Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani akifungua leo jijini Dar es salaam kongamano la siku moja la Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA)ambalo lilikuwa likijadili mambo mbalimbali ikiwemo utoaji wa haki kwa wakati.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akitoa hotuba jana jijini Dar es salaam wakati wa kongamano la siku moja la Chama cha Majaji Wananwake Tanzania (TAWJA) lilikuwa linajadili mambo mbalimbali ikiwemo utoaji wa haki kwa wakati kwa wananchi.
Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani(kushoto) na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman (kulia) wakisiliza kwa makini jana jijini Dar es salaam hotuba ya utangulizi ya Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Tanzania Eusebia Munuo (hayupo pichani) ya ufunguzi wa kongamano la siku moja la TAWJA.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) wakiwa katika kongamano la siku moja la TAWJA lilofunguliwa leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani(kulia)akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania(TAWJA) Jaji Eusebia Munuo(katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kimataifa cha Majaji Wanawake Joan Winship(kushoto) jana jijini Dar es salaam kabla ya ufunguzi wa kongamano la siku moja la TAWJA.
Waziri wa Katiba na sheria Celina Kombani akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua kongamano la siku moja la Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) lilikuwa likijadili mambo mbalimbali ikiwemo utoaji wa haki kwa wakati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Majaji wanawake wenzetu, asilimia kbwa yet sisi wakina mama bado tunapigwa na waume zetu, tkishtaki hakuna haki kamili kwa mwanamke, mabinti zetu bado wanbakwa na jamii mitaani, wanuwawa, hakuna haki kamili kwenye mahakama, haswa mwenye kosa akiwa na pesa. Wakinamama vijijini bado tunabeba maji vichwani, hakuna maji safi kwa familia zetu, hakuna nishati ya kutusaidia kurahisihsa kazi zetu, ina maan hata wale wa mjini hawana hata umeme wa kuwasidia kurahisisha kazi zao. Je wakina mama majaji tunaomba mkiwa huko juu mtuwakilishe na sisi wamama wa vijijini ili tuweze kunufaika hata kuweza kupeleka mabinti zetu shule pia, ili waweze kuondokana na huu umaskini wa hali ya juu huku vijijini kwani sisi wakina mama wakulima tunalima lakini pesa ya ya akina baba kwani mashamba ni yao, na kama unavyojuwa tunakwenda hsambani wote siku akiamka vizuri lakini akitoka shamba yeye anpitia kilabuni na mimi naelekea nyumbani kushemsha maji yake ya kuoga na shungulia nyingine za nyumbani. Tunaomba muwe sauti kwetu na kutusaidia kufahamu haki zetu wakina mama.

    ReplyDelete
  2. Mwanamke akifiwa na mumewew mali zinachukuliwa, Kupigwa bado wanapigwa kama watoto wadogo, mirathi ndio hivyo mzee asipoandika will basi wasichana hawapati kitu...Je majudge mnajua hayo? Tungeni basi sheria mpya kama hazipo au zilizopo zirekebisheni .Equality....equality.....Binadamu wote ni sawa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...