Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood akiaonge baada ya kukagua hali ya vyoo katika soko la Mawenzi, Manispaa ya Morogoro baada ya kuombwa na wafanyabiashara wa soko hilo kwenda kuviona kutokana na ubovu na uchakavu ulioambatana na kuzagaa kwa uchafu wa kupindukia na kutafutia ufumbuzi wa kudumu.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood ( mwenye suti) akikagua hali ya vyoo katika soko la Mawenzi, Manispaa ya Morogoro ,baada ya kuombwa na wafanyabiashara wa soko hilo kwenda kuviona kutokana na ubovu na uchakavu ulioambatana na kuzagaa kwa uchafu wa kupindukia.
Judith Athuman ( kushoto) ambaye ni Mama Lishe wa Stendi kuu ya mabasi Msamvu, Manispaa ya Morogoro, akisikiliza majibu ya malalamiko yake na wenzake juu ya kutozwa ushuru mkubwa na Manispaa hiyo kuhusu huduma za aina mbalimbai ikiwemo ya usombaji wa taka , kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini , Abdulazia Abood ( kulia) alipotembelea Kituo hicho cha Mabasi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera Mh Mbunge, umeanza kazi ila inabidi kuwa makini maana mambo ni mengi na siyo rahisi kuyapitia binafsi yote. Leo huko sokoni, kesho hospitali, yale yale ya sokoni nako vyoo vimeoza, dawa hakuna, ukweli ni kwamba tunahitaji kuweka mifumo inayofanya kazi. Vyoo wekeni vya kulipia na vijiendeshe vyenyewe. Soko wanaotakiwa kutupa taka wakishapewa pesa zinakwenda wapi, mfumo wa ku-outsource ni mzuri. Tuamke tuige ya wenzetu tujikomboe.

    ReplyDelete
  2. Ndugu zangu wa Morogoro, binafsisha vyoo hivyo. Hakuna mambo ya kuomba msaada wa kujengewa vyoo, hayo yamepitwa na wakati. Mwache mbunge afanye mambo ya maendeleo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...