Nahodha wa timu ya mpira wa pete ya Mkoa wa Morogoro akilinyanyua juu kombe la ubingwa wa UMITASHUMTA. Moro waliifunga timu ya Mkoa wa Mbeya kwa magoli 24 kwa 16 katika mechi ya fainali.
Washindi wa pili. Nahodha wa timu ya soka ya Mkoa wa Morogoro, Hosten Francis akipokea zawadi ya kombe kutoka kwa Mgeni rasmi naibu Waziri wa Elimu Mheshimiwa Philip Mulugo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Elimu Mheshimiwa Philip Mulugo katikati, shoto ni Naibu Katibu Mkuu OWM TAMISEMI anayeshughulikia Elimu bwana Jumanne Abdallah Sagini na kulia ni Naibu Waziri wa Nchi OWM TAMISEMI anayeshughulikia elimu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Serikali kupitia OWM-TAMISEMI ilifanya uamuzi wa kuyarejesha mashindano haya baada ya kutofanyika kwa miaka 10 mfululizo.
Wanamichezo kutoka Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na vikombe vyao mwishoni mwa mashindano ya UMITASHUMTA ambayo yalimalizika kwa mafanikio katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha.
Nahodha wa timu ya soka kutoka Mkoa wa Mbeya Yona Mtulo akilibusu kombe la ubingwa wa UMITASHUMTA mara baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi Naibu waziri wa Elimu Philip Mulugo. Katika Mchezo wa fainali, Mbeya waliifunga Morogoro kwa magoli 4 kwa 1.
>
Mchezaji mpira wa pete wa mkoa wa Dar es salaam Mariam Yusuf ambaye aliibuka kuwa mchezaji bora kwa upande wa mpira wa pete akisalimiana na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu Mheshimiwa Philip Mulugo kabla ya kumkabidhi zawadi yake.
Wachezaji wa Mpira wa miguu kwa upande wa watoto wenye mahitaji maalum kutoka Mkoa wa Dar es salaam nao waliibuka washindi katika michuano hiyo wakifurahia zawadi yao ya kikombe walichokabidhiwa na mgeni rasmi.
Mchezaji bora wa michuano ya UMITASHUMTA kwa upande wa mpira wa Miguu Hosten Francis kutoka Mkoa wa Morogoro akipozi na zawadi yake mbele ya Mgeni rasmi Mheshimiwa Philip Mulugo. Kijana huyu alikuwa kivutio cha kipekee kwenye mashindano ya mwaka huu ya UMITASHUMTA kwa kusakata kandanda safi ambayo iliwaacha midomo wazi mashabiki wengi
walioshuhudia michuano hiyo
Wanamichezo kutoka Mkoa wa Mbeya wakishangilia kwa nguvu ushindi wa timu yao, wakati wakijiandaa kupokea zawadi ya kikombe kutoka kwa mgeni rasmi. (PICHA ZOTE NA OWM-TAMISEMI)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Inatukumbusha mabli sana hii michezo ,mkuu, shukurani kwa taarifa hii

    ReplyDelete
  2. Hongera sana TAMISEMI, kwa kufanikisha mashindano haya muhimu. Nimeambiwa vijana walikuwa wanakula vizuri tofauti na miaka ya nyuma, walisafiri kwa mabasi na sio malori kama ilivyokuwa zamani, walilala vizuri na pia kupewa vifaa vya michezo. Ni mwanzo mzuri sana, na hapa ndio nilitegemea kuwaona makocha wa Taifa wakivinjari na sio wanasiasa. Safi sana TAMISEMI.( Niliwahi kuwa mwl wa timu za mpira wa wavu za mkoa wa Dodoma na kushinda ubingwa kwa miaka 7 mfululizo)

    ReplyDelete
  3. ....duh, naibu waziri wa elimu nimrefuuuuu!

    ReplyDelete
  4. natoa pongezi kwa serikali kufufua hii michezo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...