Mh. Didas Masabuli akila kiapo cha utii cha Udiwani wa Halmashauri kuu ya jiji la Dar es Salaam uliofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar leo.
Mh. Jerry Slaa akila kiapo.
Mh. Abuu Jumaa akila kiapo.
Mh. Abbas Tarimba akila kiapo.
Mh. John Mnyika akila kiapo cha utii cha Udiwani wa Halmashauri kuu ya Jiji leo katika ukumbi wa Karimjee.
Mh. Sofia Simba akila kiapo leo.
Jopo la Mahakimu Wafawidhi chini ya Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Jiji Mh. Mutaki (kati) likifuatilia kwa makini viapo vya Madiwani wa Halmashauri kuu ya Jiji la Dar es Salaam.shughuli hiyo ya kuapishwa kama Madiwani hao imefanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Eh mbona Mnyika na Simba wana uroho wa madaraka namna hiyo?

    ReplyDelete
  2. Tembeleeni shul na hospitali ktk diwani zenu muangalie macho ya watoto na magonjwa wanaokaakulala chini. Aibu tpu
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  3. We Anon wa Fri Dec 02:45:00 acha ushamba uliza kama hujui.. Mnyika na Simba na wabunge wengine wa Dar ni wajumbe au madiwani wanaoingia automatically ktk baraza la madiwani kwa vyeo vyao vya ubunge na ndio maana wanakula kiapo sio kama wamegombea nafasi hizo.

    ReplyDelete
  4. oooh asante anon was 12:28 kwa kunielewesha maana na mimi nilikuwa nataka kuchemsha hapa niulize kulikoni Mnyika na Simba madiwani? kumbe ndo hivyooooooo !!

    ReplyDelete
  5. Hivyo viapo mnavyoapa viwe na utendaji na ukweli ndani yake na siyo ubabaishaji,tatueni matatizo sugu yanayo wakabili watazania na siyo kusherehekea ushinndi tu,kama sasa tunaona mambo yanayochefua zaidi ya mgao wa umeme nk.ingieni madarakani mlete mabadiliko siyo miaka nenda rudi matatizo ni yale yale.
    mtoa maoni.
    Pugu,Dar.

    ReplyDelete
  6. Kitu nachoshindwa kuelewa ni structure ya serikali katika jiji la DAR ES SALAAM. Mkoa wa DAR ni mdogo kuliko yote Tanzania lakini una viongozi wengi kuliko wote na hakuna jipya linalofanyika.
    1-kuna mkuu wa mkoa
    2-kuna meya
    Swali nani ni mkubwa kati ya meya na mkuu wa mkoa?Who's reporting to who?

    3-tuna wakuu wa wilaya
    4-tuna madiwani
    swali nani ni mkubwa kati yao? Who's reporting to who?

    5-kuna mkuu wa polisi wa mkoa.
    6-kuna wakuu wa polisi wa wilaya(najua wamebadili majina)
    hapa hakuna ubishi wakuu wa polisi wa wilaya wako chini ya mkuu wa mkoa.
    **Swali kubwa**
    kwa nini tuna viongozi hawa wote hawa kwa nchi maskini kama yetu?

    Nchi za wenzetu tunaona mji una mayor ambaye anasaidiwa na ma-council members chini yao kuna polisi.Hata hao waingereza waliotuletea hizi serikali nadhani wanaendesha mambo yao hivyo.Itakuwaje sisi tuwe namna hii?

    ReplyDelete
  7. mbigiri.... siyo wewe tu ambaye huelewi haya mambo mkuu wa mkoa na meya hakuna mtu ambaye yuko juu ya mwenzake. Mkuu wa mkoa ni mwakilishi wa rais mkoani na meya ni kiongozi wa serikali za mitaa. Hawa watu wawili wanafanya kazi tofauti kabisa ambazo haziingiliani.
    RPC anaripoti kwa RC na IGP. Wakuu wa polisi wa wilaya wanaripoti kwa DC, na RPC. Hapo utaona viongozi wa serikali za mitaa kama Meya hawaripoti kwa mtu yoyote wa serikali za mitaa ukiondoa waziri anayehusika na serikari za mitaa na Waziri Mkuu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...