
Mgeni rasmi kwenye hafla ya kuchangisha pesa za mpango wa Somesha Mtoto wa Kike (SOMKI) inayoandaliwa kila mwaka na Unity of Women Friends (UWF) Mama Margaret Chacha, Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), akitoa hotuba wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kibo hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar usiku wa kuamkia leo

Mama Margaret Chacha akizindua
tovuti ya UWF kwenye hafla hiyo

Mshereheshaji Baby Kabaya akitangaza kwamba jumla ya shilingi milioni 47 zimepatikana katika hafla hiyo ya hisani ya SOMKI

Mama Margaret Chacha akitangaza washindi
wa bahati nasibu iliyochezeshwa

Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla hiyo

wadau mbalimbali kwenye hafla hiyo

Meza ya kampuni ya mafuta ya TOTAL ilisheheni vilivyo

Mnunuzi wa picha ya mtoto wa kimasai (mwenye buluu) akikabidhiwa mzigo wale alioununua kwa dola za kimarekani 1,500 katika mnada uliopitishwa kwenye hafla hiyo

Mshindi wa simu ya Nokia na muda wa maongezi wa shilingi 50,000 akikabidhiwa zawadi yake baada ya kushinda bahati nasibu

Mdau akifurahia zawadi ya blender toka Mini Argos aliyoshinda kwenye bahati nasibu

Mama Chacha akiwa na wana UWF baada ya kuzindua tovuti yao

Meza kuu pamoja na wanachama wa UWF na waume zao. Walioketi toka kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngereja, akifuatiwa na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndullu na mgeni rasmi Mama Margaret Chacha
watoto wetu wa kiume hakuna kusoma kuanzia mwakani loh, nami naanzisha ya kwangu somesha mtoto wa kiume kwanza, sawa?
ReplyDeleteNimependa hii kweli ilikuwa hafla ya somesha mtoto wa kike hata kwa idadi kubwa ya akina mama wanao onekana hapa wamevaa ki kike hasa wale wanawake wa kitanzanai tunao wajuwa wameachana na vibody suti vya kiulaya ulaya wanapendeza kwa kweli na ilaeta maana kuwa na shughuli ya akina mama maana vile visuti wakati mwengine vinawatowa kwenye line big up mama zetu mkiwa hivi tunawaunga mkono kwa saana tu
ReplyDeleteNadhani Jina sahihi la Mshereheshaji ni Baby Kabaya aliyekuwa mtangazaji wa East Africa Radio na sio Baby Madaha yule mwanamuziki wa Bongo Star Search.
ReplyDeletewa kiume inabidi waendelee kuwa wajinga.?
ReplyDeletemdau wa kwanza sio unavyodhani, sisi wabongo tunataka wakina-mama wapate uhuru wao kama vile mola alivyodhamiria. nikitazama hafla hii naona tuko mbele sana kulinganisha na nchi kama vile s/arabia,somalia,afghanistan,pakistan nk anyway we dont worry about them/sisi tunasonga-mbele tunaanza kubishana kuhusu mambo muhimu kama vile katiba mpya,uchaguzi halali nk Tanzania-Tanzania nakupenda kwa moyo wote!!!! msomali wa dom
ReplyDelete