Maandamano ya wanaosadikiwa kuwa wanachama na wapenzi wa CHADEMA yakikatisha mitaa ya jiji la Arusha muda mfupi uliopita
Polisi wayapiga stop maandamano hayo
Maandamano yakiwa yamepigwa stop
Maeneo ya unga limited
Arusha hapatoshi dakika hii. Picha na Aravind BK
MWENYEKITI WA CHADEMA NA MBUNGE WA HAI MH. FREEMAN MBOWE NI MIONGONI MWA VIONGOZI KADHAA WA CHAMA HICHO AMBAO WAKO MIKONONI MWA POLISI JIJINI ARUSHA DAKIKA HII, BAADA YA KUTIWA MBARONI KWA KILE KILICHOONEKANA KUWA MAANDAMANO BATILI.
TIMU YA GLOBU YA JAMII AMBAYO IKO ENEO LA TUKIO LIMEWATAJA VIONGOZI WENGINE WALIO KOROKORONI KUWA NI MBUNGE WA ARUSHA MJINI MH. GODBLESS LEMA, MBUNGE WA ROMBO MH. JOSEPH SELASINI NA WANACHAMA WENGINE KADHAA WA CHADEMA.
HABARI ZINASEMA POLISI WALITAWANYA MAANDAMANO HAYO YALIPOKARIBIA OFISI ZA TAKUKURU NA KWAMBA BAADA YA VUTA NIKUVUTE, MH. MBOWE NA WENZIE WAKAKAMATWA NA KUTUPWA RUMANDE.
AIDHA HABARI ZINADATISHA KWAMBA JIJI LA ARUSHA LINARINDIMA KWA MPAMBANO WA KUKIMBIZANA WA POLISI NA MAKUNDI YA WATU WANAODAIWA KUTAKA KWENDA KITUO CHA POLISI KUWATOA WALIOKAMATWA KWA NGUVU.
--------------------------------
Mh. Freeman Mbowe akizungumza na Tanzania Daima kutoka Arusha jana jioni alisema maandamano hayo yatakayohitimishwa na mkutano mkubwa wa hadhara, ajenda yake kuu ni kupinga hatua ya serikali kuvunja sheria kwa makusudi na kukipa Chama cha Mapinduzi (CCM) ushindi ulio kinyume cha sheria katika uchaguzi wa umeya uliofanyika hivi karibuni.
Mbowe akizungumza na Tanzania Daima kutoka jijini Arusha jana jioni alisema CHADEMA itaanza rasmi kuitumia nguvu ya umma kupinga kile alichokiita "uhuni uliofanywa na CCM na serikali yake kujipa ushindi wa lazima katika uchaguzi wa umeya kinyume na matakwa ya sheria halali za nchi.
"Mwanza hakujafanyika uchaguzi kwa sababu ya dhuluma, Kigoma na Arusha uchaguzi ulikuwa batili kabisa. Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) tumemsihi sana aingilie kati lakini ameendelea kushirikiana na chama chake (CCM) kuinyima CHADEMA haki ya kuongoza. Tunakwenda kulaani kwa nguvu zote uchakachuaji wa maamuzi ya wananchi" alisema Mbowe. Kwa chanzo na habari kamili....
BOFYA HAPA
Mbona huu ni mwanzo tu!
ReplyDeleteHuu mtindo wa jeshi la police kupewa mamlaka kinyume na haki za banadamu unabidi upatiwe ufumbuzi, sio kila maandamano yakwamishwe. lini wananchi watapewa uhuru wa kutoa dukuduku zao, kama mikutano na maandamano ayapewi nafasi?
Serikali imengangania madarakani, na aitaki kusikiliza wapinzani! tutatumia kila njia kufikisha ujumbe, serikali aiangalie unyanyasaji huu unaofanywa na police, sio haki kabisa.
Michuzi kama kawaida utabania maoni haya. hata hivo Katiba mpya itapatikana na TANGANYIKA pia!
Police waache unyanyasaji!
Nadhani serikali inapaswa kuelewa kuwa maaandamano ni njia mojawapo ya kudai haki. Kama wanaoandamana wanafanya hivyo kwa njia ya amani kunasababu gani polisi kuanza kuwabughudhi raia?
ReplyDeleteUtabiri wangu, kama hii hali ya ugandamizaji wa vyombo vya dola hautadhibitiwa na serikali basi ipo siku damu itamwagika. Hakika hii siyo dalili nzuri kwa serikali inayojali demokrasia na utawala bora.
Ipo siku wananchi wenyewe watajichukulia madaraka mikononi kama hivi vyombo vya dola ambavyo vimepewa dhamana ya kuwalinda raia ndiyo kwanza wanafanya kuwanyanyasa na kuwaonea raia!
Ila pia lazima wajue Maandamano yanafanywa vipi jamani...
ReplyDeleteMaandamano hayafanywi tu bila taarifa.
Maandamano yana heshima zake na pia jeshi la polisi linatakiwa kuheshimu maandamano kama wanajuwa yapo sio tu wameamuwa kufanya maandamano kinyume cha sheria.
Watu wa Chadema lazima mjue haki zipo vipi jamani. na wananchi mnaoona mnaonewa mna haki kupeleka malalamiko mahakama ya binadamu Arusha, mtu mkoa wowote ule.
CHADEMA JARIBUNI KUWAELIMISHA NA MASHABIKI WENU.
MZ
MICHUZI: Mimi ni muumini mzuri wa mageuzi na democrasia ila kwa hili walilolifanya CHADEMA leo siwaungi mkono kabisaaaaaaaaa.Regards Jimmy DSM
ReplyDeleteHuo ni ujinga,kwanini wasiachwe,kila mtu ana haki ya kusikilizwa.
ReplyDeleteMUNGU AINUSURU HII TANZANIA. Wanachofanya polisi wa Arusha ni kufuru, wanapiga mabomu kama mazoezi. Wnatumia nguvu kubwa sana sana. Hii nchi haina haki. Hivi wamepata wapi hizo hela za kuchezea namna hii? magari utafikiri ni maonyesho au mashindano. Mbona HOSIPITALINI hawaweki DAWA kama wanahela za kuchezea namna hii? TAIFA LITAANGAMIA TUSIPOKUWA MAKINI. MUNGU INUSURU TANZANIA
ReplyDeleteJimmy na MZ hata mie nawaunga mkono maandamano mengine jamani lazima mjue sheria zake namna hii ndio inaleta fujo na kuharibu nchi sasa CHADEMA mnajiharibia sasa sifa zenu baada kupata kichwa sana. Mdau Kigoma.
ReplyDeleteninavyojua mimi kazi ya polisi ni kulinda watu wanaoandamana, polisi wa nchi zilizoendelea huwa hawafanyi hivi,maandamano yoyote yasiyo na fujo huwa si batili...
ReplyDeleteMaandamano sio tatizo, tatizo ni wale wanaoandamana wakidhani fulani wa chama chao akiingia madarakani basi kila kitu kitakuwa mswano...hizo sio fikra sahihi kwani as soon as hao mnaowataka wawe madarakani wakishaingia hamtawaona tena kuwasaidia. Nyie mtamwaga damu zenu for no gud reason. Tatizo nchi yetu kila mtu anataka kula na watoto wake na sio kusaidia wananchi.Nchi za ulaya ni tofauti kwasababu viongozi wasipowajibika basi vyombo vya sheria huwawajibisha maana kila kitu kipo wazi; sisi hatuna vyombo vya kuwajibisha viongozi tuliowachagua. Nyie mnaoandamana fikirieni jinsi ya kujisaidia wenyewe na familia zenu through biashara, kilimo, kazi nyingine nk nk NAWAHAKIKISHIENI hakuna atakaetaka kuingine madarakani eti kuwainua nyie na ndugu zenu. Tusiumizane watanzania kwa ajili ya upuuzi huu.
ReplyDeleteMbona sisi (CCM) tukiandamana hamtupigi mabomu? Mnapendelea eeeh?
ReplyDeleteAcheni ujinga nyiee.. Hivi mtu umeomba kibali cha kutoa malalamiko yako, halafu ukanyimwa ukaambiwa marufuku kufungua mdomo. Ukaamua ukasema basi nitaandamana kuonyesha kwamba nimeonewa, pia ukanyimwa kuandamana. Sasa wewe ukatoe wapi malalamiko yako?
ReplyDeleteAcheni kutetea ujinga. Asume ni wewe umeonewa kazini na bosi wako wa kitengo, halafu ukamlalamikia akakupuuza, ukaamua kwenda kwa bosi wa juu, naye akakupuuza, utajisikiaje? utachukua hatua gani?
TML
CHADEMA HOYEEEEEEEEEEE!
ReplyDeletePEACE & LOVE TO ALL TZns
JAMANI MSHAURINI JK ASOME ALAMA ZA NYAKATI. HUKU TUNAKOELEKEA NI PABAYA SANA. TUTAKUJA KUJUTA WAKATI MAMBO YAMESHAHARIBIKA KWA KIASI KIKUBWA.
HATA CONGO, RWANDA NA BURUNDI WALIANZAGA HIVIHIVI KIDOGO KIDOGO.
MAJUTO NI MJUKUU.
ENYI WAKUBWA WA NCHI, SIMAMIENI HILI SWALA ILI HAKI ITENDEKE. KAMA HAKI INGETENDEKA HAYA YOTE YASINGETOKEA. CCM ACHENI UBABE, WATENDEENI WENZENU HAKI.
MMH (Mdau mpenda haki)
Mbona sijamwona Zito Kabwe au yeye sio CHADEMA tena? Halima Mdee nae alijificha wapi au nayeye alizimia kama mwenzake.
ReplyDeletePolice na CCM mnawapa umaarufu CHADEMA!! kwani kuandamana kuna ubaya gani? acheni hizo, mnamwaga damu ya watu wasio na hatia. Mbona mnatumia nguvu nyingi kiasi hicho? mbona wahalifu mmeshindwa kuwa dhibiti? vibaka kibao, wauza unga, majangiri, majambazi nk. Kuweni wastaarabu basi badala ya kutumia resources za walipa kodi isivyotakiwa. Yaani mnatukera mnoooo
ReplyDeleteFROM ZENJ TO MAINLAND NOW, OVER TO U SISI SASA TUNA MARIDHIANO, MAMBO MSWANO TUUUUU, U HAVE TO LEARN FROM US
ReplyDeleteMPEMBA
Tunatofautiana upeo. Kwa wengine hili ni siasa tu, kwa hiyo hawaoni kuwa kuna haki za binadamu zimevunjwa katka kuwachukulia hatua wafuasi wa chadema. Jamani, tuzijue kanuni na sheria zinazolinda haki zetu. Polisi anatakiwa atumie nguvu kiasi ili kumkamata mtuhumiwa. Sasa askari wa kiume anapompiga marungu mwandamanaji wa kike kichwani anakuwa na lengo la kumkamata au kumuua? Haya mambo yanatendeka mbele ya kamera, je wakiwa katka vtuo vyao inakuwaje kwa watuhumiwa? Hili limejitokeza sehemu nyingi: maandamano ya wanafunzi,maandamano ya wananchi wanapofunga barabara, wazee wa Afrika Mash. n.k. Kesho itakuwa zamu yako ewe unaekebehi wenzio waliojeruhiwa. Unyanyasaji wa polisi hauna itikadi!
ReplyDeleteWadau wenzangu wa blog hii naomba mnisaidie kwa hili, "hivi hii gharama waliyoitumia police si ingetumika hata kuwasaidia watoto yatima waweze kusoma kwa uhuru na furaha? eti wanatumia nguvu kubwa kwa vitu vidogo, wao walipaswa kusindikiza na kulinda hayo maandamano, sio kupiga mabomu kama walivyofanya. Basi ongezeni hata magari ya kubebea wagonjwa mahospitalini, au hata vitanda vya wagonjwa wapo wagonjwa wengi wanalala chini mahospitalini, tena hospitali za serikali, mkishindwa saidieni machokoraa huko mitaani. Acheni kuchezea pesa police, tena hizo mnazochezea ni kodi zetu.Watanzania tumechoka upuuzi wenu.
ReplyDeletePolisi ni waonevu watu wameomba na kupewa kibali cha maandamano pamoja na mkutano but still wanapigwa someni hii habari ambapo kiongozi wa polisi Arusha anathibitisha hayo http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=22575
ReplyDeleteTATIZO LA VIONGOZI WENGI WA SIASA HUKO TZ NI UMBUMBUMBU NA USHETANI!!
ReplyDeleteKATIKA HIZI NCHI ZA ULIMWENGU WA KWANZA HUTHUBUTU KUONA VIONGOZI WAKUU WA VYAMA PINZANI KUIINGIZA JAMII KATIKA MIGOGORO YA KITOTO ISIYO NA FAIDA SI KWA VYAMA VYAO WALA JAMII KWA JUMLA KWA KUANDAMANA MITAANI.
ZANZIBAR ILIKUWA HIVO HIVO, MATOKEO YAKE RAIA WASIO NA HATIA NA WENYE UPEO MDOGO WAKASHTUKIA WAMEINGIA KATIKA PATASHIKA ZA KUUMIZWA NA HATA KUPOTEZA MAISHA KWA KUFUATA BILA KUPIMA CHOKOCHOKO ZA VIONGOZI WAO, AMBAO HATIMAYE WAMEWAACHA SOLEMBA NA WAO SASA KUINGIA MADARAKANI.
UJINGA HUU MPAKA LINI?
NINI FAIDA YAKE?
IKIWA HAWA KINA MBOWE WAKO BUNGENI, KWANINI MADAI YAO WASIYAPELEKE HUKO BUNGENI?
KWANINI WATUHARIBIE AMANI MITAANI?
NINI KINACHOWAFANYA WADHANI KUWA WANA HAKI YA KUMTUMBUKIZA KILA RAIA KATIKA NJAA ZAO ZA MADARAKA? WENGINE WALA HAWAMAINDI HIZO SIASA ZAO ZA UONGO NA KWELI, WANAJALI MAISHA YAO TU.
WAONDOKE MITAANI WENDE BUNGENI DODOMA.
WATUACHIE MITAA YETU, WANAYOYAFANYA NI MATOKEO YA FIKRA ZA KUJITAJIRISHA KUPITIA SIASA TU, HAWATALETA NATIJA YOYOTE KWA MVUJA JASHO MTAFUTA RIZIKI YAKE MITAANI.
IKIWA JESHI LA POLISI TZ LINA UNYANYASAJI, WAO KINA CHADEMA MIAKA MINGI WAMEKAA BUNGENI, NINI WAMEFANYA KUBADILISHA HALI HIYO?
WATOKOMEE HUKO.
MASHETANI WAKUBWA, WASITHUBUTU KUTULETEA USHETANI WAO.
Mngengereko, Ukerewe
Much ado about nothing. It's high time the CHADEMA bigwigs or rather stalwarts found better ways and strategies to make themselves relevant.
ReplyDeleteOtherwise trying to attract unnecessary and cheap attention as away make themselves relevant will not do them any good in the long run.
There nothing with holding peaceful demonstration, but crowds begin to get out control, then it becomes a matter of disturbing the peace and it always calls for law and order.
whether it's Washington DC, London, Berlin, Tela Aviv, Moscow, Toronto, Paris, Brussels, Madrid, Lisbon, or at the Vatican.