BI SAMIRA SAIDI BAAMARY, BINTI WA MAREHEMU SAIDI BAAMARY ALIYEFARIKI KWA AJALI DAR ES SALAAM MWISHONI MWA WIKI ILIYOPITA BAADA YA KUHUDHURIA HAFLA YA KUWAKUMBUKA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI ILIYOFANYIKA LEADERS CLUB, KWA NIABA YA FAMILIA YA MAREHEMU ANATOA SHUKRANI NYINGI KWA WOTE WALIOSAIDIA KWA HALI NA MALI KUHITMISHA MAZISHI YA MPENFDWA BABA YAKE. HANA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUMWOMBA MOLA AWAZIDISHIE IMANI NA UPENDO NA KUWAAFU KATIKA YOTE MNAYOFANYA.
BI SAMIRA ANAKARIBISHA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KWENYE HITMA YA KUMREHEMU BABA YAKE ITAYOFANYIKA NYUMBANI KWAKE LEO SAA 12 JIONI HUKU EDMONTON, UINGEREZA. KWA MAWASILIANO NA MAELEZO UNAWEZA KUPIGA SIMU NAMBA +447405859533 KWA MAMA YAKE, DIANA LUMELEZI.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI
-AMIN


halafu marehemu hakuwa mzee kabisa, poleni wafiwa.
ReplyDeleteRIP brother nasi twaja
Poleni sana wafiwa. Nilipita dakika chache baada ya marehemu kugongwa pale French Embassy area, nilisikitika sana na iliniumiza roho usiku mzima pamoja na kutomfahamu. Mwenyezi mungu SAW ailaze roho yake pema peponi.
ReplyDeleteKifo cha Said "Winchester" kimenirudishia kumbukumbu nyingi za club yetu ya mpira Congo United katika miaka ya 1970. Sote umri wetu wastani ulikuwa miaka 20 hivi. Said akicheza nyuma kama full back. Wakati wote yeye akitabasamu muwe mnashambuliwa au mnashambulia. Miaka mingi imepita tumepoteana.
ReplyDeleteAllah amsawazishie njia yake. Amin.
Mohamed Said