
Kilimanjaro Stars kabla ya gemu

Timu ya taifa ya Burundi

Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars,Mrisho Ngassa akijaribu kumtoka beki wa timu ya Rwanda,Nzeyimana Hussein katika mchezo uliopigwa leo ndani ya dimba la Taifa.Kilimanjaro stars iliweza kuibuka kidedea kwa kukandamiza Burundi mabao 2-0.

Nurdin Bakari (mfungaji wa magoli mawili ya kili stars) akijiandaa kuachia shuti kali ambalo ilikuwa almanusra kupachika bao la tatu.

Mshike mshike katika lango la timu ya Burundi ambapo golikipa wake,Niyonkuru Vladimir aliweza kuizuia hatari hiyo.

Mrisho Ngassa (nyota wa mchezo) akijaribu kutaka kuwatoka kipa na beki wa Burundi.

Salum Machaku wa Kilimanjaro Stas akiwa peke yake katika eneo la tukio na kupiga boooonge la shuti ambalo lilikwenda nje,huku golikipa wa Burundi akilisindikiza kwa macho.

Nyanda wa BurundiNiyonkuru Vladimir akiwapanga wachezaji wake wakati faulo iliyokuwa ikipigwa kuelekea langoni kwake.

Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakifuraki kwa pamoja mara baada ya kupatikana kwa bao la pili lililofungwa na Nurdin Bakari.mabao hayo ndio yaliyoipelekea Kilimanjaro Stars kufuzu kuingia robo fainali ya mashindano Tusker Challenge Cup.

Washabiki wakishalilia pili liilipopachikwa bao la pili la Kilimanjaro Stars dhidi ya Burundi katika Uwanja wa Taifa jioni ya leo.

Nyomii lilikuwa si la kitoto Taifa leo.

waleee wanateremka zao kuondoka baada ya mechi kumalizika.
Habari ndugu mwandishi wa habari hii. Naomba kusema asante kwa hii habari, pia naona ingekuwa vizuri sana kufanya utafiti wa habari kabla hujaiweka kwenye WHOLE WIDE WORLD (WWW) maana kila mtu anae soma habari hii anaelewa ya kuwa leo KILI STARS imeifunga Rwanda, lakini sio sahihi kwa sababu Rwanda na Tnazania hatuko kwenye same group. Nataka hujue kuwa umetupotosha YOU misslead people kwa kutofatilia na kuzingatia unachokiweka kwenye net. KILI STARS 2-0 Burundi
ReplyDeleteHATIMAYE MAMBO YANAANZAKUBADILIKA SI KWAMBA YANATOKA NJE BALI NI UAMUZI.KUNA SWALA AMBALO HUWA NI TATIZO SANA KATIKA SEHEMU KAMA HIZI.MFANO MPIRA NA MAMBO MENGINE.KWANI HATA WAZAWA WANAWEZA KUWA MACOACHER WAZURI TENA KULIKO HATA HAO WANAOTOKA NJE ILA SASA MZAWA AKIOMBA FACILITIES HATOPEWA.KWA SASA HUYO MZUNGU ATAPEWA KILA KITU KWANINI TUSISHINDE??
ReplyDeletebACK HATA WAZAWA WALIO WENGI UBANAFSI UMEZIDI SANA LAKINI NIKAWAIDA YA KIZAZI CHA NYOKA NIKIMAANISHA WAZEE WENYEKUSEMA VIJANA TAIFA LA KESHO.WAKATI NCHI ZAULAYA VIJANA TAIFA LA LEO NA KESHO.
WATANZANIA IMEFIKIA WAKATI WA KUFUNGUA MACHO.
HONGERA KILIMANJARO STARZ.dako
Hapo ndipo tunapoana matatizo ya tamaa za TFF. Hao watu jinsi walivyojaa hivyo kama kiingilio kingekuwa Tsh 500 tu zingepatikana kama Sh milion 30 hivi. Sasa wamefanya bure kwa kuwa waliweka kikubwa mwanzoni watu wakaja hivyo. Ni watu kama hao wangeweza kumudu kulipa 500 kila mtu. Sasa utaona kuanzia jumatatu kama wataenda kulipa hiyo Sh 2,000 ambayo itakuwa kiingilio. Unajua watanzania hapo wameshaonjeshwa dezo na wameshazoea itakuwa ngumu sana kuja hapo tena na kulipa Sh 2,000 iliyowekwa. Watakuja na kujaa nje kuliko ndani wakitarajia kuruhusiwa tena bure. TFF ilifanya tamaa mbaya sana kuweka kiingilio kikubwa wakati wanajua makabwela ndio wanaopenda mpira. Mtaona jumatatu kama kutakuwa na watu uwanjani, maisha magumu sana watu kutoa 2,000 zao, ilitakiwa kiingilio kiwe 500 tu ilitosha kwanza kombe tayari lina wadhamini wa nguvu wanaolipia gharama zote sasa tamaa ya kuweka kiingilio kikubwa sjui inatoka wapi?.
ReplyDeleteni hatua kali, natumaini tutarudia hamasa za miaka ya sabini/themanini ambapo tulikuwa tunawapa taabu timu za nigeria,ghana,misri,zambia nk natoa shukrani zangu kwa wachezaji wa enzi hizo kama vile omari zimbwe, hassan gobos, manaras family, mweri simba, athmani kilambo, peter tino, mohd salim, salim amri, gibson sembuli, kasim manga,jella mtagwa, leodgar tenga,juma mkambi(rip) omar hussein,athman mambosasa(rip)juma shaban, daudi salum, mohd msomali, mwanashule mwezangu lilla shomari,kaka mtemi ramadhani nk
ReplyDeletemagoli yalikuwa mazuri sana coach lazima awe anamchezesha nurdin bakari number 10 he is good with a header to say the least
ReplyDeletemtoa maoni wa kwanza WWW sio whole wide world,NI WORLD WIDE WEB, angalia kwanza kabla hujamkosoa mwenzako
ReplyDeleteHatari , Hatari , Hatari Kubwa!
ReplyDeleteWatu kufurika namna hiyo na watu kibao kushindwa kuingia, yale yale ya kukanyagana, wekeni angalau kiingilio cha chini kama mdau wa mwanzo alivyosema.
Hongera Tanganyika Stars kwa ushindi mnono dhini ya Burundi.
Halafu kuingia bure kunasababisha uharibifu wa uwanja kwa sababu inapunguza kujihisi wapo responsible na ulinzi wa mali hapo uwanjani.Pia kuingia bure kunaleta hata watu wenye nia mbaya hasa vibaka ambao wanakuja tuu kutafuta wa kuwaibia. Mtaona mashindano yakiisha uharibifu wa mali uliofanywa.Ni vizuri kukwa na kiingilio kidogo hata 200 tu.
ReplyDelete