Kutoa mwamko kwa jamii juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kujenga na kuboresha afya zao.
Kuvikutanisha vilabu mbali mbali vya mazoezi, makocha na wanachama wa vilabu hivyo ili kutembea na kufanya mazoezi ya pamoja ili kujenga umoja, maelewano na upendo baina yao ili kimarisha udugu mingoni mwao.
Kuonesha kwa vitendo kuwepo kwa amani, umoja, uzalendo na mshikamano miongoni mwa wananchi, serikali na taasisi za kijamii za hapa Zanzibar.
Kutoa sauti na kauli ya pamoja juu ya mambo yanayohusu afya ya jamii.

Washiriki katika bonanza.
Bonaza hili litahusisha makundi yafuatayo:
Vilabu mbali mbali vya mazoezi wakiwemo wanawake, wanaume, vijana na watoto; Makocha wa vilabu na viongozi wao; Wabunge, wawalikishi; Mawaziri wa SMZ; Maafisa mbali mbali wa serikali; Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi na Wakuu wa Wilaya za Mjini na Magharibi; Waandishi wa habari; Wasomi na Wananchi kwa ujumla. Pia bendi ya Magereza itaongoza matembezi ili kunogesha shehehe hizi.

Pahala pa kuanzia na kumalizia
Maandamano ya wana mazoezi yataanza saa 12 kamili asubuhi siku ya Jumamosi ya tarehe 01 Januari 2011, katika bustani ya Michenzani-Muembekisonge kuelekea uwanja wa Amani, kupitia Kijangwani, Mfereji wa wima, Mikunguni na kuishia Uwanja wa Amaan na kutakuwa na matembezi ya mchaka mchaka. Wanavikundi watajipanga mistari na makocha na wasaidizi wao watasaidia kuongoza matembezi hayo. Nyimbo za hamasa zitaimbwa kwa kuongozwa na bendi ya Magereza. Wanachama wa vilabu watavaa sare ili kutoa taswira njema kwa jamii.

Mgeni Rasmi
Mgeni rasmi atakuwa Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi ambae atayapokea rasmi maandamano ya vilabu hivyo katika uwanja wa Amani na kuwahutubia wana mazoezi na wananchi kwa jumla. Kabla ya hutuba, wanamazoezi watasoma risala yao kwa mgeni rasmi. Wafadhili wakuu watapewa muda mfupi kuongea.

Ujumbe wa mwaka huu ni:
”Mazoezi kwa afya bora, umoja na upendo”

Washirika wakuu katika Bonanza hili?
Bonanza hili litawashirikisha wadau mbali mbali. Mbali ya vilabu vya mazoezi ya viungo ambavyo ndio waandaaji wa Bonanza hili, pia linatarajiwa kuwashirikisha wadau mbali mbali kwa kutoa michango yao ya hali na mali katika kufanikisha sherehe hii.
Mingoni mwa wadau hao ni pamoja na:
Jeshi la Polisi, Red cross, ZFA, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na taasisi za serikali, Vyombo vya habari (STZ, Zenj FM, Bomba FM, HITS FM, Zanzibar Cable, TVZ, STZ, TBC taifa, Star TV and ITV, Magazeti ya Zanzibar Leo, Blogu ya Issa Michuzi na Mzalendo.net. Pia wananchi wanaalikwa kushiriki, na wanaombwa kufuata utaratibu utakaowekwa.

Matokeo yanayotarajiwa
Baada ya Bonanza hili, tunatarajia matokeo yafuatayo:
Kuvikutanisha vilabu mbali mbali na viongozi wao na kuimarisha umoja na mshikamano. Pia washiriki wataweka sawa mwili na misuli na kutaka mafuta mwilini. Aidha, washiriki watajuana na kujenga umoja na mshikamano na kupendana zaidi, wananchi watahamasika kufanya mazoezi na pia watapata elimu juu ya afya zao. Aidha, bonanza hili litaimarisha ushirikiano kati ya serikali, vilabu vya mazoezi na wananchi kwa jumla.

Imetolewa na Kamati ya maandalizi ya Bonanza la Pili la ZABESA
kwa maelezo zaidi, wasiliana na Katibu
+255777859646, +255777415340.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...