Na Ismail Ngayonga,
MAELEZO Mbeya.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda amewataka maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano Serikalini kuwa wabunifu ili kuwashawishi waajiriwa wao kuelewa msingi wa majukumu yao ya kila siku katika maeneo yao ya kazi.
Aliyasema hayo leo (jana) Jijini Mbeya wakati alipokuwa akifunga kikao kazi cha maafisa, Habari, Elimu na Mawasiliano, na kuwasisitizia kuwa ili kutekeleza majukumu hayo ni vyema wawe na mipango endelevu inayoeleweka na kutekelezeka.
Aliongeza kuwa wapo baadhi ya Maafisa ya Habari katika Wizara, taasisi na Idara za Serikali waliofanya jitihada za makusudi katika kutangaza mafanikio ya Serikali kwa wakati tofauti na msukumo zaidi hauna budi kuongezwa ili maafisa wengine waweze kuiga mfano huo.
Akifafanua zaidi alisema kuwa ,Serikali itambua kuwa vitengo vya habari, elimu na mawasiliano vinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa mafungu, hivyo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ikiwa kama mratibu wa vitengo vya habari itajadiliana na Wizara ya fedha ili kuona ni namna gani vitengo hivyo vitavyoweza kusaidiwa.
“Kama huna fungu ni sawa na ombaomba , na Wizara, Taasisi na Idara zisizo na mafungu tutaendelea kuzifuatilia, kuwa na fungu ni suala moja tu, lakini jambo la pili ni kutazama namna ya kuyatumia mafungu hayo katika vitengo vyetu” alisisitiza Kamuhanda.
Aidha Kamuhanda alisema kuwa Wizara yake imejipanga kuandaa mafunzo kwa maafisa habari, Elimu na Mawasiliano haraka iwezekanavyo kuanzia mwakani ili kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi pamoja na kufahamu majukumu yao ya kila siku katika sehemu zao za kazi.
Kwa mujibu wa Kamuhanda alisema kwa kutambua umuhimu wa mafunzo hayo, Ofisi yake itaendelea kufanya kila jitihada na kwa kadri inavyowezekana kwa kutumia wataalamu waliopo katika Wizara hiyo ili kufanikisha mpango huo wenye malengo ya kuwasaidia Maafisa Habari hao kuelewa misingi yao ya kazi.
“Hata mimi pia naahidi kuwa mwalimu wa mafunzo hayo, na nitamwomba Mklurugenzi wa Utumishi na Rasilimali Watu kunipa mwaliko hata kama nitakuwa nimehama Ofisi hii, kwani mafaniko yenu ndiyo faraja yangu” alisema.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Clement Mshana alisema wajumbe wa kikao kazi hicho kwa kauli moja waliadhimia kuwa kuanzia mwezi Januari 2011 kila Afisa habari atakuwa mstari wa mbele katika kutoa habari kwa umma na kuelezea mafanikio yaliyofikiwa na S erikali katika eneo lake la kazi.
Yapi hayo?
ReplyDeleteNdio maana kuna waandishi wa habari wa serikali....na hiyo ndio kazi yao...AKA Michuzi....lakini sio kila mwandishi wa habari anaambiwa nini cha kufanya.... Mkishaanza kuwaambia watu nini cha kuandika tutafika kweli...
ReplyDeleteNot only achievements but also failures too. But to have a two sided assessment.
ReplyDelete