Wananchi wakikinga vikombe kupatiwa dawa na
Mchungaji Ambilikile Mwasapile kwa bei ya sh. 500 tu
Mchungaji Mwasapile akihojiwa na waandishi
Wakubwa wakijisogeza Monduli
Juu na Chini msururu wa magari na watu kuelekea
Loliondo kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile kupata tiba ya jero

MAELFU ya watu, wakiwemo vigogo wa serikali, wabunge na wafanyabiashara wakubwa nchini, wamefurika katika Kijiji cha Samunge Tarafa ya Sale wilayani Ngorongoro kupata 'dawa ya maajabu ya Mungu' inayodaiwa kutibu magonjwa mengi sugu ikiwamo Ukimwi.

Helkopta za wafanyabiashara na magari zaidi ya 1,000 yakiwamo magari ya serikali, binafsi na mashirika ya kimataifa ikiwamo Umoja wa Mataifa (UN) na Jumuiya ya Afrika Mashariki, yamefurika katika kijiji hicho kilichopo umbali ya takriban kilometa 400 kutoka Jiji la Arusha.

Dawa hiyo, inatolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile (76), ambaye anasema alioteshwa na Mungu kuitumia kutibu tangu mwaka 1991.

Mchungaji Mwasapile ambaye alifanya mahojiano na Mwananchi Jumapili nyumbani kwake wakati akiendendelea kutoa dawa kwa wagonjwa wake, anasema ndoto hiyo aliendelea kuota mara kadhaa hadi Agosti 26 mwaka jana alipoanza rasmi kutibu.

Anasema dawa hiyo inatokana na mti aina ya mugariga na yeye pekee ndiye anaweza kukupatia na kunywa kikombe kimoja pekee na ukinywa tu inaanza kazi ya kutibu maradhi sugu ya ukimwi, kisukari, pumu na saratani.

Mchungaji Mwasapile anasema gharama za dawa hiyo ni Sh500 tu na dozi yake ni kikombe kimoja tu na hairuhusiwi kurudia kuinywa. Kabla ya kukamilika mchungaji huyo huiombea dawa hiyo na kuichemsha katika maji safi.

“Mungu ameniotesha kutoa dawa hii kwa Sh 500 aliponiambia hata mimi nilishangaa. Kwanza aliniambia niwape watu wapone saratani, kisukari, pumu na magonjwa mengine na baadaye akanionyesha kuwa dawa hii niwape hata wagonjwa wa ukimwi na watapona,“ anasema Mwasapile.

Habari hii imeandikwa Mussa Juma
na Daniel Sabuni, Loliondo.

Picha zote kwa hisani ya Aman Masue.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

 1. Bongo ukiwa masikini ni kujitakia, ukizusha una dawa ya ukimwi hata kama ikiwa mavi watu watakula.. eti Mungu kamwambia auze sh 500, mbona manabii waliokuwa na uwezo wa kufufua watu na walifanya hivyo bure..(500 mara 1000) laki tano bila matata mfukoni kwa siku moja lazima na mie niache kazi yangu nije, jamaa baada ya mwezi mmoja ni tajiri wa kuendesha ma HUMMER kama wahubiri wenziwe wanauza maneno ya mungu...

  ReplyDelete
 2. Yale yale ya Kinjekitile Ngwale na dawa ya "maji maji" na bado watu wanaingia line.Ha ha ha ha ha ha...Mungu naomba unisamehe mimi mwenye dhambi. Yesu alisema mmepewa(kipaji cha uponyaji, ufufuaji nk) bure na nyinyi toeni bure.Inakuwaje huyu mchungaji atoze pesa kuponyesha wagonjwa wakati hakununua hiyo dawa? Wenye macho na waone,wenye masikio na wasikie,wenye akili na wazitumie kuchanganua mambo.Amina.

  ReplyDelete
 3. Kwa maelezo niliopata, inachukua masaa 8 safari kutoka mjini Arusha hadi kijiji cha Samunge kwa Mchungaji huyu anaetibu kwa maji yaliochemshwa na mziziz anaojua yeye kwa kuoteshwa. Swali langu, watu wanaofurika hasa wale vigogo wa serikalini na mashirika ya umma, wanasafiri wakitumia gari za serikali na ofisini mwao, je hizo ni safari ya kazi au binafsi? kama magari na mafuta yanayotumika ni ya kazini basi wanadhulumu wananchi maanaa hata watu wa kawaida wangependa kwenda kutibiwa lakini uwezo wakufika huko hawana kwa vile nauli na fedha za mahitaji muhimu mbali na hiyo dawa ni ngumu kupatika, kwa hivyo wakubwa, na viongozi waliofaidika kwa tiba za mchungaji huyu wafanye utaratibu wakusaidia wananchi nao wapate usafiri wa kufika na kupata tiba hasa ya ukimwi na magonjwa sugu mengine na hilo litawapunguzia mzigo serikali. Kwani mambo mazuri watu wote wanayataka hasa afya njema..

  ReplyDelete
 4. afadhali hatuna low season this year

  ReplyDelete
 5. Kama huyo anaweza kumobilize watu kiasi hicho! kwa nini iwe vigumu kwa CHADEMA. Ni matumaini ndiyo yanayowavuta watu.
  Miaka ya kupigania uhuru, Nyerere katika hotuba zake alikuwa analeta matumaini kwa wanainchi na ndiyo maana alivutia watu kiasi mkoloni alishindwa kuwazuia. Hili ni SOMO kubwa.

  ReplyDelete
 6. JAMANI CHONDE CHONDE, MUNGU AMETUKUMBUKA WATANZANIA. MSHUKURUNI MUNGU. MSILALAMIKE. 500 HATA CHIPS HUPATI. NENDENI MKAPONE NYINYI NA NDUGU ZENU. MUNGU ANAWATUMIA WACHUNGAJI WATUMISHI WAKE. MSIWAKEBEHI

  ReplyDelete
 7. tatizo vichwani mwa watanzania ni haiwezekani.... tupo sawa kwani hatuwezi kitu na tutaendela kuwa hawezi... ugumu upo wapi mtu kugundua mti shamba unaotibu maradhi mbalimbali.. hata huo ukimwi mnaosema hautibiki kuna watu wanatafuta dawa.. nina hakika watanzania wakisikia kuna mtu ulaya amegundua dawa ya ukiwmi tutaamini bila hata kuuliza ni dawa inayotengenezwa na nini? watu waitumie hiyo dawa ya huyo mzee halafu waseme kama imewasaidia au lah! siyo kubisha tu hata kama huna facts zozote, halafu ths 500 ni kitu gani ndugu zangu.... huyo mzee anatoza hiyo hela imuwezeshe kuishi tu, mbona akina Ndodi dawa zao ni laki tatu na hatusemi? kikubwa ni kujaribu ndiyo tuseme

  ReplyDelete
 8. Anaweza sababisha maelfu ya watu kuja TZ kupata matibabu. Hii habari sio ndogo, ukiongea na watu walio Arusha ndio watakupa habari zaidi kuhusu mchungaji huyu. yote iwe kheri

  tembeatz.blogspot.com

  ReplyDelete
 9. Naamini comment yangu pia itapita kwani haiko mbali sana na za walotangulia hapo juu. Wakati wenzetu washatuletea matibabu ya kimo na radiation kwa kansa mbali mbali, ATV drugs za kubabiliana na ukimwi nk - madawa ambayo formula zake ziko documented, na yataendelea kuwepo mpaka dawa bora zaidi zipatikane; wengi wetu bado wanakubaliana kabisa na habari ya dawa za kuoteshwa. Eti pia Mungu anamwambia aweke siri, na auze bei gani! Huyu mganga ana cover nzuri, safi tu machoni pa wengi ya "uchungaji mstaafu", hivyo kwamba ni mtu clean. Ndo maana viongozi wa dini wengi tu mielekeo yao na ya waganga haviko mbali sana kivile. Kuwa mfanyabiashara mkubwa au kigogo wa serikali au mbunge isiwe sababu ya kukufanya uamini anavyoamini yeye. Inasikitisha sie bado kiujumla ni taifa la watu tunaoamini katika ushirikina wa namna nyingi nyingi tu ndo maana tunadanganyika kirahisi. Kama walokwenda shule wanarubunika kirahisi hivi, vipi ambao dunia inavyokwenda leo kwao ni giza nene?

  ReplyDelete
 10. Nafikiri kikubwa watanzania wawe makini na ugonjwa wa ukimwi. Hamna dawa aisee ni pyscological torture tu..

  Hii Tena itachangia maambukizi yawe makubwa,na juhudi za sisi wanaharakati kuutokomeza zififie.

  Hamna dawa jamani, jitahidi kussiwe na maambukizi mapya na watu wachek afya zao itawasaidia ku plan maisha zaidi na kuwa makini

  ReplyDelete
 11. Mimi nitakuja kufungua mama ntilie tu naona nitapata faida nyingi kuliko hata huyo mchungaji.

  Nitauza chakula, maji na juisi, jee wadau munaonaje?

  ReplyDelete
 12. VINGUNGUTIMarch 06, 2011

  Hawa wote ndiyo utawasikia wakiwa pub/bar wanalewa wakisema "yule mtu mwenyewe hata shule hajaenda..." hawa ndiyo wasomi wa Tanzania hawa. Ingawa hii pia itasaidia kujua ni kigogo gani mwenye ukimwi. Hawa wote wataliwa na hawatapona ukimwi wao, na mchungaji atasema yale yale ya karne zote..."hukupona kwa sababu huna imani ya kutosha na bwana yesu"

  ReplyDelete
 13. wewe kapate dawa uendelee kula ovyo, kisukari hakina dawa ni life style.

  ReplyDelete
 14. Shuhuda atoe data humu

  ReplyDelete
 15. Umaskini si mali tu bali ni ukosefu wa akili.

  ReplyDelete
 16. Swala ni kusubiri uthibitisho wa kama kweli dawa hiyo inaponya sio kubeza kama majuha au walevi wa gongo. Wenzetu wakisikia kitu wanafanya uchunguzi ili kuthibitisha lakini sie ni kutoa maneno ya kilevi-levi in almost everything.

  ReplyDelete
 17. kwenye picha nimeona gari moja ni SM 3178,tunapiga kelele maisha magumu huku watu wanatumia magari ya serikali kwa shughuli zao binafsi.

  ReplyDelete
 18. Watu wanaosikitisha zaidi kuliko hata huyo mganga, ni wenzetu wanaokuja kwenye mtandao hapa, kwangu mimi ikiwa dalili ya kwamba ni waelewa, kwani wanajua kublog, kutoa maoni yao kwenye mitandao humu, lakini uwezo wao wa kiakili unadhihirika wanavyosisitiza eti tufanye uchunguzi kwanza! Inasikitisha sana. Uchunguzi gani wewe?? Enzi za upumbavu wa dawa za kuoteshwa zilishapita. Hata hawa wenzetu walotuletea internet hawakuoteshwa jamani - ni elimu dunia, uchunguzi, sayansi, maabara n.k Sasa hapo ndo mjue mambo ya ngozi za albino sijui zinasaidia vitu gani, hayataisha katika kizazi chetu hiki. Wajinga wametuzidi sana idadi

  ReplyDelete
 19. waliopimwa baada ya kunywa wakapona wajitokeze vinginevyo hili ni changa kama michanga mingine.
  Poleni wagonjwa

  ReplyDelete
 20. Watanzania wana tabia ya kukebehi wachungaji. Waganga wako kibao lakini hakuna anayewapinga.

  Watanzania wanapenda uchawi na wanafikiri kila kitu ni uchawi.

  ReplyDelete
 21. naona watu humu mpo brain washed na western technology, munaamini sana sijui ati dawa imepelekwa maabara etc ndo unaiamini? zamani watu wameishi longer sababu ya kutumia miti shamba, magonjwa haya yameletwa na hayoo hayo mnayoyangangania ya maabara, mwache babu wa watu auguze, km kweli au uwongo miti shamba haina madhara kama Ampicilin etc! Watu mkienda muhimbili ndo mnaamini eti, tubadilike na kuanalyse current situation na past uone ni wapi tumekuwa na magonjwa ya ajabu! kma unaumwa nenda ukatibiwe na utapona msichonge tu sababu mdomo mnao!

  ReplyDelete
 22. All to all..jamani mimi ninatoa ushahidi ulio wa kweli kabisa,Japo na mimi imani inakuja na kuondoka.Nina Bint wa wifi yangu mwenye umri wa miaka 26 ambaye ulikuwa tunaishi naye hapa Dar,na mama yake ambaye anaishi Arusha mjini..Wifi yangu huyo ameathirika na virusi vya ukimwi na tayari alikwisha anza kutumia Dozi ya kuongeza CD4..Lkn hali yako bado haikuwa ya kurudhisha,ndio mama yake aliponishauri kwamba tumpeleke kule Arusha na yeye akaijaribu hiyo Dawa,Mungu mkubwa nilipomfikisha Arusha nikamuachia wifi yangu Bint yake na mimi nikarudi zangu dar,kesho yake Wifi yangu akafunga safari kwenda huko Loliondo kwa Huyo Babu,alifika salama na mungu mkubwa hakukuta foleni,babu akampokea vizuri na kumpa Dawa yake,na pia alimuambia aache kutumia dawa zile alizopewa huku dar ambazo ni dawa za kurefusha maisha yake.Tokea amekunya dawa huyo Leo zimetimia siku 9,na kabla hajanywa ile dawa babu alimwambia baada ya kunywa dawa hii unakaa muda wa siku saba kisha unaenda kupima hospital,ndio hiyo siku ya saba ilipotimia,kiukweli kila mtu alikuwa na shauku ya kutaka kujua ukweli wa hiyo dawa,Wifi yangu na binti yake walienda hospitali ya mount Meru kwenda kuchukua vipimo...Majibu yalipotoka hakuna aliyeamini maandishi yaliyoandikwa kwenye cheti chake.Yaani ( H I V NEGATIVE )tena kwa muhuri.Hiyo ni siku ya saba ambayo yule babu amesema,Bado hakuna aliyeamini tunasubiri bint apate nguvu zaidi aje huku dar kwa vipimo zaidi,hivi hapa ninavyandika maelezo haya tuna siku ya tisa (9)Tokea anywe dawa ya babu huko Monduli.

  wasalam Mdau. Dar es Salaam.

  ReplyDelete
 23. Waganga wa kienyeji ndio wanaomshambulia mchungaji huyu kwa kuwa amewaharibia soko.

  ReplyDelete
 24. mwachen babu atoe dawa wa kufanyiwa maombi ya babu awahi ili na kiatu chako kiweze kuvuliwa .big up kwa babu

  ReplyDelete
 25. Je, "Nayakuponya Vipofu?

  ReplyDelete
 26. sioni shida kwa afisa wa serikali kutumia gari la office kwenda kupata matibabu yenye uhakika mahali popote ndani ya nchi. tena akipona itakuwa imeokoa kiasi kikubwa cha pesa ya mtazania ambayo ingetumika kugharamia matibabu hayo nje ya nchi.

  araway

  ReplyDelete
 27. Ningependa serikali au watu waliohakikisha dawa hiyo watoe ushuhuda ili watu wengi wasije wakaaangamia kwa kuacha dawa zao. Na kama ni kweli mzee awezeshwe aweze kuwatibu watu wengi wenye maradhi hayo. Wanataaluma wa Chuo cha Muhimbili, wa dawa mbadala mko wapi kutushauri, mnakalia kubishana tu ili mradi mapaka mpate maslahi ndio mhakikishe, wakati mnalipwa na serikali kuhakiki mambo kama hayo, fanyeni kazi bwana!

  ReplyDelete
 28. Its true jamani.

  ReplyDelete
 29. aminini jamani hii kitu siutani wala uongo nikitu ya ukweli mimi naandika hapa kama kuwapa watu ushuhuda kuwa ukimwi unapona. mimi binafsi kwanzia ninywe hii dawa nina miezi miwili nilikuwa na HIV positive lakini hamuwezi amini nimepima mara 7 kwa sehemu tofauti kwa sasa nina negative nimaajabu lakini nikweli. nauli nikubwa lakni msijali katika hilo. imani yako ndio inakuponya. lakini dawa ipo na inaponya. aminini ninalo waambia sijaadisiwa ni mimi mwenyewe.

  ReplyDelete
 30. WEWE KAMA UNA IMANI HABA WAACHE WANAOAMINI WAENDE KUPATA UPONYAJI. AS LONG HAJAWALIPIA NAULI. KATIBA YETU INARUHUSU WATU KUAMINI KILE WANACHOPENDA

  ReplyDelete
 31. jaman ni kweli kweli kweli kweli watu wanaponywa nina jirani zangu ndugu wameponywa kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa sasa kama huamini basi hulazimishwi kabisa hata sijui niseme nini sina haja yakuandika gazeti hapa ila ndio hivyo. MDAU KUTOKA ARUSHA

  ReplyDelete
 32. Jamani acheni kudharau kila kitu, vingine ni neema kwetu kwani Mungu uwapenda watu wake

  ReplyDelete
 33. lile liSUAREZ sijui SUAREZ silipendi nuksi kweli lilitunyima ushindi dhidi ya GHANA.

  ReplyDelete
 34. jamani watanzania wenzangu huu si wakati wakubisha na kuponda dawa anayetoa huyo mchungaji niwakati wakumshukuru mungu kwakuwezesha dawa kupatikana kwani magonwa haya yalikuwa hayatibiki haswa huu ukimwi ambao umemaliza watu ambao hakuwa natiba wataalam duniani wanaumiza vichwa kuvumbua dawa inatakiwa kila mmoja apige magoti nakumshukuru mungu kwakuwezesha dawa kupatikana na azidikumlinda huyo mzee kwani kuna wengine hawapendi hii habari kwakuwa wanajua masilahi yao itapungua sasa ni serekali itafute namna ya kumlinda huyo babu asije akauwawa na serikali itavute namna ya kuwasaidia wale wagonjwa waziokuwa na uwezo serikali itafute jinsi ya kuwasaidia usafiri na huyo babu mazingara yake yawekwe safi sio wakati wakubeza kila kitu kama wewe unabeza au uwamini kwa sababu huumwi wacha wanaumwa waamini hujalazimishwa kuamini kweli binadamu hana jema mnasubutu kulalamika kwa bei ya shilingi mia tano kweli kwa ugojwa uliokosa tiba duniani? hata ingekuwa mamilioni bado sio kitu kwani uhai uwezi kulinganisha na dhamani ya hela njua waganga wakienyeji hwatapenda habari hii lakini kama mungu ameamua dawa ipatikane sasa hakuna atakayeweza kuzuia labda huu ndio wakati mungu ameamua kutoa dawa kupitia kwa huyo mhungaji bwana apewe sifa amina

  ReplyDelete
 35. ZABRON L.MLIMBILA XOX 1131 MOSHI zlmlbila@yahoo.com

  Jamani,napenda kuchukua nafasi hii,kumshukuru Mungu,kwa kutuletea Mchungaji Mstaafu Ambilikile Mwasapile,ili atoe uponyaji, mimi nilikuwa nasumbuliwa na Kisukari kwa miaka kumi na moja sasa,Lakini Jumamosi ya Tarehe 5.3.11,ndiyo mwisho wa Tatizo la SUKARI,baada ya kupada dawa kutoka kwa Mchungaji huyu.Nimehuzunika sana na Habari za Kakobe kuwa anampnda mzee hutu,na anadai anataka waumini wake waombe na kumsambaratisha,nasema atashindwa na huduma ya mzee yule itadumu kwa vile ametumwa na MUNGU.
  Ndugu zangu wasomaji,nawashauri kuacha ubishi,nendeni kupata huduma ya uponywaji.

  ReplyDelete
 36. Mzungu akigundua dawa huyo inakuwa sawa? hivi kile kitengo cha tiba asili pale muhimbili ni cha nini kama hamtaki kuamini? Ninyi maprofesa kazi yetu ni kusoma vitabu na kukariri dawa kwa ajili ya maradhi, ukweli ni kwamba ninyi siyo wataalam wa utengenezaji dawa.

  Nilikwenda china, kule wenzetu hata katika hospitali kuna maduka ya dawa za asili na hizo za kidhungu, ukimaliza matibabu unaulizwa utatumia zipi. Sasa jamani babu kaoteshwa mwacheni aendelee na kazi, ninyi kaeni na umasikini wenu wa roho na akili.

  Na huyo aliyuliza kuhusu magari ya serikali, hivi juzi Katibu Mkuu kaagiza watu waende, wangekwenda kwa ungo?pambafu woteee mnaopinga na kusema semba hovyo hovyo tena mkome mkome kabisa! Hadi hapo hali ya hewa saffffffffffffffffffiiiiiiiiiiiiiii

  ReplyDelete
 37. Jamani nafikiri hapa tunazungumzia imani. Kam huamini usiwakatishe tamaa wengine waache waende bwana. Unakumbuka hata Musa alipoambiwa na Mungu achonge nyoka wa shaba na kila atakaemwangalia ikiwa ameng'atwa na nyoka atapona. Wale walioamini walipona na wale waliopuuza walikufa kwa kung'atwa na nyoka. Habari ndo hiyo, ukiamini utapona nenda usijali kuwa kama Tomaso.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...