Marehemu Saidi Baamary

BI SAMIRA SAIDI BAAMARY, BINTI WA MAREHEMU SAIDI BAAMARY ALIYEFARIKI KWA AJALI DAR ES SALAAM MWISHONI MWA WIKI ILIYOPITA BAADA YA KUHUDHURIA HAFLA YA KUWAKUMBUKA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI ILIYOFANYIKA LEADERS CLUB, KWA NIABA YA FAMILIA YA MAREHEMU ANATOA SHUKRANI NYINGI KWA WOTE WALIOSAIDIA KWA HALI NA MALI KUHITMISHA MAZISHI YA MPENFDWA BABA YAKE. HANA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUMWOMBA MOLA AWAZIDISHIE IMANI NA UPENDO NA KUWAAFU KATIKA YOTE MNAYOFANYA.

BI SAMIRA ANAKARIBISHA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KWENYE HITMA YA KUMREHEMU BABA YAKE ITAYOFANYIKA NYUMBANI KWAKE LEO SAA 12 JIONI HUKU EDMONTON, UINGEREZA. KWA MAWASILIANO NA MAELEZO UNAWEZA KUPIGA SIMU NAMBA +447405859533 KWA MAMA YAKE, DIANA LUMELEZI.

MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI
-AMIN


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. halafu marehemu hakuwa mzee kabisa, poleni wafiwa.

    RIP brother nasi twaja

    ReplyDelete
  2. Poleni sana wafiwa. Nilipita dakika chache baada ya marehemu kugongwa pale French Embassy area, nilisikitika sana na iliniumiza roho usiku mzima pamoja na kutomfahamu. Mwenyezi mungu SAW ailaze roho yake pema peponi.

    ReplyDelete
  3. Kifo cha Said "Winchester" kimenirudishia kumbukumbu nyingi za club yetu ya mpira Congo United katika miaka ya 1970. Sote umri wetu wastani ulikuwa miaka 20 hivi. Said akicheza nyuma kama full back. Wakati wote yeye akitabasamu muwe mnashambuliwa au mnashambulia. Miaka mingi imepita tumepoteana.

    Allah amsawazishie njia yake. Amin.

    Mohamed Said

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...