UMOJA WA WATANZANIA WAISHIO "NEW ENGLAND STATES" (Massachusetts, Connecticut, Rhode Island, Maine, New Hampshire, Vermont pamoja na New Jersey)

NCHINI MAREKANI, TUNAUNGANA NA WATANZANIA POPOTE

WALIPO DUNIANI KWA KUTUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA WANANCHI WENZETU, HASA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WALIOJERUHIWA, TUNAOMBOLEZA KWA WALE WOTE WALIOPOTEZA MAISHA YAO KWENYE MILIPUKO YA MABOMU KATIKA KAMBI YA JESHI MAENEO YA GONGO LA MBOTO, DAR-ES-SALAAM.

TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AWAPUMZISHE MAREHEMU WOTE MAHALI PEMA PEPONI. TUTAZIDI KUWAOMBEA WALE WOTE WALIOJERUHIWA NA KUWATAKIA KILA LA KHERI WAPONE HARAKA.

WATANZANIA WOTE TUISHIO PEMBE HII YA MASHARIKI MWA MAREKANI TUNACHUKUA NAFASI HII KUWAPONGEZA WANANCHI WENZETU MLIOKO NYUMBANI, VYOMBO VWA WATU BINAFSI, TAASISI NA MASHIRIKA MBALIMBALI, NA PIA VYOMBO VYA SERIKALI, KWA UPENDO NA MOYO WA KUJITOLEA MLIOUONYESHA

KATIKA KUWAHUDUMIA MAJERUHI, KUWAFARIJI WALE WOTE WALIOATHIRIKA NA WASIOKUWA NA MAKAZI YA KUISHI, WALIOPOTELEWA NA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI, KINAMAMA NA WATOTO, NA HASA KATIKA KUSHIRIKI KWENYE MAZISHI YA WENZETU WALIOPEZA MAISHA YAO.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.

New England Umoja Foundation, Inc.

www.newenglandumoja.net

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wabongo kazi kweli...New Jersey ni New England kweli au mmeshaihamishia huko kibongo bongo...Don't call it New England states kama mnajumuisha na New Jersey...New Jersey ni Tri State...Tulishaishigi huko marekani hivyo msitudanganye..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...