Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Jaji Dan Mapigano wakati wa ibada ya mzishi iliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo jioni
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Jaji Dan Mapigano wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo jioni.viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Makamu wa Rais Dr.Mohamed Gharib Bilal,Waziri mkuu Mizengo Pinda,Jaji Mkuu Othman Chande na Mawaziri Wakuu wastaafu Joseph Sinde Warioba na Frederick Sumaye walihudhuria Mazishi hayo.
Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Jaji Dan Mapigano
Marehemu Jaji Dan Perto Mapigano enzi za uhai wake.Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Jaji Dan Petro Mapigano nyumbani kwake Mwenge jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Marehemu Dan atazikwa leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Majaji wastaafu, Thomas Mihayo, akisoma risala kwa niaba ya wanachama wa chama hicho wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu leo.
Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wa familia ya Marehemu Jaji Mapigano wakionekana ni wenye huzuni wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Jaji Mapigano katika viwanja vya Mnazi Mmoja mchana wa leo.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akitoa mkono wa pole kwa Mjane mke wa Marehemu Dan, Florence Mapigano, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo mchana.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akitoa mkono wa pole kwa Mjane mke wa Marehemu Dan, Florence Mapigano, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo mchana.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Joseph Warioba akiwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kuaga mwili wa Jaji Mstaafu,Jaji Dan Petro Mapigano.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Fredrick Sumaye nae akiwasili viwanjani hapo.
Baadhi ya Majaji wakiwa katika shughuli ya kuaga mwili wa Jaji Dan Petro Mapigano leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Poleni familia ya Mapigano. R.I.P.

    ReplyDelete
  2. Jina ni Dan Petro Mapigano!

    ReplyDelete
  3. poleni sana ndugu zangu , mwenyezi mungu hailaze mahala pema peponi
    roho ya marehemu...

    ReplyDelete
  4. pole ndugu wa familia,pole sana Maiga.jaji alikuwa akiishi mt shaaban robert(ilipo sasa TIC),Maiga alikuwa anavuka barabara tu kuja shule Bunge primary.

    ReplyDelete
  5. wa- ChirangiJanuary 20, 2011

    Natoa pole na kuomba Mola awafariji Familia na Jamaa wote wa marehemu Jaji Mapigano (RIP)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...