Rais Jakaya Kikwete (katikati) akisalimiana kwa furaha na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu( SUMATRA) Bw. Israel Sekirasa mara baada ya kuhitimisha ziara yake Wizara ya Uchukuzi leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoshuhudia ni Katibu mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Eng. Omari Chambo (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa wizara ya Uchukuzi muda mfupi baada ya kuwasili katika makao makuu ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ambapo alizungumza na uongozi pamoja na wafanyakazi .
Naibu waziri wa Uchukuzi Dkt. Athuman Mfutakamba (kulia) akizungumza jambo na Rais Jakaya Kikwete katika ukumbi wa wizara ya Uchukuzi leo jijini Dar es Salaam . Rais Jakaya Kikwete aliitembelea Wizara ya Uchukuzi ili kupata taarifa ya utendaji kazi wa Wizara, Mamlaka, Taasisi na Idara zilizo chini ya wizara hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Watendaji wa Wizara, Idara, Mamlaka na Taasisi za Wizara ya Uchukuzi leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amewataka viongozi hao kuzifanyia kazi changamoto zinazoikabili wizara hiyo zikiwemo uboreshaji wa huduma za reli, usafiri mijini,uboreshaji wa huduma za bandari, matengenezo ya viwanja vya ndege nchini na migogoro ya wafanyakazi.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. What the heck is going on? Mbona President ana furaha sana huko mawasiliano na uchukuzi?

    ReplyDelete
  2. tabasamu ni sehemu ya maisha ya mkuu wetu ya kila siku

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...