Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko akimkabidhi hati za kusafiria za Wasanii 14 wa kikundi cha ngoma cha Wamasai na Wadatoga waishio maeneo ya hifadhi ya Ngorongoro mratibu wa kikundi hicho Mhe. James Moringe ambaye pia ni Diwani wa kata ya Endulen tarafa ya Ngorongoro.Hati hizo ziligharamiwa na Serikali kupitia iliyokua Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ili kuwawezesha wasanii hao kuhudhuria mwaliko wa Serikali ya Afrika Kusini uliowataka kutumbuiza wakati wa sherehe za ufungaji wa Michuano ya Kombe la Dunia la FIFA zilizofanyika nchini humo tarehe Julai 2010.


Hii si imepita au macho yangu - aliyetakiwa kuleta hizi habari awajibishwe, huu ni uzembe wa hali ya JUU. bongo tunarudishwa nyuma na watumishi WAZEMBE! kapewa task ya kuleta hizi habari kwa michuzi miezi mitano iliyopita ndio analeta leo... ningefukuzilia mbali hii takataka!!!!! yaani na jazba na watumishi wazembe mpaka basi!!! lol
ReplyDelete