Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Alex C. Massinda (wa pili kutoka kushoto) akiwa na Mhe. Percy Paris (wa tatu kutoka kushoto), Waziri wa masuala ya Afrika na wakazi wenye asili ya kiafrika wa Jimbo la Nova Scotia. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Lorne Berndt wa Ofisi ya Uwakilishi wa Nova Scotia jijini Ottawa, Richard Tibandebage na Joseph Sokoine wote maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, na Wayn Hamilton, Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya masuala ya Afrika na wakazi wenye asili ya kiafrika wa Nova Scotia.

Balozi Massinda alikutana na Waziri Paris na ujumbe wake ambao walifika Ubalozini kuzungumzia tamasha la kuenzi mila na utamaduni wa Mwafrika litakalofanyika mnamo Septemba 2011 jijini Halifax, Nova Scotia.

Pamoja na maelezo kuhusu tamasha hilo, Waziri Paris alielezea jinsi mkutano wa "African Diaspora Heritage Trail" ambao ulifanyika nchini Tanzania mwaka 2009 ulivyotoa changamoto kwa watu wenye asili ya Afrika walioko ughaibuni kutambua umuhimu wa Afrika Mashariki kama chimbuko lao sawa na Afrika Magharibi.

Kwa hiyo wenyeji wa tamasha la Halifax wangependa Tanzania ishiriki na kuonyesha utamaduni na sanaa zake kwenye tamasha hilo. Waziri Paris aliomba Balozi Massinda asaidie kuhamasisha ushiriki wa Watanzania wanaoishi Canada pamoja na taasisi za Tanzania. Kwa upande wake Balozi Massinda aliahidi kuyafanyia kazi maombi hayo.

Aidha alishauri Waziri Paris na ujumbe wake wapange kuonana na Mabalozi wa nchi nyingine za Afrika Mashariki na kuwaalika nao washiriki kwenye tamasha la Halifax.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...