wachezaji nyota Kolo Toure na Emmanuel Adebayor wa Manchester City wakizipiga baada ya kuchezeana rafu mazoezini. Ugomvi huu inasemekana umeanza toka Desemba mwaka jana wakati Toure akiwa kama nahodha alisikika akiwalaani wachezaji wanaoongea na vyombo vya habari bila mpango. Adebayor, ambaye yuko benchi kwa muda mrefu, inasemekana alikuwa akilalamika kila mara kwamba hali si hali kwake hapo Man City, hivyo akahisi kijembe kimeelekezwa kwake.
Kocha wa Manchester City Roberto Mancini na wachezaji wengine wakiamulia zogo hilo. Leo Man City wanakipiga na timu ya zamani ya Toure na Adebayor na redio mbao zinasema Adebayor anataka kuogelea Bwawani.
Kwa chanzo cha habari na picha zaidi
BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi hakuna kitu kikubwa kuhusu hao mabwana ukiuliza utaambiwa Wanagombe Mchumba, Hivi sisi wabongo tuna nini hata siku moja ujaona Roone anapigana na Terry, Terry alikuwa amegombana na mwezake kuhusu mchumba hata siku moja hawakupigana leo haya ni yepi wenzetu hawa yaliowakuta kazi ipo wabongo.

    ReplyDelete
  2. Kama mtu umesha cheza soccer, na kuwa kambini , swala zima la kupigana ni kawaida tu , ila mambo huwa yana stay in locker room

    --mkongwe wa soka DC

    ReplyDelete
  3. Kwa taarifa yako na kama kumbukumbu kwa wengine wote, kupigana ni jambo la kawaida makazini katika nchi za magharibi. Ingawa ni kosa la jinai lakini bado watu wanapigana. Hii si tu kwa mweusi wala mweupi. Hii ni kwa kila mtu kike kiume.

    ReplyDelete
  4. wewe mtowa maoni wa kwanza wacha kasumba zako, na inaonyesha kuwa hata sio mpenzi wa mpira. Pia michuzi heading yako inadhalilisha kwa kuwa nawe unahisi ni wamatumbi tu ndio wanaopigana mazoezini.

    Nirudi kwa mdau wa mwanzo, wachezaji tele wanapigana katika viwanja vya mazoezi, nikianza kuweka list hapa nitachukuwa muda mrefu tu. Na sio kweli kuwa wanagombania mchumba kabisa.

    N'Zogbia and Andy Carroll walipigana kule newcastle. kila mpenzi wa kweli wa mpira anakumbuka 10. Joey Barton alivyompiga Ousmane Dabo wakati wakicheza Manchester City mwaka 2007, Gravesen alipopigana na Robinho kwenye Real Madrid training centre, Arjen Robben kazitwanga na Philipp Lahm mazoezini bayern, na hata Freddie Ljungberg alipigana na Olof Mellberg wakiwa katika timu ya taifa ya Sweden. Mifano ni mingi tu.

    Kwa hivyo mdau wa mwanzo, tuliza boli kwanza uwaze na kama kweli mpenzi wa mpira utajua kuwa hii sio mara ya mwanzo na haitokuwa mara ya mwisho na la muhimu zaidi sio rangi ya wachezaji bali sbabu mbali mbali wanazozijua wenyewe wagombanao.

    ReplyDelete
  5. watu wengine wanarukia rangi tu moja kwa moja, binadamu awe Rangi yoyote damu ya mwili ikimruka tu mishipa ya kupigana anakuwa mwengine anashindwak ujizuia anapigana.

    ReplyDelete
  6. Hakuna kinachoniudhi kama mtu asojua jambo kijifanya anajua na kujifanya expert na kuleta mawazo yake finyu hapa, yote tu kwa kuwa wakuja sasa yuko ulaya (uk).

    Mfano ni huyo jamaa wa mwanzo hapo juu. Kwanza terry na rooney hawawezi kupigana mazoezini kwa sababu hawachezi timu moja (labda wakiwa katika timu ya taifa) pili terry hakuchukua mwanamke wa Wayne rooney bali alichukuwa mwanamke wa Wayne Bridge (unaona tafuti ya jina mdau wa mwanzo?). Terry na Wayne Bridge hawakupigana kwa sababu (tena) iliporipotiwa habari hii Wayne Bridge alishaondoka chelsea!!!! hizo ni fact.

    Wachezaji mpira wanapigana sana tu katika kambi zao za mazoezi, ukiwa ni mtu unaefuatilia mchezo wa mpira utakuwa umewahi kusikia tu vituko hivi, na vinatokea kwa wachezaji wote bila ya kujali rangi au asili yao. Na hiyo pia ni fact.

    ReplyDelete
  7. Two points:

    1. Brother michuzi kichwa cha habari ni kibaya sana na kinadhalilisha wamatumbi wote, kwa sababu (reading between the line) unaonyesha unajaribu kusema kuwa ni wamatumbi peke yao wanaopigana wakiwa katika kambi za mazoezi, jambo ambalo sio kweli kabisa. Kunatokea wachezaji wa timu mbali mbali katika mabara yote kupigana, ni jambo la kawaida sana. (mdau mmoja hapo juu ameweka list fupi tu lakini list ni kubwa sana)

    2. mdau wa kwanza Wed Jan 05, 04:35:00 PM ujumbe kwako ni get your fact straight kabla ya ku-comments. Umeongea utumbo mtupu.

    Mdau in exile

    ReplyDelete
  8. Hapa nadhani Adebayor ndio atakuwa aliyeanzisha ugomvi,ni bishoo sana mimi aliniudhi alipoamua kustaafu timu ya taifa kisa eti walivamia kule Kabinda,Angola. Aliamua kustaafu timu ya taifa wakati anaendlea kucheza klabu yake ya Man City, wakati timu yake ya taifa ndiyo iliyomtangaza kipaji chake akajulikana na klabu za Ulaya, kwanza mpira wake umeshaanza kuisha hana lolote analofanya zaid ya kuingia kama substitute au kutopangwa kabisa. Nawe Michuzi mbona siku hizi huandiki tna habari za timu yako ya bwawa la maini? au kwa kuwa sasa bwawa linazidi kukauka?

    ReplyDelete
  9. mpirani kawaida mambo haya bwana..ukiwa mchezaji mpira unajuwa kinachoendelea.

    ReplyDelete
  10. michuzi TUTAKE RADHI ndio nyie kila cha mtu mweusi kibaya hivi mmeshawahi kukaa na hawa wazungu mkajua tabia zao,ugomvi jambo la kawaida kwa kila tabaka, haijalishi ni rangi gani UMENIKERA

    ReplyDelete
  11. MDUANZI U.KJanuary 06, 2011

    BROTHER MICHUZI KICHWA CHA HABARI KINADHALILISHA WAAFRIKA..SI KWAMBA WAZUNGU HAWAPIGANI..KILA TEAM IWE YA PREMIERSHIP AU LIGI YOYOTE MAMBO HAYO HUTOKEA NA HAITOKEI KWA WAAFRICA TU..MFANO MZURI ROBIE KEANE WA SPURS ALIWAHI KUZITWANGA EDGER DAVIDS NA KUMTOA MENO MAWILI MAZOEZINI,ANDY CARROL WA NEWCASTLE ALIPIGANA NA KUMVUNJA TAYA BEKI STEVEN TAYLOR MWAKA JANA TU HAO SI WAMATUMBI,ROY KEANE AKIWA MAN UNITED ALISHAWACHAPA SANA WENZAKE MAZOEZINI NA ALIKUWA AKIOGOPWA NA KILA MCHEZAJI WA MAN U KA KUWA ALIKUWA FUNDI WA KARATE..HIVYO ADEBAYOR NA KOLO SIO TOFAUTI..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...