Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager na ushirikiano wa kituo cha televisheni cha ITV leo wameweka bayana ukumbi ambapo fainali ya Tuzo ya heshima ya “Shujaa wa Safari lager” itafanyika. Ukumbi huo uko katika Hoteli maarufu na ya kisasa Paradise City Hotel.

Akizungumzia fainali hiyo ya aina yake, Meneja wa Bia ya Safari lager Fimbo Butallah (pichani juu) alisema; Maandalizi yote yameshakamilika, na washiriki wote watatu walioingia fainali watakuwepo katika hafla hiyo ambapo mshindi atatwaa tuzo hiyo ya heshima ikiambatana na kitita cha pesa shilingi milioni saba, pia washiriki wawili waliobaki watapata zawadi ya shilingi milioni moja kila mmoja.

Pia katika fainali hizo zitakazofanyika siku ya Ijumaa tarehe 21 Januari, kutakuwa na burudani toka kwa msanii bingwa wa kughani mashairi Tanzania Mrisho Mpoto, maarufu kama “Mjomba” akiwa ameongozana na bendi yake.

Bw. Butallah pia alitumia nafasi hiyo kutaja jopo la majaji wanaoendesha mchakato mzima wa “Tuzo ya Shujaa wa Safari Lager” ambao ni;-

Bw. Richard Magongo – Mkaguzi mkuu wa Mahesabu, TBL

Bw. Deogratius Rweyunga – Mkurugenzi wa Redio One Stereo na

Bw. Alex Mgongolwa – Mwanasheria na Wakili aliyebobea.

Butallah pia, alitumia muda huo kuwapongeza wananchi kwa kuweza kuonesha ushirikiano wa hali ya juu kuanzia hatua za mwanzo za kupendekeza mashujaa na hadi hivi sasa tukiwa katika mchakato wa kuwapigia kura washiriki watatu walioingia finali ili hatimaye tupate mshindi. Mashujaa walioingia fainali ni:
Ms. Mercy Shayo wa Bomang’ombe – KilimanjaroBw. Paul Luvinga wa Sinza – Dar Es Salaam.Bw. Leonard Mtepa wa Mwananyamala – Dar Es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...