NDUGU PETER MAKUMBI AISHIYE QUEENS, NEW YORK (USA) ANAWATAFUTA NDUGU ZAKE WALIOKO NCHINI TANZANIA NA AMBAO HAJAWASILIANA NAO KWA MIAKA NANE AU ZAIDI.
(1) SUSANA MAKUMBI
(2) BENJAMIN MAKUMBI
(3) LUCY MAKUMBI
(4) MUZE
KWA YEYOTE KATI YA WATAJWA HAPO JUU ATAKAYELIONA TANGAZAO HILI AU MTANZANIA YEYOTE ANAYEMFAHAMU BW. PETER MAKUMBI BASI TAFADHALI AWASILIANE NAYE KWA NAMBA HII YA SIMU
917 520 9154

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Naona unauza nyago Makumbi, sawa bwana lakini nakushauri acha kuuza sura kiwanja, wewe chana box kama huna akili nzuri na bills za nchi hii hadi uchange hela ya kisawasawa si leo wala kesho.

    Any way nakushauri ujitahidi babu upate japo ka- italy Trans kamoja kakasumbue Dar. Benja nilimwona Bongo mwaka 2007 nadhani alikuwa kawaida tu, tulikutana nae pale Bamboo Bar kinondoni anakunywa soda lakini nikamkaushia maana niliogopa kupigwa mizinga.

    ReplyDelete
  2. kaka hauna e mail kumbuka kupiga cm ni gharama sana siyo kwa kuwa wewe unachana box hali yako ni nzuri kidogo kumbuka bongo

    ReplyDelete
  3. ah ,mdau alietangulia ametaja italy-trans sasa nimepata jibu konda alikua beach boy jamaa mfupi sana halafu bonge sijui sasa yuko wapi kipindi hicho niko form 1 student ukipanda costa yao yani wewe ni mjanja kinoma,anyway kaka yako Juli anaofisi ya bima ubungo jengo la nssf yuko na kakake benja.benja nilimuona kipindi kidogo kama miaka 2 iliyopita kndoni lkn bro amechoka,Kaka jipange kama huna ishu huko rudi mapema kablamambo hayajaharibika na kupoteza washkaji bongo
    mdau

    UFIPA STREET K'NDONI

    ReplyDelete
  4. kaka enzi zenu mlitesa.wote sijawaona lakini jipange uje bongo ni kama marekani siku hizi.aliyekosa kakosa japo anatafuta lakin kupata kupo kazi ileile

    ReplyDelete
  5. sasa wewe Anonymous hapo juu jamaa anaulizia ndugu zake wewe unaanza historia na maneno kama muuza njegere wa kitaaa aje bana, kama unainfo mchane tuu ila si maneno mengi ambayo hayana msingi ndio maana akawaweka simu kama unataka kumsimanga, JIHESHIMU

    ReplyDelete
  6. ati bongo ni kama new york weweee, huku umeme haujawahi kukatika masaa 24! watu wanalala gizani bila umeme na joto kali lililopo sasa hivi ni aibu kubwa, sio ubwabwaje tu hata siku moja bongo haitakaa iwe new york neverrrrrrrrrrrr!!!

    ReplyDelete
  7. matangazo mengine yanashangaza sana, yaani mtu hakuwa na mawasiliano na ndugu zake kwa miaka minane? why? nashindwa kuamini kabisa, utapotezaje contact za ndugu zako miaka yote hiyo?

    ReplyDelete
  8. Huko nyuma kulikuwa na tabia kwa watanzania wengi waliopo nje ya nchi wanapokuja nyumbani huwa wanadanganya wenzao kuwa maisha ya nje ni poa, kazi nje nje na malipo ni poa bila ya kuweka ukweli wote kuwa maisha yalivyo, wapi wanaishi na kadhalika. sasa naona waliopo bongo wanataka kuleta mchezo huo huo, mtu anataka kutudanganya hapa eti maisha ya bongo ni sawa na NY!! ahhh bora nibaki kimya!!

    ReplyDelete
  9. Mdau wa "simu gharama" - sio lazima umpigie simu unaweza hata kutuma sms/text ali mradi mwisho wa siku uwe umemsaidia kama alivyoomba hapo juu... kama hujui ni hujui, hiyo misengenyo haitomsaidia kuwapata nduguze. na kupoteza mawasiliano huwa inatokea, sio kitu cha ajabu sana.. (msaidieni kama mnaweza.)

    ReplyDelete
  10. Binaadamu hebu wacheni mambo hayo. Inawezekana watu kupoteza mawasiliano sio cha ajabu. Inawezekana POBox imebadilika, namba za simu zikabadilika hilo sio geni. Kama mtu unaweza au unawajua hao aliowataja na kuna ugumu gani kumsaidia? Hebu tuache mambo ya roho mbaya yanaweza kumkuta yeyote. Peter mimi hao wote uliowataja nawafahamu lakini sina contact zao. na wewe mwenyewe pia nakufahamu in fact nilivyoenda TZ jamaa zako walikuwa wanakuulizia kama nimekuona huku niliko. kwani na mimi mtoto wa Kinondoni pia. Nitajitahidi kuongea na jamaa nyumbani waende pale kwenu kuwapa hiyo contact yako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...