Viongozi wa TBL pamoja na Makatibu wa klabu za Simba na Yanga katika picha ya pamoja huku wakionyesha baadhi ya vifaa walivyokabidhi kwa klabu hizo.Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na jezi za mechi, jezi za mazoezi, jezi za kupasha moto misuli, mabegi ya mazoezini, mabegi ya mipira, traksuti, filimbi, mipira ya soka, viatu vya soka, viatu vya mazoezi na kadhalika.
Mkurugenzi wa Masoko TBL Bw. David Minja(kulia) akikabidhi jezi kwa Katibu wa Klabu ya Simba Bw. Evodius Mtawala. Jezi hizo zitatumika katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania maarufu kama Vodacom Premier League.
Wachezaji wa Simba na Yanga wakiwa
wamevalia jezi walizokabidhiwa na TBL
Picha na Mo Blog Team

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Leodgar Tenga tembeeni muulize kule mpira ulipoinuka umesababishwa na nini?

    Msitegemee kuona mpira ukipanda kwa kuziwezesha timu mbili tu.

    Tengenezeni muundo utakaohusisha timu nyingi kutoka at least 80% ya nchi yetu.

    Hata wadhamini mna la kujibu, kunavituo vyenu vya biashara Moshi, Arusha,Mwanza hata Mbeya........kwanini imani yenu ya kujitangaza hapo tu?

    Imani kwamba mpira upo Dar tu haina ukweli.

    ReplyDelete
  2. Hivi bukta zinaruhusiwa kuvaliwa 'mlegezo' (chini ya makalio) kama ninavyoona hiyo picha ya chini kabisa kushoto?

    ReplyDelete
  3. TFF, wadhamini kama TBL, TV, Radio,viwanja vya mpira mikoani/wilayani na wadau wengine wote lazima kujua kuwa mpira siyo Darisalama tu.

    Mfano ktk Uingereza(UK)mji wa Manchester(wakazi laki nne ishirini) ni mji wa tisa kwa ukubwa UK(United Kingdom)hivyo tuseme ni Iringa kwa Tanzania,lakini mjini Manchester kuna timu kubwa kama ManUTD, ManCity n.k na wadhamini/wadau wamezisaidia sana timu kujulikana kuwa ni timu kubwa. Hakuna kusahau mji wa Liverpool(wakazi laki nne arobaini) ni wa nane kwa ukubwa Uingereza(UK)huku kukiwa na timu kubwa ya Liverpool FC.

    Kwa Tanzania pia tunatakiwa kuwa na timu nzuri pia toka Kigoma, Moshi, Tanga, Mtwara, Dodoma,Lindi n.k ili kuweza kuibua vipaji toka huko na siyo kufanya Darisalamu ndiyo Tanzania.

    Ikiwa TFF, wadhamini, magazeti, TV, Radio na wadau wengine wakiona umuhimu wa kuwa na timu toka kona zote za Tanzania zitakazozitoa jasho timu za Simba na Yanga, basi mpira wa Tanzania utakuwa mkubwa na pia wadhamini na wadau wote kufaidika kibiashara na kimichezo kwa kujazana viwanjani kuangalia timu zote bila kujali kama ni Simba au Yanga kutokana na ushindani mkubwa utaokuwepo ktk soka.
    Mdau
    Ntwara Mjini

    ReplyDelete
  4. hizo bukta kama sketi eboo......... man u hatushikiki..

    ReplyDelete
  5. mchezaji wa yanga anakifriji...lol
    bia za bure hizo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...