Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo (kulia) akitoa ufafanuzi jana jijini Dar es salaam kwa waandishi wa habari jinsi Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani(IMF) lilivyofurahishwa na juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuboresha uchumi nchini na jinsi ilivyokabilina na changamoto za mtikisiko wa uchumi duniani. Kushoto Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa IMF John Wakeman -Linn.

Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Mustafa Mkullo(kushoto) akiwa katika mkutano wa siku tano wa mashauriano kati ya Serikali na wadau juu ya sera za kuondoa umaskini na mchakato wa mapitio ya utekelezaji na matumizi ya umma. Wengine ni Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Gregory Teu (kulia) na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Pereira Ame Silima ( katikati).

Na Tiganya Vincent, Dar es salaam

Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) limesema kuwa Tanzania imefanikiwa kufanya vizuri katika Sekta ya uchumi licha ya kukabiliwa na changamoto za mtikisiko wa uchumi duniani.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es salaam na Mwakilishi Mwandamizi wa Shirika hilo hapa nchini (Senior Resident Representative) John Wakeman-Linn wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Serikali ya Tanzania.

Alisema kuwa Bodi ya IMF imeridhishwa na maendeleo ambayo Tanzania imeyapata ikiwemo matumizi sahihi ya fedha za mikopo na misaada kutoka kwa wahisani mbalimbali ambayo yamewezesha kuboresha miundombinu.

Wakeman-Linn aliongeza kuwa kufuatia mafanikio hayo Bodi ya IMF imeidhinisha mkataba mpya wa miaka mitatu wa kisera(PSI) ili kuiwezesha Serikali ya Tanzania kuiuchumi kuanzia Juni mwaka huu.

Naye Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo alisema kuwa kwa mujibu wa IMF Tanzania imefanya vizuri wakati wa mgogoro wa uchumi ukilinganisha na nchi nyingi zilipo katika kundi lake kwa kudhibiti matumizi ya mikopo na fedha za wahisani katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Tanzania tumeanza kufanya vizuri licha ya matatizo ya mtikisiko wa uchumi duniani tumeweza kudhibiti matumizi ya fedha za wahisani na kuhakikisha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa kwa ajili ya maendeleo ya nchi na wananchi wake” alisema Mkulo.

Alisema kuwa kila mwaka Tanzania inakutana na IMF na kuzungumza juu ya Mkataba wa Kisera unaoangalia mambo ya kiuchumi na kuishauri Serikali jinsi ya kuboresha uchumi nchini ambapo mwaka huu walifanikiwa kukutana mara mbili Aprili na Septemba mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...