Taarifa kwa vyombo vya Habari

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inafuatilia kwa ukaribu taarifa kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Southwark mjini London, Uingereza kuiamuru Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza kulipa faini ya Paundi za kiingereza laki tano 500,000 kwa kushindwa kuweka kumbukumbu sahihi za kihasibu kuhusu fedha zilizolipwa na kampuni ya BAE Systems kwa Mfanyabiashara Shailesh Vithlani wa Tanzania miaka mitano iliyopita.

Serikali ya Tanzania,kupitia Ubalozi wetu nchini Uingereza imeomba taarifa rasmi kutoka Serikali ya Uingereza kuhusu uamuzi huo. Serikali inasubiri kwa hamu kubwa kurejeshwa kwa bakaa ya Dola Milioni 30 za Kimarekani kama ilivyokuwa katika makubaliano kati ya Idara ya Serious Fraud (SFO) na Kampuni ya BAE Systems baada ya kuondoa faini ya kiasi cha Paundi Laki tano za Kiingereza ambazo kampuni ya BAE Systems imeamuriwa kuilipa Mahakama ya Southwark mjini London.

Mara baada ya kupata taarifa rasmi, Serikali ta Tanzania itachukua hatua muafaka ikiwa ni pamoja ni pamoja na urejeshwaji wa kiasi cha fedha kinachotakiwa kurejeshwa Tanzania kulingana na makubaliano kati ya SFO na Kampuni ya BAE Systems.

Imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

22 Desemba, 2010

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Napendekeza watumie hiyo hela kuboresha haospitali za serikali kwa kununua mitambo kama X-ray na Dialysis etc.

    ReplyDelete
  2. Sheikh Yahya Wangu wee, Mwee!?!

    ReplyDelete
  3. Hii wizara inatufanya sisi limbukeni kweli. Inasikitisha kwamba serikali ya TZ haikutuma hata mwakilishi mahakamani. Pili issue hapa sio kurudiwha hela. Ni lini serikali ya TZ itakuwa na UTHUBUTU wa kuwawajibisha mafisadi? Hawa wahuni waliosuka dili ya rada wanaeleweka ni akina nani. Lakin tunaambiwa kwamba serikali ya TZ imekataa kutoa ushirikiano kwa serious fraud ofisi ili hawa mafisadi washughulikiwe. Wamwgawana bila shaka!

    ReplyDelete
  4. Tunashukuru kwa kutoa taarifa ya suala hili, je watu waliotajwa kuhusika katika kashfa hii nao watachukuliwa hatua?na je hela zao zilizotajwa kuwa nje zitarudishwa nchini Tanzania, haya ndiyo mambo ya kutueleza au Takururu ndiyo wanaanza kesho kusafisha watu sasa.

    ReplyDelete
  5. "Serikali inasubiri kwa hamu kubwa kurejeshewa bakaa ya usd 30 million" Mbona haisemi itashukua hatua gani kwa waliohusika kwa upande wa TZ? Inasubiri mpaka serikali ya UK imalize kesi ndio nayo inakurupuka...hii ndio shida ya kuongozwa na Rais corrupt.

    ReplyDelete
  6. na zikirudishwa hizo zitayeyuka kimaajabu ajabu kama kawaida ya viongozi weyu wa tanzania.

    ReplyDelete
  7. Mbona taarifa imeshindwa kusema wahusika wote watachukuliwa hatua?

    Chonde Chonde hizo hela za watanzania jamani tunaomba zipelekwe kwenye uduma za jamii sio zinaangukia kwenye mikono ya waovu.

    ReplyDelete
  8. Na hizi pesa zikishafika tuambiwe ziko wapi nani anazo na zinatarajiwa kufanyiwa nini? Na mtuonyeshe mahesabu yote jinsi zinavyotumika.

    ReplyDelete
  9. mdau wa Wed Dec 22, 10:40:00 PM mbona unafanya masihara namna hii? Hii Tanzania bwana hatufanyi hayo, pesa zikipatikana alomjanja zaidi ndio zake, hakuna masuali wala data kuwekwa wazi.

    ReplyDelete
  10. Hii taarifa inajaribu kuleta 'minimization -effect', maana haisemi mfanyabiashara wa kitanzania alikatiwa kiasi gani, ambacho 'hakikuingiza ktk vitabu vya mahesabu ya BAE System ikalazimu mahakama ukipa BAE System faini ya paundi 500,000!

    Na je mshiko aliopatiwa mfanyabishara wa kitanzania hautafuatiliwa na serikali ya Tanzania ipate angalau wa asilimia 80.

    ReplyDelete
  11. hizo hela jamani sio za wananchi hio hela ni ya mkopo toka barclays bank ndio maana worl bank waka mind kwa nini mnunue rada kwa mkopo kitu ambacho sio necesary kwa sasa kwa nchi masikini kama tz ambayo kipaumbele kingekua ni huduma za jamii sio rada ambayo haitakua na umuhimu kwa sababu hatuna jeshi la anga so hizo hela wazirudishe wasitutie kwenye madeni ambayo hayatuhusu plse nyie viongozi vichwa vibovu

    ReplyDelete
  12. Mmmh, zije tu lakini najua mafisadi wetu watakuwa tayari wameanza kuzitumbulia mimacho.
    Subirini mtaona na kusikia

    ReplyDelete
  13. Naomba mtambue kuwa serikali ina kitu kinaitwa supplementary budget ambapo kuna matumizi ambayo hayakuwa kwenye budget ya 2010/11 ambayo serikali inataka kuyatekeleza ikiwa ni pamoja ana ahadi lukuki za mheshimiwa wakati wa kampeni, hata kama ni mkopo waliochukua kipindi hicho naamini wako tayari deni liendelee kuwepo lakini hiyo hela waitumie kwenye mambo yao ikiwa ni pamoja na kuliwa na wachache. Mimi kama mwananchi ninayeyaona haya yakitendeka, ningeshauri tena hapa waandishi wa habari mtusaidie sana..serikali ya uingereza waturudishie hela kwenye mfumo wa miradi, mfano..watutengenezee barabara zetu za ring roads hasa kwa jiji la dsm, hata kama si hiari yetu, lakini mateso ya wananchi wa dar sote tunayajua, leo hii hata mwanao akiugua ghafla, ukiwa mbali na alipo huwezi kuwahi kumpeleka kwenye huduma za afya, kutoka ubungo tu hadi mbezi mwisho ni masaa 3, hizi huduma za afya nazo ni muhimu sana ila kwa kuwa kuna hospitali wana mashine hizo tunaweza tukalipa kipaumbele cha pili.

    Mdau

    ReplyDelete
  14. Mimi napenda tuanze na huyu mfanyabiashara Vithlani ni nani na anauhusiano nakina nani. Tukimchimba huyu tutapata majibu mengi ya wahusika wakuu wa rada na kwanini hawashtakiwi. Ni vizuri tukaponya kabisa vidonda kuliko kilasiku kuweka bandages zisizokwisha. Tunahitaji kusafisha huu uuozo jamani Watanzania.

    ReplyDelete
  15. Ati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inasubiri kwa hamu...Lol hata ningekuwa mimi ningezisubiri kwa hamu...!! Yaani kweli wanataka kutufanya kuwa sisi hatupendi pesa? Mr. Membe tukumbukane basi...!!

    ReplyDelete
  16. Ina maana tunatakiwa tuchekelee bakaa hiyo au? Walioiingiza nchi kwenye mkenge huu wanaendelea kupeta na mashangingi huku wengine tunahangaika. Shughulikieni waliotuingiza mkenge kwanza.
    Hata hiyo bakaa sitashangaa ikipotelea visiwa vya Jersey.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...