Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(kushoto) akizundua awamu ya pili ya Mpango wa Taifa wa Kukuza uchumi na Kupunguza umaskini(MKUKUTA II) na ripoti ya mwaka ya utekelezaji wa MKUKUTA I 2009/10. Uzinduzi huo ulifanyika jana jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa siku tano wa mashauriano kati ya Serikali na wadau juu ya sera za kuondoa umaskini na mchakato wa mapitio ya utekelezaji na matumizi ya umma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na uchumi Ramadhan Khijja picha na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. MKUKUTA 1 imepata mafanikio gani ya kiuhalisia?

    Na jee indicators zilizotumika kwenye kupima hayo mafanikio ni zipi, na ziko realistic??????

    ReplyDelete
  2. Ikiwa MKUKUTA unalenga walalahoi, na wengi wao hawaelewi Kiingereza, kwa nini tunazidi - kila kukicha - kutumia hii lugha (Kiingereza), kama lilvyo hilo bango hapo pichani?

    Sijui, ni lugha ipi iliyotumia hapo mkutanoni wakati wa kuzindua huo MKUKUTA AWAMU II? Je, haingeweza kuwa safi endapo hilo bango lingeandikwa pia kwa Kiswahili?

    Imeandikwa, "...mashauriano Serikali na wadau..." Wadau hao ni akina nani: wakulima ama wafadhili wa nje au wote pamoja?

    ReplyDelete
  3. hata huo mkukuta wa kwanza hatuuelewi ije kuwa wa pili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...