Transfoma mpya inayofungwa katika kituo cha kupooza umeme cha Kipawa baada ya kuondolewa kwa transfoma iliyoungua na kuchangia mgao wa umeme jijini dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bw. David K.Jairo akifanya mahojiano na mwandishi wa habari wa BBC juu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kukabiliana na tatizo la umeme nchini.kushoto kwake ni Msaidizi wa Katibu Mkuu bwana Elias Kayandabila na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasialiano Bw.Aloyce Tesha.
Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini Bw. David K.Jairo akipata maelezo toka kwa Meneja Mwandamizi Udhibiti na Njia kuu za umeme (TANESCO) Eng.Abdullah Fereshi ( kulia kwa KM) juu ya maendeleo ya kazi ya ufungaji wa Transfoma mpya katika kituo cha kupooza umeme cha Kipawa.kushoto kwake ni Msaidizi wa Katibu Mkuu bwana Elias Kayandabila na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasialiano Bw.Aloyce Tesha. Bw. Jairo ameamuru mafundi wa TANESCO wafanye kazi kwa masaa 24 ili hali ya upatikanaji umeme ilejee kama kawaida katika kipindi kifupi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hata mimi ninaweza kusupply mitambo mingi tu inayotengenezwa na General Electric. Nitanunua iliyotumika lakini at least nitahakikisha inafanya kazi. Na commission yangu ni poa tu, asilimia 10. Siyo commission inakuwa kubwa kuliko hata bei ya mitambo yenyewe.

    ReplyDelete
  2. sasa hiyo kazi itachukua muda gani au huyo mtoa habari hakuwa na nafasi ya kuuliza michuzi wacha kutoa habari nusunusu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...