Dereva wa Pikipiki akiwa amevalia jaketi maalumu la matumizi ya kazi yake , baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya ( watatu kutoka kulia) na wa pili toka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh. Saidi Mwambungu
Baadhi ya Askari wa Usalama Barabarani wa Mkoa wa Morogoro wakijumuika pamoja na waendesha pikipiki na wamiliki wao , kwenye mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya ( hayupo pichani) wa kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva hao
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Fatma Mwassa, ( wa kwanza kushoto) akipata maelezo ya ukarabati wa kisima cha maji katika Kijiji cha Melela, kutoka kwa Diwani wa Kata hiyo , Christopher Maarifa ( wenye mavazi na njao) kupitia ufadhili wa Kampuni ya Uhandisi wa Ujenzi wa Barabara ya CGI. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo , Radisay Ilic ni wanne kutoka kushoto.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Fatma Mwassa, akisalimia na wanafunzi wa shule ya Sekondari Melela, alipowatembelea kukagua maendeleo ya shule. Picha zote na mdau John Nditi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hayo mapikipiki ni matatizo tuu. yanajeruhi, kuua na kuleta vileama kila siku. In fakti gharama za madhara yake ni kubwa mno kwa taifa. Futa pikipiki na leta mabasi makubwa kila eneo.Hakuna short-cut kwenye maendeleo. asikudanganje mtu. Uliona nchi gani iliyoendelea eti inatumia mapikipiki kama njia ya usafiri wa umma. Uza ma shangingi yote nunua mabasi makubwa kila mtu atasafiri raha mustarehe. Ongeza/panua barabara.
    Hii ni fakti...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...