Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal akiwa ameshikilia Reki kuvuta taka zilizozagaa kwenye uzinduzi wa Usafi wa Mazingira ya Miji na Majiji ya Tanzania aliouzinduwa rasmi katika Viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam leo. kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk. Terezya Hovisa.


Nashukuru kama Makamu wa Rais Dr Bilal amekubali mualiko wa kushiriki siku ya usafi kwa kushika fagio na kuonesha "mfano" kwa kufagia. Lakin mbona waandaji shughuli hii ya Mzee wamempeleka sehemu ilio safi? Nadhani wangempeleka kama vile manzese, soko la Tandale akaone hali halisi ilivyo na ajue sababu za kushindwa kuweka mji au jiji katika hali ya usafi unaoridhisha. Wote tunakubali kinga ni bora na rahisi kuliko TIBA ambayo hatahivyo haipo... Milipuko inapotokea wanao athirika ni wakazi wamaeneo yasiweza kusafishika. Kisa Manispaa haina uwezo, ingawa wanakusanya fedha za kuzoa taka iwe kutoka kwa wafanya biashara sokoni au majumbani, kuanzia 2000/- hadi 3500/- kila mwezi... fedha hizi zina kwenda wapi? na kusema kweli haziwezi kununulia magari yakutosha ya kubebea taka zinazo zalishwa jiji la DSM.
ReplyDeleteLabda kwa kutumia mikokoteni na hapo ndio mtihani, kwani taka hutupwa katika matrela yanao egeshwa na manispaa na wasukuma mikokoteni hujatupa taka hapo, cha kushangaza, matrela hayo yanajaa hadi kufurika na taka kuenea sehemu kubwa kama dampo bila trela kuondolewa. Lakini hao hao serikali za mitaa ni wepesi kuja kamata wenyenyumba 'uswahilini' na kuwatoza faini eti kwa mazingira machafu, na ya kuchekesha ni kamata hii si endelevu, je tuko sirias kwa jambo la kuweka JIJI SAFI? angalieni mitaro inavyojaa taka hadi aipitishi maji mvua inaponyesha, je wajibu wa nani? mhhhh ina maana hadi aje kiongozi kutuonesha jinsi ya kusafisha mitaro humu mitaani kwetu?