Habari,

Ndugu zetu wadau wa kiwanda cha filamu Tanzania, Zanzibar International Film Festival (ZIFF) inapenda kuwataarifu kuwepo kwa ZIFF Min-Festival itakayofanyika Ngome Kongwe, Zanzibar kuanzia tarehe 31/12/2010 hadi 2/01/2011, itakua ni Tamasha dogo la siku 3 katika kutoa muamko kwa Tamasha kubwa la ZIFF lijalo (2-10 Julai, 2011).

Tamasha hili dogo litajumuisha filamu za kitanzania peke yake ili kuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema katika tasnia hii, Tamasha hili litaonesha filamu 6 za Kitanzania na filamu 2 bora kati ya hizo zitaenda kuoneshwa katika Tamasha kubwa la filamu Afrika - FESPACO huko Burkina Faso.

Kama ilivyo ada ya Tamasha la Filamu la Nchi za Majahazi, tutakua pia na makundi ya muziki na wakati huu kundi zima la THT litafanya maonesho kwa siku zote tatu, watakao kuwepo ni Mwasiti, Marlaw, Mataluma, Amin, Barnaba, Pipi, THT Dancers na wengineo. Kwa habari zaidi tembelea www.ziff.or.tz

Tunapenda kuwakaribisha wadau wote na waandishi wa habari katika mkutano wa waandishi wa habari utakaofanyika katika ukumbi wa Habari - Maelezo, Dar es Salaam, kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 5 asubuhi kesho Jumatano, tarehe 22/12/2010

Ahsanteni!

Daniel Nyalusi
Festival Manager
Zanzibar International film Festival

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Congratulations ZIFF.

    Lakini nadhani kazi za kuripua si nzuri kama tunataka kufikia pale tulipoacha miaka minne iliyopita. Zimebaki siku 10 mpaka tarehe 31 tunapoanza tamasha letu dogo. Je, hamkujua hili mpaka muanze matangazo leo?
    HAPANA; TUNAHITAJI KUBADILIKA ILI TWENDE MBELE NA SI KURUDI NYUMA1

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...