Kiongozi wa Jumuia ya Wanafunzi wakitanzania nchini ALGERIA (ATSA), Mh. Habibu H.RUHOMBO (kulia) akimsikiliza kwa makini Gavana wa jimbo la Constantine (430KM toka Algiers) Mh. Kimati wakijadili mafanikio na matatizo ya uongozi wa awamu ya nne wa Mh. Jakaya Kikwete kwa watanzania wasomao nje ya nchi pia kumpongeza Mh. MEMBE kwa ushirikiano wake kwa wanafunzi wasomao nje ya nchi.

Jumuiya ya wanafunzi wakitanzania wanaosoma nchini Algeria (ATSA) wanatoa salaam za pongezi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete kwa ushindi mkubwa alioupata katika matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, hiyo inaonyesha jinsi gani watanzania walivyo na imani nae kubwa kutokana na ufanisi na mafanikio ya kiutendaji ya ilani ya CCM ya 2005.

Tunatarajia mafanikio makubwa zaidi hususan katika Nyanja ya elimu kwa kipindi cha pili cha uongozi wake.

Pia uongozi wa ATSA unampongeza Mh. Jakaya Kikwete kwa uteuzi wake wa baraza la mawaziri kwakujali vigezo vyao kwa mfano kumpa wizara ya elimu na ufundi Dr. Kawambwa pia kumrudisha Mh. Membe katika wizara ya mambo ya nje ni ishara tosha kuwa nimchapakazi hodari na anayajua majukumu yake katika wizara hiyo na si vibaya akawa mrithi wake 2015.
Mawsiano.

Rais wa jumuia ya wanafunzi (ATSA):
HABIBU H.RUHOMBO
(+213551713920)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Habari haijatulia. Inabidi kusoma mara mbili mbili kuelewa.

    ReplyDelete
  2. hamna jipya, baraza la mawaziri limeshatajwa.

    ReplyDelete
  3. Nakuunga mkono (hata mguu pia) mchangiaji wa kwanza. Halijakaa sawa hilo tamko. Huu unaitwa 'ukombi'!

    ReplyDelete
  4. Naunga mkono pongezi zaidi kwa Mh.JK
    kwa uteuzi wake!

    ReplyDelete
  5. imekaa njema!liazungumziwa baraza baada ya kutajwa je mkombi ulitaka lizungumziwe baraza kabla ya kutangazwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...