Washiriki wa shindano la Kisura Tanzania 2011 wakiwa katika picha ya pamoja na Mganga mkuu wa Manispaa ya Ilala Asha Mahita katikati na aliyesimama nyuma ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana Meshack Shimwela.Rais wa Kampuni ya RBP Group Rahma Al- Kharoos akimkabidhi mmoja wa wauguzi Bi.Kuruthum Mohamed kwenye wodi ya Wazazi msaada wa chakula,kushoto kwake ni mwandaaji wa shindano la Kisura Jully Urio na kulia kwake ni mshiriki wa kisura 2011 akishuhudia tukio hilo. Rais wa Kampuni ya RBP Group Rahma Al- Kharoos ambaye pia ni mlezi wa kambi ya washiriki wa Kisura 2011 akizungumza mbele ya waandishi wa habari ndani ya hospitali ya Amana,Ilala jijini Dar,kulia kwake ameambatana na Mwandaaji wa shindano la Kisura 2011 Jully Urio wakati walipowasili hospitali hapo kwa ajili ya kutoa misaada ya vitu mbalimbali,ikiwemo chakula kwenye wodi ya wazazi pamoja na waathirika wa mabomu.Bw. Fabi Kishado akishusha chakula kwenye gari na kuwapatia washiriki wa kisura 2011 kwa ajili ya kukigawa kwa wagonjwa kwenye wodi za hospitali ya Amana,jijini Dar jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mrembo wa kimasai upo wpai au kashakimbia , maisha ya mjini yamemshinda !! lol kwah kwah kwah kwah

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...