Habari Mjomba Issa,
Kwa majonzi tunaungana na Wasanii, washereheshaji , wana burudani na Watanzania wote kwa ujumla kuomboleza kifo cha wasanii wa Five Stars Modern Taarab, aidha tunawatakia wapone haraka majeruhi wa ajali mbaya iliyotokea. Poleni sana na wote tunawatakia subira – “Innah lau maswabilina – kila mwenye kusubiri yupo karibu na mwenyezi mungu”
Mjomba jana 22/03/2011 ilikuwa ni siku ya heri sana kwa wanachama na wapenzi wa Laxmi Darts Club kwa kukabidhiwa jezi bin uzi toka kwa wafadhili hapa Tukuyu (Champion) na pia Darts Board na Mishale toka kwa mfadhili wa Dar-es-salaam ambaye hakutaka kutaja jina lake wala thamani ya vifaa hivyo.
Hii yote ni kutokana na wewe mjomba kuandika habari zetu katika Globu ya Jamii na watu kujitokeza kutusaidia, hivyo shukurani za pekee ni kwako Mjomba Issa Michuzi kwa kututangaza. Ni imani yetu kuwa wengi wataendelea kutupa sapoti wanyambala wa Tukuyu katika vifaa. Shukurani wote.
Mwisho ni swali kwa wenye taarifa juu ya Club maarufu hapo Dar Kishamapendo Darts Club (Club Kongwe) ya pale Ilala je bado ipo? tupeni contacts zao tuje kukipiga wakati wa Pasaka.
Habari na picha
Mjomba Juma wa Globu ya Jamii, Tukuyu
Kwa mawasiliano: laxmidarts.club@gmail.com
Katibu, Mwakatobe 0787 087 955
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...