Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Bw. David Mgwassa (katikati) akihutubia wakati wa hafla ya wafanyakazi kusherehekea uzalishaji na kuvuka malengo ya mauzo ya vinywaji vinavyozalishwa na kiwanda hicho, Dar es Salaam wikiendi ilopita. Kushoto ni Meneja Mauzo na Usambazaji wa TDL, Joseph Chibehe na kutoka kulia ni Kaimu Meneja wa Ufundi, Aranyael Ayo pamoja na Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala, Mustafa Nassoro.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Mustafa Nassoro, akielezea siri ya mafanikio ya kiwanda hicho,wakati wa hafla ya wafanyakazi kusherehekea uzalishaji na kuvuka malengo ya mauzo ya vinywaji vinavyozalishwa na kiwanda hicho. Kutoka kulia ni Meneja Mkuu wa TDL, David Mgwassa na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kiwanda hicho, Joseph Chibehe.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Konyagi ya Tanzania Distilleries Limite (TDL), wakifungua kinywaji aina ya Chamdol ikiwa ni ishara ya kufurahia mafanikio ya kuvuka lengo la mauzo ya bidhaa za kiwanda hicho. Kutoka kushoto ni Halima Nassor, Majid Shomari na Elizabeth Mhamiji.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Konyagi ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), wakigongeana chupa na glasi zenye vinywaji na viongozi wa kiwanda hicho kufurahia mafanikio ya kuvuka lengo la mauzo ya bidhaa za kiwanda hicho wikiendi ilopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Konyagi ni kiwanda kizuri sana sema Ujamaa ndio umekirudisha nyuma. Hata Dododma Wine pia.

    ReplyDelete
  2. Funny.
    hakuna hata konyagi moja kwenye meza!

    ReplyDelete
  3. Mdogo wangu David hongera sana kwa bidii yako ya kazi na pole sana kwa msiba wa Mzee.

    Godfrey
    ex Mzumbe

    ReplyDelete
  4. "mauzo mazuri kupita malengo" sasa kwa nini hampunguzi bei na walalahoi waache kunywa gongo? ngoja tu gongo iruhusiwe kama kule kenya ndio mtapunguza bei!!!!!

    ReplyDelete
  5. heheehee kweli its interesting konyagi hazionekani kwene sherehe yao wenyewe mmh!!
    wapandishe bei sasa pato la taifa liongezeke

    ReplyDelete
  6. hongera konyagi

    ReplyDelete
  7. Watu wa Uswahilini huwa tunajua kuwa wauza gongo huwa hawanywi gongo hata siku moja.

    Konyagi asili yake ni gongo, naona wanaendeleza huo utamaduni.

    ReplyDelete
  8. Wadau angalieni vizuri. Chupa mbili za Konyagi zinaonekana vuzuri tu katika picha ya juu kabisa. Bofya kwenye picha ili kuikuza na utaona vizuri. Ningeshangaa sana kama Konyagi, ambayo ndio bidhaa maarufu zaidi (flagship), ya kampuni hii ingekosekana katika hafla hiyo.

    ReplyDelete
  9. Mbona mimi Nyagi naziona hapo nyingi tu kwenye picha,wadau vipi..hamna macho nini?

    ReplyDelete
  10. HUREEEE KONYAGI TUJIVUNIE BIDHAA ZA KITANZANIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...